wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, July 29, 2009

TweetThis! "Mwendawazimu" Anney Anney apelekwa kwa Pilato

Hii picha aliipiga bro Msimbe wa Lukwangule Ent. siku chache zilizopita. Leo mambo yamekuwa si mambo, soma habari yake hapo chini

Raia wa Irak kizimbani kwa kuwakashifu Mwinyi, Mkapa


Raia wa Irak, Anney Anney (59), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam kujibu shtaka la kutoa maneno ya uchochezi yenye hisia za kusababisha uvunjifu wa amani. Anadaiwa kutoa maeno hayo wakati akiwakashifu viongozi wastaafu wa Tanzania.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka na Mrakibu wa Polisi, Naima Mwanga, mbele ya Hakimu Samwel Maweda.

Mrakibu Mwanga alidai kuwa Julai 23, mwaka huu katika eneo la Ikulu jijini Dar es Salaam, na kuanza kumshutumu Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akisema aliuza Azimio la Arusha.

Aliendelea kudai kuwa kana kwamba haitoshi, mshtakiwa huyo alimshutumu Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisema aliuza mashirika ya umma na ardhi ya wananchi wa Tanzania kwa waarabu na wazungu bila kujali utu na utaifa. Mwendesha mashataka huyo aliongeza kudai kuwa mshtakiwa huyo baada ya kuwakashifu viongozi hao, alihitimisha kwa kutoa maeneo ambayo pia yanaweza kusababisha vurugu na uchochezi nchini pale alisema: “Udumu ujamaa na kujitegemeana, zidumu fikra za Mwalimu Nyerere."

Vilevile Mwanga alidai mshtakiwa huyo katika matamshi yake alidai Rais Jakaya Kikwete amekuwa analinda ardhi ya Watanzania, utaifa na uzalendo.

Mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 10, mwaka huu.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads