Amri yatolewa mabasi ya abiria yawe na mikanda ifikapo Oktoba
Nimefurahi kusoma taarifa inayosema kuwa, amanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania bwana James Kombe, ametoa amri kwa mabasi yote yanayotoa huduma ya usafiri wa abiria nchini Tanzania kuwa na mikanda kwa ajili ya kulinda usalama wa abiria wawapo safarini. Ni matumai ni yangu kuwa amri hii itatekelezwa na kwamba hatua hii itasaidia sana kupunguza idadi ya watu wanaofariki punde ajali inapotokea. Kwa upande mwingine, ufungaji mikanda utasaidia kupunguza tatizo sugu la kusunda abiria kupita kiwango kilichoidhinishwa jambo ambalo huwasababisha kusimama kwa mwendo wa aghalabu safari nzima.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kombe alisema suala la kufunga mikanda katika mabasi sio jambo la hiari na halina mjadala ni wajibu wa kila mmiliki wa basi kuhakikisha anatekeleza agizo hilo kwani ni moja ya sheria za usalama barabarani nchini.
Alisema ifikapo Oktoba mosi basi ambalo litakuwa halijatekeleza agizo hilo litakamatwa na askari na kupelekwa mahakamani pamoja na kulizuia kuendelea kufanya kazi hiyo ya kusafirisha abiria. Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na mabasi ambayo hayatatekeleza agizo hilo na watapewa adhabu kali kwa kudharau agizo hilo.
Amesema lengo la agizo hilo ni kukabiliana na ajali za barabarani zimalizike ama zitoweke kabisa na kila basi linatakiwa liwe na cheses nzuri, na mikanda ya kuvaa abiria wanapokaa kwenye siti kwa kuwa abiria wamekuwa wakijeruhiwa na kufa kwa kukosekana kwa mikanda hiyo
0 feedback :