wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, November 27, 2008

TweetThis! Salam za pole. The terrorist attack in India [updated]

Nachukua fursa hii kuwapa pole na kuwatakia heri na afya njema ndugu, jamaa na rafiki zetu wote waliopo India kwa hali ya msukosuko wa mashambulio ya kigaidi yaliyotokea katika eneo la Mumbai hasa Taj Mahal, Oberoi na maeneo ya karibu.

Dk. H. Kigwangallah anaripoti kuwa yupo salama, ninatumai kuwa Dio Ndabagoye na Albert Joe (asanteni kwa kunifahamisha kuwa mpo salama) pamoja na marafiki wengine mpo salama u salmin.

Dk. Hamisi anaandika:
I am in Mumbai currently na kuna mashambulizi makali ya kigaidi hapa kwenye kiini cha jiji, ambapo ndipo nilipo. kwa kweli hali ni mbaya sana na tuombe mungu tu haya mambo yasifike nyumbani kwetu Bongo. Magaidi wameteka hoteli za kiwango cha five star; watalii na foreigners wametekwa na wengine wameuawa. Ni vijana wadogo sana, kati ya 20 hadi 25 wanaowasumbua makomandoo, polisi, usalama, na anti-terror squad ya hapa India. Waliingia kwa boti wakiwa wamevalia ki-brothermen - jeans na tshirts (ofcourse ni vijana), wana mabegi mawili mawili hivi yamejaa ammos, wameshikilia AK47, walipotia nanga tu wakashuka kama wanajeshi vile na kuvamia hoteli kubwa ya kihistoria hapa Mumbai iitwayo The Taj Mahal hotel na nyingine ikiwa jirani hapo inayoitwa The Hotel Oberoi, wanawashambulia watu na polisi kwa AK47 na viazi! wamepiga mitaa ya jirani hapa center, railway station, wamelipua taxi, wamepiga kwenye hospitali na wameteka jengo moja ambalo ni makazi ya watu. tokea saa 4 usiku jana, wanarushiana risasi na mabomu na wanausalama. watu walitawanyika hovyo na kuumizana, watoto hawaonani na wazazi wao, basi ni vilio tu! magaidi walifanikiwa kuteka polisi van na wakaitumia kuzungukia na kufanya mashambulizi. wameua polisi 11 na kujeruhi wengi. high-ranked policemen 5 were killed on the spot thru sharp bullets despite wearing bullet proofs na helmets. Mpaka sasa watu wanaozidi 100 dead, na wengine takriban 200 severely injured.
Kutoka nje hairuhusiwi, tuliokuja kibiashara zetu tumekwama hapa, na hali ya usalama ni mbaya, hatujui kama tutatoka salama katika hili jiji.
Jamani bora kuhadithiwa au kuyaona haya mambo kwenye TV, movie, na kusoma kwenye magazeti na internet-bali ukiwepo eneo la tukio inatisha sana! Usiku kucha tupo macho, hatujalala. Yaani ni mabomu, milio ya risasi. Barabara zote zipo kimya kabisa, watu hawatembei.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu tuepushie haya mambo ya violence kwetu Tanzania, Amina.
Hamisi Kigwa.News from BBC Word says more than 100 people are confirmed dead while leaving more than 300 physically wounded.
Some photos from Mumbai courtesy of Reuters.
  

Burning and flames of fire from Taj Mahal

Police exchange fire trying to free hostages


Hostage speaks after release


Hostages have been freed from the hotel

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads