Baadhi ya Polisi hawajui mipaka ya kazi zao
Ikiwa kweli jambo hili limetukia kama ilivyoripotiwa, basi bila ubishi Jeshi la Polisi la Tanzania linatakiwa kuangalia kwa kina na kuondoa kabisa walakini mkubwa uliopo ndani ya Jeshi hilo.
Kilichoripotiwa hapa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki ya msingi ya binadamu yeyote yule aliye huru na anayeishi katika nchi huru bila kujali misingi ya umri, jinsi ama tabaka la aina yoyote ile.
Kilichoripotiwa hapa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki ya msingi ya binadamu yeyote yule aliye huru na anayeishi katika nchi huru bila kujali misingi ya umri, jinsi ama tabaka la aina yoyote ile.
Polisi wamweka rumande mtoto babake ajitokeze
Sunday, 10 May 2009 09:58
Na Glory Mhiliwa, Arusha
JESHI la polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mtoto wa miaka tisa aitwaye Richard Grayson mkazi wa Shangarai ili kumshinikiza baba yake anayetuhumiwa kuhusika katika matukio ya ujambazi ambaye anadaiwa kukimbia kusikojulikana kujisalimisha.
Tukio hilo lilitokea juzi alfajiri majira ya saa kumi na moja baada ya askari polisi wakiwa na gari aina ya Land Rover Defender kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambapo walipomkosa waliamua kuondoka na mtoto huyo.
Mtuhumiwa huyo Grayson Mollel (34),Jeshi hilo linadai kuwa linamtafuta kutokana na tuhuma za ujambazi zinazomkabili. Hata hivyo halikuwa tayari kutaja baadhi ya matukio ya ujambazi ambayo mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika nayo.
Akizungumza na Majira Jumapili kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Bw. Basilio Matei alisema kuwa taarifa za mtoto huyo kushikiliwa ili kumshinikiza baba yake kujisalimisha hazijawasilishwa kwake.
‘Mimi ndio kwanza nasikia kutoka kwenu lakini naahidi kufuatilia ili kujua ukweli wa tukio hilo kama kweli mtoto huyo alikamatwa na kulazwa rumande kwa kosa ambalo linamhusu baba yake nitawapatieni taarifa kamili’ alisema Basilio.
Aidha mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi ya Moivo wilaya ya Arumeru anadaiwa kutiwa nguvuni na askari polisi wakiwa na silaha baada ya kuvamia nyumbani kwao eneo la Shangarai wilaya ya Arumeru.
Hata hivyo askari hao baada ya kumchukua mtoto huyo walimwamuru wamweleze baba yake alipo ambapo aliwaelekeza nyumba ya mama yake mdogo ambae ni mke mdogo wa baba yake anayeishi Sanawari. Hata hivyo hawakufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na ndipo walipoamua kumkamata na mama huyo pia. Aidha mama huyo aliyefahamika kwa majina ya Georgina Grayson alikamatwa na kuswekwa rumande kama ilivyo kwa mwanae
Hatua ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa aliyekuwa ametoka hospitali ya wilaya ya West Meru alipokuwa akiuguza kifua baada ya kuanguka kwenye mti kumetafsiriwa na wananchi kuwa jeshi la polisi linakiuka haki za mtoto. Bi Neema Florence ambae ni mkazi wa Shangarai anasema kuwa mtoto huyo ni mdogo sana
kulazwa mahabusu ya watu wazima tena kwa kosa alilofanya baba yake - http://www.majira.co.tz.
1 feedback :
Ninachelea kuamini tukio lililoripotiwa kuhusu polisi kumuweka rumande mtoto ili baba yake ajitokeze. Habari hii sio ya kweli, na kama ni kweli basi, polisi sasa imevuka mipaka ya kazi zao. mtoto ana kosa gani? kila anayeshikiliwa na polisi ni lazima apelekwe mahakamani, je huyo mtoto atapelekwa mahakamani? kwa kosa gani? la baba yake? haiingii ikilini na imekaa vibaya hii. nashukuru si mtoto wangu. jamani wanaharakati za haki za binadamu na za watoto mko wapi?