wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, May 10, 2009

TweetThis! Subhash Patel amjibu R. Mengi

MFANYABIASHARA Bw. Subhash Patel amekana tuhumu za ufisadi zilizoelekezwa kwake na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi kuwa ni mmoja wa mafisadi papa watano.
Akizungumza Dar es Salaam jana kupitia kwa Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wake wa Motisun Holdings Limited inayoendesha viwanda na hoteli mbalimbali nchini, Bw. Aboubakary Mlawa, alisema si mara ya kwanza kwa Bw. Mengi kumshutumu tena bila sababu yoyote ya msingi.

Alisema katika tuhuma zake nyingi Bw. Mengi amekuwa akimhusisha na ufisadi katika mchakato wa kumpata mbia wa kushirikiana na Serikali katika mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na wa chuma cha Liganga iliyopo mkoani Iringa.

Bw. Mlawa alisema tuhuma nyingine zilizotolewa na Bw. Mengi kupitia moja ya chombo chake cha habari ni kuwa kampuni ya MMI Steel Mills Limited inayomilikiwa na Bw. Patel ilitoa rushwa kwa wanakijiji na pia anafadhili gazeti linalomchafua.

"Napenda kuuarifu umma kwa si Bw. Subhash Patel wala kampuni yake yoyote iliyopewa mradi wowote katika eneo la makaa ya mawe ya Mchuchuma. Tuelewavyo sisi mchakato wa kupata mbia au wabia kwa mradi huu unaendelea. Hivyo habari hizi si kweli na ni uzushi mtupu.

"Kilichopo ni kwamba moja ya kampuni zetu iitwayo MM Steel Resource Public Limited Company ilishiriki katika zabuni namba PA/068/2008/NDC/PPP/01 ya Aprili 2008 ya kutafuta mwekezaji wa ndani ambaye atakuwa na ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) katika kuanzisha na kuendeleza mradi wa kuzalisha chuma kiitwacho 'sponge'.

"Kampuni yetu ilishiriki zabuni hii kwa kufuata sheria na taratibu zote zinazohusiana na ununuzi wa umma. Mchakato wa kizabuni bado unaendelea chini ya Uenyekiti wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ukiziangalia shutuma hizi kwa undani, utaona wazi kuwa zina nia ya kuingilia mamlaka zinazohusika katika kuwapata wawekezaji katika miradi hii miwili," alisema Bw. Mlawa.

Kuhusu kutoa rushwa kwa wanavijiji, alisema Bw. Patel hajawahi kufanya hivyo isipokuwa anatumia haki aliyonayo katika kusaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii nchini.

Alisema Bw. Patel ama kupitia kampuni zake mbalimbali amekuwa akitoa misaada ya maendeleo kwa makundi mbalimbali ya wananchi kama anavyofanya Bw. Mengi ambapo kwa mwaka jana pekee alitumia zaidi ya sh. milioni 800 ambapo misaada hiyo alitoa hata mkoani Kilimanjaro ambapo hana maslahi yoyote ya kibiashara.

Pia alisema hamiliki, hafadhili wala hana hisa katika gazeti la Sauti Huru wala chombo chochote cha habari lakini hutangaza huduma zake na bidhaa zake kupitia vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya Bw. Mengi.

Aliwataka wananchi watambue kuwa yeye ni Mtanzania halisi aliyezaliwa na kukulia Kijiji cha Lugoba mkoani Pwani na uwekezaji wake nchini hauhamishiki, hivyo hawezi kutoroshea fedha zake nje ya nchi kama alivyoshutumiwa.

Bw. Mlawa alisema wanachofahamu ni kuwa uhusiano uliopo kati ya wawili hao ni wa kibiashara tu ambapo maeneo mengi ya viwanda ambayo yalikuwa yakimilikiwa ama kuhusiana na Bw. Mengi yamenunuliwa na kampuni zinazomilikuwa na Bw. Patel.

Kuhusu kwa nini Bw. Patel hakwenda mahakamani kama aliona ametuhumiwa uongo na Bw. Mengi, Mwanasheria wake Bw. Deusdedit Duncan alisema ni uamuzi wa mtu binafsi lakini bado hajaamua kama atakwenda au la - majira.co.tz

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads