wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, April 27, 2007

TweetThis! Tofautisha bendera/rangi hizi!

Leo katika kudadisi mambo nimekutana na bendera iliyonifanya niseme; Bendera kama hii SIYO bendera rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rangi kama hizi, ukiwa nazo kwenye kitambaa, ukiibeba, ukiivaa, ukiiweka kama picha ya kompyuta yako, ukiisimika katika mhimili ama popote kwenye makazi yako ama kwa namna yoyote ile ukiitumia, basi jua unawakilisha LGBT (Lesbians, Gays, Bisexuals and Transgenders), tafsiri ya KiSwahili sanifu ni Wasagaji na Wasenge.
Hizi ni rangi za bendera ya LGBT na kwa vile wameweka alama za rangi ya Nchi yetu Tukufu, basi inaashiria LGBT - Tanzania.

Wana harakati wa kusumbukia kupatikana kwa amani duniani walikuwa wakibeba rangi za upinde wa mvua ili kuashiria amani kwa watu wote bila kujali rangi, utaifa, daraja, tabaka n.k. lakini kwa miaka ya hivi karibuni, ili kuepusha mkanganyiko, wao huweka jina PEACE katikati ya rangi za upinde wa mvua. Pia ukitizama utagundua kuwa mpangilio wa rangi hizo ni tofauti na ule wa bendera hapo juu, hivyo bendera ya AMANI huonekana hivi:
 [Peace flag] ama [Peace flag]
Hivyo ukijitwika bendera (hasa kwa wale wapenda kuiga kubeba bendera alimradi amemwona fulani kabeba) usijeshangaa macho na yakakutoka pima wenyewe watakapokufuata mwenzao.


Salam zangu...

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads