wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, November 28, 2008

TweetThis! Salam za Dk. Hamisi baada ya kunusurika India

Jana nilitoa pole na kuandika kwa ufupi kuhusu mkasa wa mashambulizi ya kigaidi nchini India, kwa bahati nzuri walikuwepo wawili kati ya WaTanzania waliopo huko. Dk. Hamisi alitufahamisha yaliyotukia huko jana, na hivi leo anaandika:
Ndugu,
Namshukuru mwenye enzi mungu kwa kunitoa kule salama! Nashukuru sana kwa kunisalia niwe mzima na nirudi salama. Na muda si mrefu nimetua nyumbani. Maana ilikuwa kama Movie vile kwa sisi ambao hatujazoea. Maduka na maofisi mengi yalifungwa. Hali ya hatari bado ipo japokuwa makomandoo walionekana kuwazidi nguvu magaidi. Polisi 12 wameuawa wakati magaidi waliouawa ni wawili tu na aliyekamatwa ni mmoja, wengine wapetoea at large. Inasemekana kulikuwa na magaidi kati ya 25 na 30! (Ikionesha ni jinsi gani walivyokuwa well trained and prepared!) kwanza walikuwa wamevaa jeans au khaki zenye mifuko mingi na humo walikuwa wamejaza ammos na gadgets mbali mbali za mawasiliano kama vile satellite phones, radio calls etc na walikuwa wamevalia all-terrain boots na kila mmoja alikuwa na ranksacks mbili (moja kwa mbele na nyingine kwa nyuma, zote zikiwa na ammos! wengine waliuwa na AK47, wengine automatic machines, na mabomu (viazi) na chemicals na nyaya za kutengenezea mabomu - walikuwa wakiona makomandoo wamekaribia, wanatega bomu linalipuka na jitihada za kuwasogelea zinatulia kwa muda. wameuwa wazungu wa marekani na uingereza takriban 8. Death toll mpaka naondoka ilikuwa 128 na majeruhi zaidi ya 320. wenyewe wahindi wameiita hii insidence kama 26/11 a. k. a India's 9/11! Usalama umeongezwa nguvu. wageni wengi wameondoka kwa ghafla. masoko ya fedha yalifungwa. mashule yalifungwa. mpaka jana usiku naondoka, walikuwa hawajadhibiti au kuzitawala hizo hoteli mbili na nyumba moja ya makazi ya watu.
Subira unaweza ukatumia tu hizi habari, na bahati mbaya sikuwahi kupata taarifa zozote zile za mbongo aliyedhurika, japokuwa eneo hilo ndo kuna wabongo wengi (wengi wao niliobahatika kukutana nao, kabla ya tukio; bahati mbaya sana walikuwa wanauza unga tu, wengine mateja tu, walienda kutafuta maisha mabo yakakwama wakabaki kuwa wateja au wachuuzi wa mihdarati - nilisikitishwa sana na hii encounter).
Ahsanteni sana,
Hamisi.
Hamisi, Asante kwa ruhusa ya kuitumia taarifa. Pia, ninafurahi pamoja nawe na familia yako kwa kurejea salama u salmin nyumbani Tanzania.

1 feedback :

Yasinta Ngonyani said... Fri Nov 28, 07:03:00 AM MST  

Nasi pia tunamshukuru mungu kwa kuweza kukutoa kule India salama na kuwa na familia yako. na pia kurejea nyumbani TZ

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads