wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, July 30, 2009

TweetThis! Waraka kwa Watanzania kutoka kwa watumishi wa Bunge

Nimeupata ujumbe huu kwa njia ya barua pepe na nimeona vyema kabisa kabisa kuiweka hapa ili ikiwa haya yaliyosemwa humu ni kweli, basi yafanyiwe kazi na tusiishie kuja kulaumia kuwa mbona tulifahamu na tusipashane habari. Ikiwa yaliyoandikwa humu si kweli, basi si neno, hakuna litakalotukia. Na mtu asiniambie tunatumia uhuru wa mawasiliano vibaya, acheni maneno na hulka zenu za kipumbavu za kuzuia kila jambo linaloandikwa kuihusu hii nchi. Ni yetu wote. Mnatuwekea vipingamizi kama vile mlipewa upendeleo sijui na nani kuwanyanyasa wenzenu. Vyeo vyenu ni dhamana, msipokuwa makini ndivyo vitakavyowasimamisha kizimbani siku ya kiama. Mtajuuuta kuvikalia hivyo viti.

Waraka wa wazi kwa Watanzania kutoka kwa watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ufisadi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania

Ndugu zetu Watanzania. Sisi ni wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tunapenda kutumia nafasi hii kuwafikishia ujumbe huu muhimu kupitia waraka wetu huu wazi kwenu.

Tunaomba ifahamike kuwa, haikuwa nia yetu hata kidogo kutumia njia hii kueleza mambo ya siri sana yanayofanyika ndani ya Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Tumelazimika kuchukua hatua hii baada ya jitihada zetu za kufikisha taarifa hizi pamoja na malalamiko yetu ngazi husika kutokufanikiwa. Aidha, mbali na hayo hata juhudi za ziada tulizochukua kuwasiliana na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kueleza uvundo ulio katika taasisi hii hazikufanikiwa kutokana na nguvu ya pesa iliyotumika na ofisi ya bunge kuwafunga midomo waandishi wa habari na wahariri wao.

Lakini kikubwa zaidi kilichotusukuma kuandika waraka huu kwa Watanzania wote ni baada ya kubaini kuwepo kwa njama za kuchoma moto ofisi ya uhasibu ya bunge ili kupoteza kumbukumbu muhimu kabisa za matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi ya ofisi ya bunge yaliyofanywa Spika pamoja na marafiki zake.. Tunaomba watanzania waelewe kuwa kuanzia sasa ofisi hizo zitaungua moto wakati wowote. Na kama jambo hili litatokea watanzania wote hasa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndivyo vinavyopaswa kulaumiwa zaidi kwa kushindwa kubaini ufisadi wa kutisha katika ofisi hii hadi njama za kuchoma moto ofisi..

Ndugu zetu Watanzania, tunapenda kuwafahamisha kuwa Ofisi ya Bunge, katika kipindi cha miaka mitatu na ushee, imekuwa ikikaliwa na mafisadi wanaojificha katika jina la vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi, na kiongozi wao wa Mkuu ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Tunajua kuwa wapo baadhi ya Watanzania wenzetu wanaoweza kuona kuwa tunasema mambo ya uongo au tusiyo kuwa na uhakika nayo. Kwa kuthibitisha haya tunayoyasema, tunaomba tueleze mambo machache machafu ya kifisadi yanayofanywa na Spika Sitta pamoja na wabunge kadhaa walio karibuni naye, wakisaidiwa na badhii ya watendaji wenye nyadhifa kubwa katika Ofisi ya Bunge.

*Tangu Spika alipoingia madarakani amekuwa akiiongoza ofisi ya bunge kidikteta. Analazimisha kupatiwa fedha kutoka katika ofisi ya bunge anapokuwa katika ziara zake binafsi katika Jimbo lake la Urambo Mashariki. Ushahidi wa haya upo katika vocha za malipo haya. Tunaomba wakaguzi waje wakague watakuta haya.

*Spika Sitta amekula akilazimisha kukiukwa kwa kanuni za bunge ili tu kuwapa nafasi wabunge wenzaki walio katika kambi moja kuisulubu serikali ili kuwaaminisha wananchi serikali ni ya hovyo bali yeye na wabunge hao ndiyo wana uchungu wa kweli na taifa hili.

*Spika Sitta hafuati taratibu za uchukuaji fedha za ofisi. Huwa anaamrisha apewe hata fedha za kununua vifaa muhimu vya ofisi akiwa hana fedha na anapokuwa akizihitaji. Fedha zilizopotea kwa njia ni mabilioni, lakini hakuna anayemuhoji.

*Spika Sitta hata siku moja tangu aliposhika wadhfa huo, amekuwa hafuati taratibu za kawaida za sheria ya manunuzi umma katika mambo mengi hapa bungeni. Yota haya ushahidi wake upo ofisi ya uhasibu lakini analindwa na kundi la wabunge wanaodai kuwa wanapoambana na ufisadi kwa sababua anakula nao.

*Spika Sitta ameshinikiza kukodishiwa nyumba ya gharama kubwa. Dola za Marekani 8,000 kwa mwezi wakati alikuwa amepewa nyumba nzuri tu ya serikali huko Oysterbay. Baada ya kukodishiwa Nyumba hii, alilazimisha pia Ofisi ya Bunge itoe sh milioni 250 kwa ajili ya kununua samani za ndani alizodai kuwa ndizo zinazolingana na hadhi yake ya Spika.

*Spika Sitta ambaye baada tu ya kuingia katika wadhfa wake alinunuliwa gari jipya aina ya benz. Sasa amelichoka likiwa hata halijamaliza miaka mitatu, anataka kununuliwa jingine na amekwishamuarua Katibu wa Bunge, Thomas Kahililah ambaye ni swahiba wake mkubwa kwa sababu wanakula pamoja kutoa kiasi cha sh milioni 367 kwa ajili ya kununulia gari hilo . Tayari zimekwishalipwa sh milioni 270. wakati haya yakifanywa na Spika, anajua fika kuwa taifa liko katika hali mbaya kifedha na bunge liko katika hali mbaya zaidi kiasi kwamba vikao vyake vinakatishwa.

*Spika Sitta ana sifa mbaya ya ukware. Tangu ameshika wadhfa huo amekwishatembea na wabunge wanawake wa bunge la Jamhuri ya Muunagni ambao ni wake za watu zaidi 12 na ushahidi wa hili upo kwao wenyewe wabunge. Akikanusha hili tunaomba watumwe maofisa usalama waje wafanye uchunguzi kwa siri, watabaini jinsi anavyofanya ufirauni na wake za watu ambao ni wabunge. Anatembea mpaka na wabunge wa upinzani halafu anajitapa kuwa ni Spika wa wote hivyo lazima awalee. Ni aibu lakini huo ndio ukweli.

*Ni mtu anayevidhalilisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa sababu amekuwa akisema wazi kuwa hakuna chombo chenye nguvu za kumchunguza yeye na bunge kwa sababu bunge ni dola. Na ukweli sasa umeanza kubainika kwa sababu ni dhahili kuwa serikali inamuogopa Spika na timu ya wabunge wake. Ndiyo maana licha ma malalamiko na ushahidi mwingi tuliokwishatoa toa kuhusu ufisadi wake, si TAKUKURU, polisi waka usalama wa taifa waliothubutu hata kumuhoji.

*Spika amewagawa wafanyakazi wa Bunge wa Idara ya Uhasibu. Wapo ambao amewateua kuwa watu wake ambao wanashughulika na malipo yake yeye, makamishina wa tume ya huduma ya bunge ambao wanakula naye pamoja, pamoja na wabunge kadhaa ambao uchunguzi wa kina ukifanyika watafahamika.

*Wahasibu hawa pamoja na Kashililah ndiyo wanaolipwa mishahara mikubwa, wanalipwa posho hata kama hawakufanya kazi za ziada na wanasafiri na Spika kila anapokwenda nchi za nje. Watumishi hao ni kama ifuatavyo hapa chini.

1-Evance Nkanta- Huyu ni muhudumu wa idara ya uhasibu. Ni mtu wa karibu sana na Spika Sitta pamoja na Mhasibu Mkuu wa Bunge, Bwana Kombe. Cha kushangaza hakifanyi kazi za bunge kama inavyotakiwa, kazi kubwa ni kupeleka fedha katika akaunti ya Spika na Kombe au kupeleka fedha katika miradi yao . Nkata ana miradi mingi na utajiri mkubwa wa kutisha. Anamiliki taksi nyingi mjini Dodoma na Dar es Salaam , ana nyumba za kifahali Dar na Dodoma na anamilioni ya fedha katika benki kadhaa hapa nchini. Ana sauti kubwa kuliko hata baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa bunge. Akataka ufukuzwe kazi anamwambia tu Spika au Kashilalah kuwa kuna matu anafuatilia nyendo zao, kesho mtu huyo anafukuzwa kazi. Hii ndio maana Spika na tume yake ya huduma za bunge imepipitisha sheria mpya tofauti na ile iliyosainiwa ya rais inayompa Spika Sitta na tume hiyo madaraka makubwa ya kuajiri au kufukuza mtumishi yoyote, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.

2-Rose Mlalase- Huyu ameajiliwa hivi karibuni bila kufanyiwa usaili. Ana uhusiano wa kingoni na Spika Siita. Ndiye mshika mikoba yenye nyaraka za siri za Spika Sitta. Huwa hatumwi na mtu mwingine zaidi ya Spika mwenyewe katika masuala ya kihasibu. Katika muda mfupi usiozidi mwaka mmoja kazini amekwishapa mali nyingi zikiwemo nyumba kadhaa na magari. Huwa analipwa posho za vikao na safari za nje bila kufanya kazi yoyote au kusafiri kwa maelekezo ya Spika mwenyewe. Mhasibu Mkuu, Bwana Kombe. Ana mabilioni ya shulindi katika benki za CRDB, NMB na NBC. Amejenga hotel ya kisasa inafahamika kwa jina la African Dream, mjini Dodoma kwa kutumia fedha za bunge. Hana sifa za kuwa mhasibu mkuu wa bunge kwa sababu ana cheti cha chini kabisa cha uhasibu badala ya NAD. Amefanya mitihani kadhaa ya uhasibu lakini anashindwa.

Bwana Kombe, akitaka pesa kwa ajili ya kupeleka kwenye miradi yake huwa anajiidhinishia hadi milioni 100. ndiye anatoa fedha za bunge kwa ajili ya shughuli binafsi za Spika. Anahusika kulipa yeye mwenyewe malipo yoyote kwa mbunge ambaye Spika ataamuru alipwe bila maelezo yoyote kuhusu kutolewa kwa fedha hizo.

3-Hassan Mohamed-alifeli diploma ya uhasibu mwaka 2005 katika chuo cha uhasibu Arusha. Hivi sasa anasoma IFM. Yuko chuoni lakini ndiyo msimamizi mkuu wa masuala ya fedha katika ofisi ndogo ya bunge mjini Dar es Salaam. Naye ana utajiri wa kutisha ambao haulingana hata kidogo na kipato chake na umri wake kazini.

4- John Joel- Ni mhasibu lakini kwa sasa amehamishiwa katika ofisi ya utawala. Mdiyo msiri mkuu wa Kashililah kiasi kwamba akisafiri ofisi huwa anaiacha mikononi mwake. Ameteuliwa hajamaliza kata miezi minne lakini sasa anawazifdi hata walio na miaka 10 kazini.

5-Bwana Mtenda- Huyu alichukuliwa na Spika mwenyewe na kuwekwa uhasibu pasipo kwa sababu ambazo mpaka sasa haziko wazi. Lakini ndi miongoni mwa watu wanaohusika kushughulikia vocha za malipo ya Spika, makamishina na Tume ya huduma za bunge na kundi la wabunge marafiki wa Spika Sitta. Mtenda ana historia mbaya katika utumishi wa umma lakini inashangaza kuona Spika Sitta akiwa amemng’ang’ani katika kufanya kazi ofisi ya bunge. Alikuwa mtumishi wa idara ya ustawishaji makao makuu Dodoma (CDA) ambako aliondolewa kutokana na kuandamwa na kesi lukuki ambazo almanusura zimpeleke gerezani. Kila mara huwa anachukua fedha kwa ajili ya kwenda semina nje ya nchi lakini huwa anaishia Dar es Salaam kuponda na baadaye kurudi Dodoma . Haifahamiki ni kwanini anafanyiwa hivi na wakubwa.

6- Bwana Ndalo- huyu ndiye anayechukua masurufu yote ya Spika Sitta. Anahusika kuwalipa wote walio katika orodha ya kulipwa na Spika, iwe wanasiasa au watu binafsi. Ni kama kichwa cha Spika. Huwa anavchukua masurufu mengi hadi anashindwa kurudisha. Kwa ufupi sana hii ndiyo timu ya Spika Sitta hapa bungeni. Timu ambayo inashirikiana nayo kujitajilisha kupitia bunge.

Tunawaomba Watanzania mfahamu kuwa Serikali inamuogopa Spika Sitta kwa sababu amefanikiwa kuwa na nguvu kubwa ya wabunge wenye uwezo mkubwa wa kuongea na kujenga hoja zao. Inafahamu fika ufisadi unaofanyika hapa kuwa ni mkubwa kuliko hata ule wa Richmond lakini kamwe haiwezi kuthubutu kumgusa Spika Sitta kwa vile anaweza kuiangusha. Hivyo kwenu Watanzania wote kama tunaamua kukaa kimya huku haya yakiendelea sawa au tuchukue hatua ya kushinikiza uchunguzi huru kufanyika.

Kama wafanyakazi wa kawaida, kwa kizingatia baadhi ya wabunge akiwemo Spika wanavyohuburi vita dhidi ya ufisadi na mambo yanayofanyika hapa tumeona bi bora kuyaweka wazi ili watanzania waamke na kushinikiza kuundwa tume huru ya kuchunguza ufisadi ndani ya ofisi ya Spika.

Waraka huu tunaomba ukikufikia upeleke kwa mtanzania mwenzako ili sote tujue jinsi wakubwa wetu tuliowachagua kwa kura zetu wanavyoishi maisha ya utukufu huku wakituhadaa kuwa wanapambana na wanatumia jasho letu kihiana kuishi maisha ya utukufu. Tuwezalo tumefanya kwa faida ya taifa letu. Mungu ni shahidi yetu.

Huu ndio ujumbe wetu.
Asanteni sana.
Mungu Ibariki Tanzania

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads