Marufuku ya dawa ya Metakelfin Tanzania - TFDA
Mamlaka ya udhibiti Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imepiga marufuku uagizaji, uingizaji na usambazaji wa dawa ya kutibu malaria aina ya Metakelfin baada ya kubainika kuwa dawa hizo zina kasoro na nyingi ni za bandia. Dawa hizo zitahitajika kurejeshwa kwatika maabara ya Laborex kwa uchunguzi zaidi.
Dawa hizo bandia hazina kiwango cha kemikali inayohitajika kwa ajili ya kuua vimelea vya malaria.
Anayeonekana katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, bi Margareth Ndomondo-Sigonda wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo.
Habari hii imeripotiwa na Father Kidevu na Lukwangule Ent.

0 feedback :