wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, August 02, 2009

TweetThis! TFF na ndoto ya kualika akina Eto'o, Kaka kucheza Tanzania

Unajua si vibaya kuota? Si vibaya kabisa. Yaani kuota si sawa na kukaa bure bila kuota. Maana'ke ujue, ni kuwa kwa kuwa na kipaji tu cha kuota ndoto basi tiketi mojawapo tu kuwa ndoto nyingine hugeuka na kuwa kweli. Sasa ni ipi ndoto ya viashiria vya kuwa itageuka na kuwa kweli na ipi ni zile ndoto za Ali Nacha mi sijui. Ila TFF ina ndoto...

...inasimuliwa na Ibrahim Bakari wa http://www.Mwananchi.co.tz
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga amesema shirikisho lake litaweka utaratibu wa kuwaalika wachezaji wanaocheza soka ya kulipwa Ulaya kuja kuchezea timu za Tanzania kwa lengo la kuinua kiwango cha soka nchini.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Tenga alisema: "Hatuna kingine, tunachotaka kwa wachezaji hawa wa nje, tunataka waje kuwaambukiza utaalamu wachezaji wetu.

"Tunaelekea kwenye soka ya kulipwa na hili nadhani ni la msingi. Mfano, tunamchukua Samuel Eto'o aliyeko Inter Milan au Kaka wa Real Madrid au hata Ronaldinho, tunamwuingiza kwenye timu kama Simba au Yanga, wanafanya mazoezi na baadaye mechi, lengo hapa ni kuona utaalamu wake.

"Hawa wenzetu wako mbali na sisi tuwatumie...najua wakati ligi zinaendelea inakuwa ngumu, tunaweza kuweka ka-program baada ya ligi zote kumalizika wachezaji hawa wakaja na inawezekana. Tuna wadhamini wengi, lakini tunasimamia palepale, tunataka kutengeneza mpira wetu," alisema Tenga.

Akizungumzia hali ya soka Tanzania, Tenga alisema kwa sasa anafurahi kuona imepiga hatua kutokana na kuwepo kwa programu mbalimbali za vijana.

Alirejea kauli yake ya awali kuwa anamalizia kutengeneza misingi ili kwa watakaokuja baadaye waweze kuendeleza badala ya kuanza moja.

"Tanzania inao wapenzi wengi wa soka na hili ndilo naweza kusema, msingi wake ni huu, tunajenga na tunaimarisha misingi," alisema Tenga.

2 feedback :

Anonymous said... Sun Aug 02, 06:00:00 AM MST  

Holiday period for professional footballers is very short. Not sure if the plan is feasible. Mshiko wa kuwalipa hawa jamaa nani atatoa? Halafu kucheza mazoezi na etoo itasadia nini? Wachezaji wa bongo waisha muona etoo mara kibao.

Tatizo si upande wa wachezaji peke yao, kuna factors nyingi, kocha, formation, mshikozzzz na psychology ya wachezaji.

Wakisema wanaleta kocha (Mourinho, Guus, Benitez aje akochi for a week hivi, at least nitawaelewa kidogo)

Na kwanini Simba na Yanga sio Taifa stars?

Mzee wa Changamoto said... Sun Aug 02, 08:35:00 AM MST  

Dada Subi. Nauliza na hapa (kama kule hujaona) UMESHWAHI KUSHIBA NJAA??
Ndiko ninakoelekea
Heaven help us all. Ameen

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads