wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, March 07, 2009

TweetThis! Third place CHAN 2009 Senegal vs Zambia [updated]

Mshindi wa tatu CHAN ni Zambia kwa ushindi wa 2 - 1 dhidi ya Senegal.

Matokeo hadi sasa ni Senegal 1 na Zambia 1 leo anaotizama online wamelipia, nadhani Malkiory anafaidi sana hii mechi. Mi sijalipa naishia kupekua tovuti ya CAF Online kupata majibu ya kwenye ubao wa matangazo!
Kick off time 16:00hrs GMT
hopefully the Senegalese Tv embedded here will show it live
Alternative links : http://www.lc2international.tv and http://www.tv-direct.fr/live_lc2.php

8 feedback :

Anonymous said... Sat Mar 07, 07:53:00 AM MST  

ahsante sana dada subi kwa jitihada zako hizi.
sasa nilikuwa nauliza inawezekana kutuunganisha na TV za nyumbani hasa kwenye taarifa za habari?
manake hapa naona umetuunganisha na tv kuangalia mechi ya zambia na senegal na tv inapatikana safi tu.
ahsante
martin,
UK

Anonymous said... Sat Mar 07, 08:16:00 AM MST  

Martin,
Pole kwa usumbufu nami natamani sana ningeweza kuunganisha Tv za nyumbani lakini tatizo ni kuwa hizo Tv hazipatikani mtandaoni. Kuna wakati fulani iliwezekana kuzipata kupitia JumpTv, zilikuwepo Channel 10, StarTv na TvT ila baada ya muda wa majaribio na JumpTv kwisha nao wakatokomea kwa sababu wanazozijua wao sielewi ikiwa ni kutokuwa na uwezo wa kulipia, kutokupata biashara, kutokupata wateja, kushindwa kujitangaza, mitambo na nishati isiyo hakika au mchanganyiko wa hayo yote.
Kwa sasa ni KBC tu iliyobakia JumpTv BURE, zilizobakia ni za kulipia.
Wapo watu wanaoishi Ulaya na Asia wanasema wanaweza kutizama Tv za Tz kupitia JumpTv kwa kulipia na wengine wanalipia na kutumia satellite kuzipata.

Anonymous said... Sat Mar 07, 11:11:00 AM MST  

Bila shaka mpira utakuwa umekwisha, sikuweza kulipia, kwani nilitegemea hawa Wasenegal wangeturushia. Any way kesho hakusi mtu final live.

Anonymous said... Sat Mar 07, 01:30:00 PM MST  

anhaa kumbe!!
ah basi bwana. hao wenye tv zao tz wajue kmwamba kama tv zao ni kwa watanzania basi kuna watanzania nje!!
haya dada subi lakini nakupongeza sana kwa kuwa mstari wa mbele kutufahamisha yatokeayo nyumbani tena kwa taarifa zisizo za kiudaku. hongera sana mungu akutie nguvu na moyo katika hili.
martin
UK

Anonymous said... Sat Mar 07, 02:59:00 PM MST  

Martin shukrani kwa pongezi.
Malkiory, nadhani mpira ulikwisha muda, mi nilichelewa kuandika matokeo ya mwisho kwa kuwa nilipata dharura nikawa mbali na mawasiliano ya intaneti.
Kesho tutadowea kwako utuelezee yatakayojiri ama tupitie mgongo wako kupata kuona mechi. 8-)

Anonymous said... Sat Mar 07, 03:14:00 PM MST  

Kesho mapema kabisa nitalipia subscription fee ya myafricanfootball. Then nitawapa details ili na nyie muweze kuitizama live.

Anonymous said... Sat Mar 07, 07:50:00 PM MST  

Dada mimi nina ka-tabia ka kuchunguza na kuchunguza na kuchunguza mpaka basi.
sNimeona ka .77 paleeee kwenye http: yako. Hongera saana. Naona unakua kama unavyostahili na kisha kutuonesha njia nasi tusonge.
sKazi njema sana.
sKuhusu game nashukuru mno. Asante kwa kila update, asante kwa elimu na uhabarishaji na mwisho ASANTE KWA KUWA WEWE.
s Baraka kwako na siku njema ya wanawake / mabinti ulimwenguni

Anonymous said... Sat Mar 07, 11:29:00 PM MST  

Mube ni kweli kuwa nimeweka .77 kama favicon, nilikuwa niiweke muda mrefu lakini nilikuwa ninaahirisha kwa sababu nilitaka kujua faida hasa hasa ya kuwa nayo. Nitaelekeza nilivyoiweka kwani ni rahisi sana, kisha mwenye kupenda atajaribu.
Jana nimepita barazani kwako nimekutana na mada zako za changamoto (mbili nilikuwa sijazisoma) nilipomaliza na kuwasikiliza wajumbe wa kijiji nikaondoka kichwa nimekiinamisha kwa kutafakari kwa kuwa mada na chambuzi mbalimbali wanazoandika wanablogu mbalimbali huwa zimejitosheleza. Laiti watawala wangekuwa wakwenda na kasi ya chambuzi na maoni ya WaTanzania, tungeshapiga hatua kiasi fulani mbele. Ninajua wanasoma na wengine wanapelekewa zilizochapishwa wanajisomea, angalao ujumbe unafika.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads