wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, August 17, 2009

TweetThis! Abdallah Zombe aachiwa huru

Habari ndo hiyo kwa mujibu wa blogu mbalimbali, hapa ninanukuu kutoka blogu ya Basil Msongo - Maisha
Breaking News
WASHITAKIWA wote katika kesi maarufu iliyomuhusu aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Polisi Dar es Salaam, Abdallah zombe na wenzake wanane wameachiwa huru.
Walishitakiwa kwa kosa la kuwaua watu wanne akiwemo dereva wa teksi na wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge mkoani Morogoro.
Unaweza kutizama picha za tukio hili ambapo Zombe na waliokuwa watuhumiwa wengine wanasindikizwa kwa vyombo vya kusalama kutoka eneo la mahakama kuelekea uraiani makwao. Picha zaidi zipo kwenye blogu ya John Bukuku - FullShangwe (bofya hapa) au bofya kwenye picha kuekelea huko. 
[5.JPG]

Picha zaidi zinapatikana pia katika blogu ya Othman Michuzi - Mtaa kwa Mtaa
Washtakiwa wenzake na Zombe wakiwahi kupanda Land Rover ya Polisi (farasi mweupe) baada ya kuchoropoka katika kesi iliyowakabili takribani miaka mitatu.

2 feedback :

Subi Nukta said... Mon Aug 17, 09:07:00 PM MST  

Mzee, huu ni uwanja huru, kila mtu anasema au kukaa kimya kwa uhuru wake. Hata na hivyo, nikikwambia useme kuhusu hili, utanijazia ukurasa bure hapa na hao unaowaambia masikio yao yana nta na pamba kwa pamoja. Unataka chenji yako? (tena si chenji basi, ni deni). We umeona mi nimeshindwa kuandika lolote nimebaki kuripoti tu.
Mtu mmoja kashauri tuache kujadili hili suala maana ni kujitafutia ugonjwa wa mtindio wa ubongo bure.
Mwingine kasema leo ni Kimeo Dei na besdei ya Shetwain.
Mi nimesema, tudei is tudei, whomever says tumoro is a big laya. Fikiria hili la Zombe, jumlisha Chiluba hana kosa kisha umalizie na Ivo Mapunda kibarua kuota majani huko Ethiopia.
What a Black Monday this was!

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads