wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, December 21, 2008

TweetThis! Serikali yaiamuru TaNeSCo kutoinunua DOWANS (maoni yangu mwishoni)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imeiamuru kampuni ya umeme Tanzania, (TANESCo) kuvunja mipango iliyokuwa nayo ya kuinunua kampuni ya uzalishaji umeme yenye utata ya DOWANS kwa manufaa ya Taifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa W. Ngeleja alisema kuwa, Wizara yake ilishirikisha Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba katika suala  hili na kwamba baada ya mapendekezo yaliyotoka Wizara ya Sheria, uamuzi umefikiwa kuhusu faida na hasara za kuinunua DOWANS. Ingawaje wizara ya Sheria na Mambo ya katiba iliafiki ununuzi wa kampuni hiyo kulingana na taratibu za sasa, bado uamuzi huo haukuonekana kuwa wa manufaa yoyote na ndipo Kamati maalum ya Bunge kuhusiana na Nishati na Madini ilipoanisha kuwa haitakuwa sahihi kwa Serikali kununua kampuni hiyo ya uzalishaji umeme, hasa ikizingatiwa kuwa sheria za sasa za ardhi zingekuwa zinakiukwa.
Waziri Ngeleja aliongeza kuwa, awali Serikali ilikuwa imeruhusu ununuzi wa DOWANS kwa kuwa kampuni hiyo ilikuwa katika hali ya uzalishaji na kwamba huenda hilo lingesaidia katika suala la kurejesha matumaini ya kupatikana kwa ufumbuzi wa tatizo la upungufu wa upatikanaji umeme nchini Tanzania.
Kampuni ya DOWANS imekuwa ikitengeneza nishati ya umeme wa kiasi cha megawati 112.5, kiwango ambacho ni sawa na jumla ya nishati inayotengenezwa na vituo vya Mtera (megawati 80), Nyumba ya Mungu (megawati 8) na Hale (megawatri 21).
Kwa mujibu wa mamlaka inayohusika na uratibu wa mipango ya uhitaji wa kiwango cha nishati nchini, Power System Master Plan, kumekuwapo ongezeko la mahitaji ya umeme kwa wastani wa asilimia kati ya kumi na kumi na tano ( 10% - 15%) kwa mwaka au megawati sabini (70MW), kiwango kinachotarajiwa kubakia hivyo kwa mwaka huu wa 2008 na pengine hadi mwaka 2012. Kwa mantiki hiyo basi, tatizo la kupungua kwa nishati ya umeme litabakia pale pale ama kuongezeka!
Ni wakati muafaka kwa Serikali kuchukua hatua zaidi ya kushirikisha wananchi wenye maoni tofauti juu ya namna ya kupatikana kwa ufumbuzi wa tatizo la umeme. Ikumbukwe kuwa, katika kamati maalumu iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe na ripoti kusomwa bungeni, kamati iliishauri Serikali kinagaubaga kuvunja mkataba iliyokuwa nao na kampuni ya DOWANS na kuwapeleka kortini wale wote waliohusika katika uzembe ulioisababishia Serikali kutokana na ushirika huo ambapo serikali ilitumia gharama yenye thamani ya fedha ya KiTanzania bilioni sabini.

Nadhani ni wakati muafaka Serikali iwe na wachunguzi makini wa mambo  kwa ajili ya kusoma yale mengi yanayoandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari na mawasiliano, kisha ijaribu kuyatendea kazi kwa vitendo maoni kadhaa yanayotolewa na wasomi ama watendaji wa sekta mbalimbali. Maoni ya Wananchi yapewe kipaumbele na kufanyiwa kazi kwani ni Wananchi pekee wanaofahamu kwa ufasaha shida, matatizo yao na pengine suluhisho lake, zaidi ya kutegemea viongozi na wawakilishi ambao muda mwingi hawapo katika maeneo yao ya uwakilishi. Ikiwa itafanyika hivi, huenda nchi ya Tanzania ikapata suluhisho ama njia mbadala kuhusiana na masuala mbalimbali yanayoikabili jamii yetu kwa sasa, mojawapo likiwa ni hili la kupambana na tatizo la upungufu wa nishati ya umeme ambayo ni muhimu sana katika maendeleo ya uchumi na hasa katika kuchangia ubora wa maisha ya raia wake.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads