wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, June 26, 2008

TweetThis! Nyonyo/Mbarika (Castor)

Mnyonyo (KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka (KiRusi) ni mmea wa jamii ya Mbono Kaburi, kwa jina la kitaalamu Japtropha - nitauzungumzia siku zijazo.

Jani la mnyonyo
Jani la mnyonyo/mbarika
Baadhi ya faida za mnyonyo na mazao yake.
Mbali na kuweza kutumia mnyonyo kama uzio hai, njia hii inaweza kutumika kwa wale wasio na eneo kubwa la shamba ndiposa wakapata faida zake kama ifuatavyo:
Majani ya mnyonyo yanaweza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kukanda (massage) ili kuondoa maumivu na majani haya yakifungwa kwenye mguu unaouma huleta nafuu hasa kwa maumiviu yanayokuja baada ya kuteguka, pia hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama.

Mizizi ya mnyonyo huweza kutumiwa kama dawa ya mafundo fundo, uvimbe, kuungua, macho ya manjano, kuumwa koo na magonjwa ya kuambukiza ya kisonono na kaswende. Ukijaza maji baridi kwenye kikonyo cha mnyonyo na kumpa mtu mwenye kwikwi kila baada ya dakika mbili au tatu hivi, mara nyingi huondoa usumbufu unaoletwa na kwikwi.

Mbegu/Punje/Tunda/Njugu za mnyonyo zikimezwa na maji bilauri moja kila siku kwa muda wa siku tano huweza kutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua. Vile vile, mbegu hizi huweza kusagwa na kisha kuenguliwa mafuta kwa ajili ya kulainisha mashine na mitambo viwandani.
mbegu za mnyonyo kabla ya kukomaa
Mafuta yatokanayo na mbegu za nyonyo mfano Ricinoleic Acid, Oleic Acid, Linoleic Acid nk hutumika kutibu ugonjwa wa wa jongo (rheumatism) unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na baridi, pia hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama arthritis na gauti.Mafuta ya mnyonyo pia yanaweza kutumika kama njia ya kupanga uzazi kwani yana kiasi fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalamu kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo, huweza pia kutumiwa kama mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana. zazi wa mpango.

Tahadhari:
  • Mnyonyo ni mti wenye sumu inayoweza kuua binadamu au wanyama endapo itatumika kuzidi kipimo.
  • Mazao yoyote yatokanayo na mnyonyo huhatarisha au/na kuharibu mimba na hata kuweza kusababisha kifo cha mjamzito, hivyo, matumizi yake lazima yawe ya uangalifu mkubwa.
  • Mafuta ya Ricinoleic acid yanayopatikana kutokana na mnyonyo vile vile yanaweza kutumika kurekebisha hedhi (mzunguko wa damu ya mwezi kwa wanawake) ikiwa mzunguko umechelewa ama kusimama katika umri usiotarajiwa. Huweza pia kupunguza maumivu makali yanayotokea wakati wa hedhi.
  • Mafuta ya mnyonyo yanayojulikana kitaalamu kama Undecylenic Acid huweza kutumika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi na vidonda vinavyosababishwa na bakteria ama ukungu (fungus). 
mbegu za mnyonyo baada ya kukomaa


Akina mama wanaonyonyesha pia wanaweza kutumia mafuta baridi ya mnyonyo (kiasi kidogo ili kuepuka madhara ya mafuta hayo kwa mtoto, kumbuka hapo awali nimeandika kuwa mafuta haya yakitumiwa kwa kiwango kikubwa ni sumu) kuongeza wingi na mtiririko rahisi wa maziwa. 

Nywele nzuri, safi, nadhifu na zisizokatika pia ngozi imara inapatikana kutokana na matumizi ya mafuta ya mnyonyo.Mafuta ya mnyonyo pia ni dawa nzuri ya kufungua tumbo la uyabisi (kuvimbiwa).

Faida nyinginezo: Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na ukungu (fungus).

Njia:
  1. Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama eneo lenye maumivu ama kidonda. Vinginevyo, chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea na shughuli za kawaida.
  2. Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini.
  3. Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja.

3 feedback :

Anonymous said... Sun May 10, 11:26:00 PM MST  

woooh, nimekubali huu mmea unajiotea tu kule klwetu lakini faida zake ni lukuki. Kwa kuongezea baaada ya kufanya kautafiti kidogo nimekuta haya;
- inatibu mba
- inatibu magonjwa mbalimbali yangozi k.v mapunye, psoriasis n.k
- mafuta yake hutumika kupikia
- ni ingredient ya utengenezaji sabun, polishes, Rangi, varnishes n.k
_ inaua wadudu

Subi Nukta said... Sun May 10, 11:46:00 PM MST  

Anon wa Mon May 11, 09:26:00 AM EAT,
Asante sana kwa mchango wako kuhusu mmea huu.
Doh, ama kwa hakika elimu haina mwisho, walijisemeaga wahenga wetu!

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads