wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, January 06, 2009

TweetThis! Albino Tanzania kupewa simu za kukabiliana na mauaji

Hatimaye jamii ya albino inatarajia kupewa simu za mkononi ili kuwawezesha kuwasiliana na polisi kwa haraka ikiwa ni mojawapo ya kutafuta njia muafaka za kupambana na mauaji ya albino yanayochochewa na imani potofu za uchawi na ushirikina.

Kamanda wa polisi mheshimiwa Suleiman Kova amesema kuwa simu takribani 350 zimekusanywa toka kwa watu mbalimbali waliojitolea katika zoezi hilo na kwamba simu hizo zitagawiwa kwa albino na familia zao kwa lengo la kuimarisha usalama wa wanajamii hao.

Hadi sasa, idadi ya watu waliopoteza uhai kutokana tu na rangi ya ngozi yao ni 35.

Siku kadhaa nimewahi kuandika kuhusiana na suala la ualbino na Tanzania.

Nadhani inaweza ikawa ni wazo zuri lakini nachelea kufikiri kuwa inaweza ikawa hatari zaidi kwa albino na familia zao kwani watu waovu wakishafahamu kuwa wanajamii hawa wana simu za bure, inawezekana kabisa hiyo ikawa ndiyo sababu ya kuwashambulia ili kujipatia simu za bure, na hivyo, badala ya salama ikawa karaha. Suala jingine pia ni kuhusu kuihudumia simu yenyewe kwani simu ili iweze kufanikisha lengo lake la mawasiliano, itahitaji kupewa nguvu kwa kuchaji na kuwa na muda wa hewani. Sifahamu kwa watu wanaoishi vijijini ambapo nishati ya umeme ni tatizo, watawezaje kumudu kuziweka simu zao na nguvu ya kutosha kumudu mawasiliano. Pia, ikiwa wanaopewa simu hizi hawatakuwa na kipato cha kuwawezesha kununua vocha za muda wa hewani, huu utakuwa mzigo badala ya msaada, labda iwe kwamba makampuni ya simu za mkononi yameruhusu baadhi ya namba zao zitumike bure kwa ajili ya mawasiliano haya (kama ilivyokuwa kwenye simu za bure za HIV/AIDS Helpline ya TAYOA).

Nijirudi mwenyewe na kusema kuwa, kwa kila jambo, lazima kuwe na pa kuanzia, hivyo basi ni vyema tujaribu na tuone ikiwa tunafanikiwa katika hili, la, isipowezekana na kama hasara itaonekana mapema, basi zoezi hili lisitishwe na tutunge tena njia nyingine ya kuwalinda wanajamii wetu. Ni vigumu sana kwa binadamu kupata suluhisho la moja kwa moja kwa matatizo yake ndiyo maana nakubali kuwa, tujaribu njia hii na tuone ikiwa itafanikiwa ama la.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads