wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, July 28, 2009

TweetThis! Mkutano Mkuu wa CCM Tawi la London 26-07-2009

Habari hii imeletwa na M.O wa Uingereza:

Wana CCM wa matawi ya nje ya nchi wametakiwa kuitangaza Tanzania kwa mema ikiwemo fursa mbalimbali zilizoko Tanzania. Hayo yanmesemwa jana nchini Uingereza na Katibu wa NEC Uchumi na fedha Amos Makala wakati akifungua Mkutano Mkuu wa CCM Tawi la London Uingereza ulihudhuriwa na mamia ya WanaCCM waishio Uingereza.

Amewataka wana CCM kufanya kazi hii kwa sababu kubwa mbili;
kwanza wana CCM kama Watanzania
Pili Wana CCM kama wadau wa serikali yao ya CCM iliyoko madarakani.

Amewataka wana CCM waishio nje ya nchi kushirikiana na serikali yao kuendelea kushawishi uwekezaji, watalii kuja Tanzania huku wakiwahakikishia sifa kuu ya Tanzania ya amani na utulivu.

Adha Makalla amewabeza Watanzania wengine aishio nje ya nchi ambao wamekuwa siyo wazalendo ambao siku zote wamekuwa wakibeza maendeleo mazuri ya CCM na sifa nzuri ya Tanzania.

"Nasema makada wa CCM fanyeni kazi hii kwa nguvu kubwa na wapuuzeni hao wapika majugu na fitina kwa maslahi yao binafsi"

Kuhusu hali ya kisiasa Makala amewahakikishia wana CCM waishio nje ya nchi kwamba Tanzania ni shwari na hivi sasa vyama vya siasa vinajipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani.
Na amewahakikishia wana CCM wa Tawi la London kwamba CCM imejipanga vizuri na itashinda chaguzi zote kwa kishindo.
Amesema utekelezaji wa Ilani wa uchaguzi mwaka 2005 ndiyo kipimo kwa CCM kuendelea kuungwa mkono na imejirihirisha kwa serikali ya awamu ya nne kuendelea kwa kasi kuwaletea Watanzania maendeleo.

Aidha kwa upande mwngine, wana CCM Tawi la London walipenda kujua Chama inashughulikiaje kero za Muungano na ufisadi. Kuhusu Muungano Makala aliwaambia Chama cha Mapinduzi kinaendelea kuamini kwamba muundo wa muungano wa serikali mbili ndiyo unaofaa na kwamba kero zilizopo zitashughulikiwa pasipo kuathiri muungano wetu na CCM itahakikisha Muungano huu inadumishwa.

Kuhusu ufisadi amewaambia kwamba serikali ya CCM imechukua hatua mbalimbali kuwafikisa mahakamani watuhumiwa wa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za Umma na madaraka ya umma. Amesema ni mahakama pekee ndiyo itakayotoa hukumu na kuwasihi Watanzania kuheshimu Mahakama.

"Wapo watu nyumbani ambao wakati serikali ikichukua hatua hizi wameonekana kutoridhishwa. Wao ndo wamekuwa polisi, waendesha mashtaka na majaji. Kwa hiyo ningewaomba kwamba tuendelee kuheshimu mahakama. Serikali ya awamu ya nne ina dhamira ya dhati kupambana na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za Umma. Dhamira hii imejirihirisha kutokana na jitihada za makusudi za Raisi Kikwete kuiongezea uwezo taasisi ya kupambana na rushwa.

Mwisho Makala aliwataka Watanzania na Makada wote waishio nje ya nchi kuendelea kushirikiana na serikali yao kuleta maendeleo ikiwepo na wenyewe Watanzania hao kuwekeza nyumbani.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads