Julius Kambarage Nyerere - Dodoma, Tanzania (1995)
Hii video niliiposti mwaka jana, hivi leo nairudia ikiwa ni katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu, Baba wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere!
Marehemu Baba wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipozungumza na WanaCCM mwaka 1995 katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi huko Dodoma(nadhani ilikuwa ni Chamwino) katika ukumbi wa Chimwaga (asante kaka Michuzi I.M kwa marekebisho sahihi) kwenye mchakato wa kumtafuta mgombea wa kiti cha uraisi kwa tiketi ya CCM. Mwalimu alisema:
Audio:
Audio (alternative):
Video:
Marehemu Baba wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipozungumza na WanaCCM mwaka 1995 katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi huko Dodoma
Audio:
Audio (alternative):
Video:
34 feedback :
Ahsante sana Dada Shubi kwa kazi yako.Nimekua nikifuatilia hotuba hizi za Rais habazo hatuwezi kuzipata katika vyombo vya habari vya serikali.Katika hotuba hiyo ya Chimwaga nimefikia Tamati ya Rais wa awamu ya tatu Mkapa na huyu wa awamu ya Nne Kikwete Hawakua na hawana sifa za kua marais aibu tupu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.Advocate Jasaha
Asante kwa kushukuru Adv. Jasha!
Dada Subi. Unafanya jambo la maana kabisa kuweka mtandaoni hizi hotuba. Inashangaza kuwa hamna hotuba zozote katika mtandao aidha audio/video. Ziliwahi kuwekwa ktk tofuti ya Mwl Nyerere Foundation, ila kwa sasa tovuti yenyewe imekufa. Kwanini taasisi husika hawaweki public hizi hotuba muhimu? Do a simple experiment, search Nyerere vis a vis Nkrumah on google videos. Utashangaa kuona hits chungunzima za Nkrumah, na chache tu za Nyerere. And this goes for several other issues. Mpaka leo hii hamna live streaming Radio from Tanzania (Radio Maria tunawasifu), hamna television yenye page on youtube (watani wetu wa jadi wanasonga>> http://www.youtube.com/user/standardgroupkenya ) Asante dada Subi kwa kuweka jiwe la msingi ktk kumbukumbu zetu za taifa. Tunahitaji historia ya nchi yetu iwe digital ili hata wale walio mbali na wenye kupenda kujua kuhusu Tanzania waweze fahamu. Asilimia kubwa ya tovuti za Tanzania ni za entertainment (musiki, miss ustakencheke nk), few on important issue like those portrait by Subi here. Hongera tena dada.
Mdau wa San't Egidio
too much clapping.
Mdau wa Sant'Egidio, dah, umenikumbusha mbaaaaali sana!
Allora, Come stai?
Nitarekodi kipindi kizima cha Sala kutoka Transtevere kanisani Sant'Egidio na kukiweka hapa walao tukumbuke...
Kuhusu hifadhi ya hotuba za Mwalimu, heshima za pekee nawarudishia wale wote waliofanikisha kupatikana kwa hotuba hizi. Nimekubali kula gharama ili kuziweka hotuba hizi hewani kwa madhumuni ya (1) kuzitafakari kauli za Mwalimu na (2) kutia chachu kwa waliohodhi hotuba kama hizi wakumbuke kuwa mwenyewe angekuwa na uchoyo, asingekuwa anazungumza kabisa, angeazimu kukaa kimya, na hapo tusingekuwa na la kuhoji ama kujifunza!
Elimu faida yake ni uishiriki na wengine wachambue ubaya na uzuri wake, na siyo kuificha! Uchoyo mpaka wa elimu? Ni aibu! Sijui wangefichaga elimu za Einstein, Aristotle, Marx, Nkrumah nk tungechambua na kujifunza vipi mazuri na mabaya.
lakini pengine chombo chenye dhamana ya mambo yote yanayomhusu Mwalimu kinaandaa utaratibu mzuri wa kutupatia kumbukumbu hizo, tuvute subira na tuone.
Honestly,this is amazing!!Thanks 4 this.
Joseph
Joseph,
You are welcome!
what does it serve us now? simply memories of the better times we had under a steadfast leadership? look at all the mess we are in, and could you believe it all started after these words right here! God Bless us and Keep us safe, we love you Tanzania!
Nasikia TBC wanauza tape hizi,kweli? Maana bongo kila kitu dili.
Nashukuru Subi kwa jitihada zako.
St.Mimi
St.Egidio,
Nami nimesoma kama ulivyosikia wewe, kuwa wanauza kanda moja ya sauti kwa kati ya shilingi alfu na alfu na mia tano.
Subi,
Good job kwa kweli. But it is also sad as said earlier, right after those words it was the beggining of apocalypse! We have lost direction, leadership has failed flat on the surface, our society is becoming lawless and valueless etc. Tuombe jamani, we love this beautiful country which neighbours wanaitolea macho na uchu! God bless us.
Isaac K
Subi... this is nice. I enjoyed the speech! Thanks and please keep it up!
I will be visiting more often for more goodies!
Dada Manka
Isaac K and Dada Manka,
I am glad that you listened to the speech.
I will keep on posting if anything new comes up.
This is awesome, incredible fantastic, you are doing marvellous job, I am not sure if Tanzanians do vist in mass your blog, for me it is number one. You the way he talks about RUSHWA!!! WATANZANIA TUIOGOPE RUSHWA KAMA UKOMA, WANYONGE NDO WANAKUFA NA RUSHWA.
Thanks Ed.
Thats good job Subi,
For posting words of prophet.Its amazing how most those uttered reflects current situation in my beloved country. Its also shame how our current leader lived up to Nyerere predictions. they surely didn't dissapoint. Apocalypse? i would'nt use that term yet, i still have faith in my country.
first i believe there should be another Nyerere somewhere he need to spring up to big stage
secondly sometimes circumstance shape our corrupted thinking, major crisis might awake lot of people with "it is not my busness attitude"
Lastly its everybody country we choose leader to represent us,if they don't deliver (actually insult us by abuse power)we get rid of them by collective effort, i like what some of important institution is doing so far..
otherwise i again thank Subi for putting us on our feet
goodjob
angalia pia kama kuna uwezekano wa kuweka hotuba za mzee karume.
Subi!
Unafanya kazi kubwa kuliko unavyofikiri. Ahsante sana!
As time goes by I slowly and solidly realize why Julisu Nyerere was that much admired by big brains.
He had his weaknesses and failures but he lived an honest and heroic life.
RIP Mwalimu.
Anon wa Wed Dec 24, 07:17:00 AM EAT
Ningezipata hotuba za Mhe. Karume ningeziweka, lakini sina namna ya kuzipata labda hadi ajitolee yeyote mwenye uwezo wa kuzisaka.
Anon wa Wed Dec 24, 07:24:00 AM EAT
Asante kwa kushukuru!
hi subi,
No one is 100% perfect, that's every one has strenghts and weaknesses,but real Mwalimu's strengths overcomed weaknesses,he built a good foundation for our country but Fisadi,are misleading our country,we,youngs we have a great tusk to restore the lost hope, for ur information Tanzania is not a peaceful country anymore, its guided by dictatorship gvt,though its too underground,if you have ur relatives who are in the system(fisadi network) you won't realize and understand what i mean,if your in TZ,recall how many issues/things you supposed to get for free,that's its your right but yet you attempted to lobe throug corruption,refer in hospitals,education,or any ,
Kama viongozi wote wangekuwa kama Mwalimu real tungekuwa mbali, let bad fortune fall on all leaders leading our country badly
Mwalim's speeches will never fade!
by frank
Ohoo !! its fantastic to hear this. By the way, I thing the man who was targeted by Mwalimu did not hear what he was saying and emphasizing. Why???!!!! What we are witnessing now is indirect proportional to what Mwalimu and the rest of us expected.
I thing if Mwalimu was alive today, he would not wish to hear this great speech of all time.
Dada Subi,nyumbani kwangu huku Ugiriki ukiingia basi utakutana na kwanza picha ya mwanangu binti mpendwa,halafu pili ni picha ya Mwl Nyerere.watu wakija wanauliza kama ni picha ya babu yangu basi nami nawaambia ni picha ya babu wa Watanzania wengi na maybe Waafrika kadhaa.ni mojawapo ya vitu vinavyonifanya nijisikie sana kuwa Mtanzania.
Ahsante kwa kututumia hotuba hizi za Mwalimu.....
Mdau,Thessaloniki,Ugirki..
Thank you all for commenting, I love reading your views.
Dada Subi,kwa kweli umetubariki kwa kuweka hii hotuba hapa.Ingawaje aliyechaguliwa kwa sasa ni historia,hotuba kama hizi ni muhimu kwenye kuwatia chachu wanakuja mbele na kutukumbusha kwamba mengi tunayoyakumba sasa marehemu JK Nyerere aliyazungumzia na viongozi wetu kuyajua (i.e. helps us keep the politicians accountable).Umefanya la maana sana na Mungu akubariki na kukuwezesha kuendelea na moyo huo wa upendo.
Ni kitu cha kujivunia na kuendelea kumshukuru Mungu kwamba kiongozi wetu wa kwanza,Baba wa Taifa,alikua ni mtu "special",mwenye hekima na busara sana,tena sana.
Mungu ibariki Tanzania,dumisha uhuru na umoja. Amen.
Ndimi nduguyo,
Majaliwa Kadebe Nicholaus
Ndugu yangu Majaliwa, shukrani sana kwa maoni na uchambuzi wako, inafurahisha kusoma jinsi watu mbalimbali walivyomfahamu na kumsoma marehemu Mwalimu.
Katika kila jambo, kuna la kujifunza na kuacha, tujifunze mazuri na tuache mabaya, ndiyo sifa ya ubinadamu tena hiyo.
Subi this is great.
Listening to these speeches, I can’t figure out what exactly happened to Benjamin Mkapa during his last five years.I do ask myself if BM was an evil man even before became president, but Nyerere didn’t know him well? Was there any wicked creature crept to state house after the death of Mwalimu? Who was this? Was his wife? Or? These speeches are good enough as management toolkit. Mkapa had no reason at all to fail Tanzanians and Mwalimu if he was fair and clean person from the beginning. Actually, we can not be speculating now to who deceived he; I believe he himself is an evil man since he was born. Imagine now being numb, does it shows that he regrets to what he did? ----- Tarnish his name and image including the late Mwalimu who fought for his ascendance? I know he knows very well that he made stupid mistake that’s why has no guts to come public and tell Tanzanians the truth. And he knows very well that if Tanzanians are serious united he will be prosecuted as an ordinary guy- no protection for any body or above our mother law---the constitution. Mwalimu mentioned in one of the speeches that kiongozi aliyeapa kuilinda katiba, akiikiuka hiyo katiba tutamshitaki. Sasa iweje leo hii? Tunafukuza visamaki vidogo vidogo babalao tunaliruka eti linalindwa na katiba aliyoisigina. Kichekesho cha baadhi ya watu kwenye mjadala unaoendelea sasa kuhusu Mkapa ni kuwa sheria yetu inamruhusu - mtu kuaapa kuilinda katiba, na akishindwa kuilinda kama alivyoapa basi katiba inamlinda yeye ili asishitakiwe. Hapa kuna incentive yeyote ya kuilinda katiba?. The fate of this man is prosecution, if not now time will tell.
