wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, December 02, 2008

TweetThis! Prof Leonard Kanagwe Shayo wa Demokrasia Makini afariki dunia [update]

Ipo habari katika blgu ya Mroki kuhusu kicho cha Profesa Leonard Shayo (1948 - 2008) na kwa mujibu wa Mashayo.com, mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Alhamisi kwenda Mbezi, Dar es Salaam ambapo heshima za mwisho zitatolewa majira ya saa nne asubuhi katika Kanisa dogo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nah hatimaye kwenye maziko yatakayofanyika Kinondoni tarehe 5 Disemba 2008!

Apumzike pema!

Mroki Mroki (Father Kidevu) anaandika:
Leonard ShayoMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini na Mhadhiri Mwandamizi wa Hisabati katika Chuo Kikikuu cha Dar es Salaam Prof Leonard Kanagwe Shayo amefariki dunia jana akiwa safarini kikazi mjini Arusha.
Prof. Shayo atakumbukwa na wasomi wengi na wanasiasa hasa baada ya kuwa miongoni mwa wanasiasa waliotulia na mmoja wa wagombea Urais katika uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo licha ya rais Kikwete kushinda kwa kishindo lakini naye aliambulia kura 17,033 sawa na 0.15% kati ya kura 10,590,016 zilizopigwa katika uchaguzi huo.
Ni mwandishi wa habari pia maana aliandika makala nyingi katika magazeti kadha ya Tanzania.
Tutamkumbuka kwa mengi lakini kubwa ni rekodi yake kisiasa alipofanya kampeni za Urais kwa Mark II.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads