wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, November 12, 2008

TweetThis! TeknoHaMa

http://www.teknohama.com/makilla_r2_c2.gifTeknoHaMa ni kifupi cha maneno Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Teknolojia hii imetiliwa mkazo tangu  katikati ya karne ya ishirini na kushika kasi katika karne ya ishirini na moja ama milenia mpya. Tumeishuhudia ikichukua nafasi kubwa katika utandawazi na shughuli za kawaida kabisa za binadamu kwa mfano mawasiliano ya simu, runinga (televisheni), tarakilishi (kompyuta) nk. Teknolojia hii inatumika sana katika kujuliana hali, kupashana habari na taarifa za matukio mbalimbali iwe ni nyumbani, maeneo ya kazi, safarini nk.

Umuhimu wa TeknoHaMa ulidhihirika zaidi katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Marekani ambapo wagombea uraisi wawili Seneta McCain na Obama walichuana vikali. Mheshimiwa Obama aliweza kuitumia vyema teknolojia hii na inasadikiwa kuwa ilitia changamoto kubwa katika kuhamasisha vijana na watumiaji wengine wa tarakilishi kushiriki katika kupiga kura za uchaguzi.

Ama katika nchi yetu ya Tanzania, teknolojia hii imesaidia sana kuhabarisha watu kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi yao. Pamona na kupashana habari nzuri na za kupendeza, mMchango wa waziwazi umeonekana zaidi katika mapambano yakufichua wabadhirifu wa mali ya uma, mafisadi na viongozi wazembe. Hii ilidhihirika hasa pale mheshimiwa Dk. Wilbroad Slaa alipotoa kauli ya kuthibitisha madai ya uovu wa baadhi ya viongozi alioupata kupitia mawasiliano ya barua pepe.

Idhaa ya KiSwahili ya BBC katika kipindi cha Dira ya dunia walizungumza na wana TeknoHaMa wa nchini Kenya na mwingine wa Tanzania, ndugu Muhidin Issa Michuzi, ambao walitoa maoni yao kuhusiana na teknolojia hii. Wasikilize kupitia hapa: TeknoHaMa

Pia katika siku za hivi karibuni tumekuwa tukisoma habari mbalimbali na kusikia juhudi wanazozifanya jirani zetu wa Rwanda katika kuharakisha maendeleo katika nchi yao hasa katika nyanja za teknolojia hata kukiri kuwa jembe la mwananchi wa kawaida wa Rwanda kwa sasa ni tarakilishi na siri ya maendeleo ni kuwekeza katika teknolojia. Mwezi jana walithibitisha hilo kwa kutekeleza mpango wa awali wa kumpatia kila mtoto wa Rwanda kompyuta binafsi,  vile vile walizindua simu iliyotengenezwa kutoka nchini mwao.

Mwaka jana katika mojawapo ya vipindi vilivyorushwa na Dira ya BBC ni kile kilichokuwa na sehemu ya mahojiano juu ya siri ya mafanikio na maendeleo ya TeknoHaMa katika nchi ya Rwanda.
Ili kusikia siri ya mafanikio hayo, bofya hapa: ICT Rwanda

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads