Amninginiza mwenzie dirisha la orofa ya tatu!

Basi katika kisa kinachosadikika kuwa cha ugomvi wa kimapenzi, almanusura kigeuke kuwa tukio la mauaji katika mji mmoja wa Kunming huko nchini China.
Tuki hilo lilinaswa na mpiga picha aliyekuwa akiendelea na shughuli zake za kawaida pale alikumbana na kisa chenyewe na hatimaye kuazimu kupiga picha tunazoziona hapa.


Kisa chenyewe kiliishia kwa kijana kukubali kujisalimsiha kwa askari baada ya wataalamu wa kuzungumza na watekaji walipoingilia kati na kuokoa jahazi.
Hiki si kisa cha kwanza kutukia katika enao hili la mji kwani, visa viwili vya kufanana na hivi vimetokea kwa nyakati tofauti. Kisa kingine kinachofanan na hiki kilitokea majuzi mwezi huu ambapo mtu mwenye kisu aliwajeruhi wanawake watatu kabla ya kumteka Muuguzi mmoja katika supamarkiti ya Carrefour.
Kabla ya polisi kumlaghai mwanaume huyo kwa bakuli la supu na kisha kumuua, kisa hicho kilidumu kwa muda wa saa nne
Na kisa kingine kilitukoa hapo Disemba 19 ya mwaka 2005, kilitokea kisa kinachokaribiana na hicho kaama kinavyoonekana katika picha zilizo kwenye linki hapa.
.
0 feedback :