Racket
Subi,
Ubarikiwe na asante sana. Sina la kuongezeaila nabaki najiuliza, "Hivi hawa vilaza Mkapa na Kikwete walikuwa kwenye huo mkutano ?" Kama walikuwepo, waliweka pamba masikioni ? Kama hawakuweka basi ni vijitu visivyostahili hata kupewa uongozi wa kijiji, what a waste,all that human flesh and not an iota of brain !! God forbid, aarrghh, grrrrr grrrr !!!
yaani hongera mno SUBI,
kuweka mambo ya babu! ni vitu muhimu na adimu mno!sina la kuongeza ,ina tafadhali ,mwingine mwenye Hotuba ya mtu huyu muhimu mno kwenye historia ya nchi yetu atuwekee humu!kwani ikumbukwe kuwa kama hatutakuwa na uwekaji wa kumbukumbu wa vitu muhimu vya bongo basi ,tutavisahau baada ya muda si mrefu.zamani ,ilikuwa kila wiki kama sikosei,tunasikiliza habari za mzee huyu muhimu!!
hawa marais wetu kwanini hawasikilizi mambo muhimu kama haya humu ndani mfano "rushwa,umasikini,udini,ukabila" kwanini hawa marais wasiwe wanasikiliza hotuba za babu yetu huyu ingawa ni marehemu sasa!
Yasser
Anon Sun Jan 04, 05:17:00 PM EAT
You have asked touched the core issues and indeed questioned about the integrity of our leaders and whether they really understand and interpret the constitution (which is the foundation of a good leadership of any country) as it should be interpreted.
Just like you, it's hard for me to understand why they (leaders and law makers) are quick to cover up the obvious translation of all the rules and laws that should go against anyone that operates beyond the margins of a democratic country like ours.
May be, just may be, the current initiative and movements to crack down frauds, we shall be able to re-define our values and make sure that we stand for our rights and demand justice.
Anon Tue Jan 06, 03:37:00 AM EAT umeniacha mbavu zinauma, sijacheka kwa kuwa ulichoandika kinachekesha ila nimeichora taswira ya hao uliowataja na kushangaa kama kweli walikuwemo na walimsikiliza Mwalimu ama walikuwa zzzzz bin brrrrr muda wote. Na sijui mawazo yao yalikuwa yakitafsiri vipi maneno ya Mwalimu.
Ama kwa hakika binadamu hakosi kasoro, lakini kasoro zinapozidi hata yale ya msingi na ya maana kabisa tunayoaswa, hii inatia shaka sana na walakini mkubwa kwa viongozi na watawala waliopewa dhamana na wananchi.
Mathalan, Mwalimu alizungumzia juu ya vita na mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu, je, waliokuwa 'njuka' ambao ndiyo viongozi wa leo walimwelewa vipi? Ule ukali na uchungu wa kuiba mali ya umma aliousemea Mwalimu uliwaingia vipi akilini?
Ama kwa hakika, maswali ni mengi kuliko majibu. Inahitaji nguvu ya kila mmoja wetu katika kupambana na mambo ya hovyo nchini mwetu.
Safari ingali ndefu!
Yasser,
Nashindwa kupata jibu la swali lako la kwa nini viongozi wasimsikilize Mwalimu, huenda wakikusoma wataona unawazeveza tu.
Lakini nafikiri tatizo halipo katika kumsikiliza Mwalimu, hawa wanaweza kufungiwa bungeni kila siku ya bunge wasikilize hotuba ya Mwalimu kwa dakika thelathini ama wanaweza kumsikiliza asubuhi hadi jioni na hata ikibidi kuwawekea 'headphones' masikioni watembee wakimsikiliza kwenye 'walkman' inaweza isisaidie lolote. Ikiwa hawataki kubadili nia na kukubaliana na dhana ya 'uongozi bora', bado tupo kwenye maktaimu tu.
Wamkatae Mwalimu kuwa alikuwa na UShuKi wa elimu na maongozi ya uchumi, lakini wakubali basi kuwa alikuwa na upeo wa juu wa kuzingatia mambo ya umoja wetu kwa kila hali iwe ni elimu, afya, mgawanyo wa mali nk. Waige mazuri yake na waache mabaya, yeye aliwahi kusema kuwa "ujinga wa viongozi wetu, wana-question hata yale mazuri".
Nadhani ikibidi tulumbane rasmi kimdahalo kama wa Taifa, na tujadiliane tu ili watu tuafikiane juu ya mambo ambayo Mwalimu aliyafanya vizuri tuyafuate na yale aliyokosea tuachane nayo. Haiwezekani akawa alikosea kila kitu. Haijawahi pia akatokea kiongozi aliyeweza kila kitu (pengine mitume waanzilishi wa dini).
Ndiyo dhana ya ubinadamu tena hii (hatujakamilika).
SUBI, SIJUWI UMRI WAKO LAKINI NAHISI NI MTU MAKINI SANA. FIKIRIA CAREER KATIKA UMMA BACK HOME, I MEAN POLITICS, JIANDAE VIZURI TU INAWEZEKANA. MIMI NIMEKUWA SHABIKI MKUBWA SANA WA NYERERE, HAKUWA WAKATI NYERERE AKAHUTUBIA LIVE KUPITIA VYOMBO VYA HABARI SI KUKAA CHINI KUMSIKILIZA, HIZI HOTUBA ZOTE NAZIKUMBUKA WAZI WAZI, HUYU BWANA ALIKUWA MAKINI SANA NA NI MSOMI KWELI, WAZUNGU WALIMU-UNDERMINE BURE KWA VILE HAKUWAKUMBATIA KAMA AKINA KENYATAA NA MANDELA NDO MAANA BADO WANAMWAGIWA MISIFA KULIKO NYERERE, THIS MAN WA SIMPLY THE BEST. KATIKA HUTUBA ZAKE NYINGI NILIZOHUDHURIA LIVE NILIKUWA KILA WAKATI NAKAA MBELE KU-EXAMINE HOW HE WAS MSOMI, KWA MFANO NILIKUWA NAMSHANGAA SANA WAKATI MWINGINE ANAWEZA KUONGEA BILA MAANDISHI AKASEMA LEO NITAONGEA MAMBO KUMI NA AKAYATAJA NA AKAANZA KUYAONGELEA MOJA BAADA YA JINGINE KWA MTIRIRIKO ULE ULE BILA KURUKA HATA MOJA NA KWA UFASAHA USIO NA MFANO, HUTUBA YA MWISHO NILIYOHUDHURIA NI ILE PALE JANGWANI AKIMNADI MKAPA, ALITOWA HATUBA AMBAYO ILIKUWA SAFI KIASI KWAMBA CUF WAKAFANYA FUJO NA NYERERE NI MTU MWENYE AKILI NA MAKINI SANA AKASOMA UMATI AKAONA HAPA PANAWEZA KUFA MTU, UNAJUWA ALIFANYA NINI! ALIKATIZA HOTUBA NA TUKAONDOKA BILA FUJO ZA KUTISHA. HUYU BWANA NI KICHWA.
Ahsante sana Dada Subi, kwa collection yako hii.
Hotuba kama hizi wanapozisikia Viongozi wetu wa sasa, wanaziona ni "mwiba" mkali kwao. Hawapendi kuzisikia, maana mambo wanayoyafanya sasa hivi, walikatazwa na Baba Wa Taifa, tangu zamani.
Viongozi hawa sasa wanashindwa kuzificha nyuso zao hata mbele ya "Wajukuu" zao wanapowauliza kama wanayajua hayo aliyoyasema Nyerere.
This Is Black=Blackmannen
Dada, I real like 'nukta double seven. I've discovered it today for the first time. Frankly You are doin great dada.
Keep it up.By the way i've been asking myself how talented u could be for 'nursing has nothing to do with what u are doing. This is your calling dada I suppose!!!
Thanks for the tireless speech of JK original"Mwl" I adore him. I've been looking for since long.
I love my country TZ and I pray that Almighty God protects it from all kinds of discriminations( Religious, Colour,Tribal,etc), corruptions, and that our current and future leaders may consider the wealthy and spirit of Nyerere's speeches by putting them not only in political platforms but also in action. Amen
Mdau mpya M,Simon
Paris-France
Hi Mdau M,Simon
I am glad that you were able to listen to Mwalimu and that you have enjoyed listening and reading posts in this blog. I think my love for computers has led me to exploring more and wanting to share with others the 'discoveries'.
Karibu sana!