TCRA - Usajili wa “SIM-CARD” Tanzania
Kutokana na kukua kwa tekinolojia ya mawasiliano, kumekuwepo na ongezeko kubwa la vifaa vinavyotumika kusambaza mawasiliano ya simu za mikononi. Baadhi ya simu hizo zina “SIM-CARD” zinazoweza kutolewa na baadhi haziwezi kutolewa kwa vile zimejengewa kwenye simu za mikononi.
Pamoja na ukweli kuwa watumiaji wengi ni waaminifu, wanaheshimu sheria na ni wastaarabu, kuna wachache ambao wanatumia huduma hii isivyo. Kutokana na kero ya watumiaji wachache wenye nia mbaya na wasiowastaarabu, Mamlaka imeagiza watoa huduma za mawasiliano kuanza utaratibu wa kusajili watumiaji wote wa simu za mikononi.
Utaratibu ufuatao utafuatwa katika utekelezaji wa zoezi hili.
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

- Wateja wanaolipa baada ya huduma wataendelea kusajiliwa kwa utaratibu ambao tayari upo katika kila kampuni;
- Wateja wanaopata huduma kama M-Pesa, E-Pesa, E-Fulusi mobipawa, m-Commerce n.k wataendelea kusajiliwa kwa utaratibu ambao tayari upo;
- Wateja wengine wote ambao laini zao hazijasajiliwa wanapaswa kusajiliwa na makampuni ya simu husika wanakopata huduma kuanzia tarehe 1 Julai, 2009;
- Kuanzia tarehe 1 Julai, 2009, wateja wote wapya wa huduma ya malipo kabla (prepaid) watapaswa kusajiliwa kabla ya kuuziwa laini ya kampuni yoyote ya simu za mkononi;
- Kuanzia tarehe 1 Machi, 2009, makampuni yote ya simu yanapaswa kutekeleza utaratibu wa kuruhusu namba zote zilizoko kwenye mitandao yao kutambulika kwa mpokeaji wa simu. Jambo hili si la hiari bali ni agizo.
- Sheria husika ya usajili wa laini za simu za mikononi iko katika hatua ya mwisho kwakuwa jambo hili si la mjadala tena;
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
0 feedback :