Malkiory Matiya anakukaribisha katika blogu yake
WaTanzania wanashika kasi katika kushiriki nia na mawazo yao kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo za siasa, uchumi, michezo, elimu, afya, utamaduni, imani nk. Ni kwa sababu hii basi ninayo furaha kujumuika katika dunia ya TeknoHaMa kwa njia ya ku-blogu na kumtambulisha kwenu MTanzania mwenzetu Malkiory Matiya!
Malkiory anasema kuwa blogu yake itakuwa chachu ya kusemea na kukosoa kile ambacho anaona hakijakaa sawa popote pale katika nchi ya Tanzania.
Tafadhali changia mawazo yako huru katika blogu ya Makiory kupitia: http://www.malkiory-matiya.blogspot.com
Malkiory ni mmoja wa rafiki zangu katika Google Connect & Follow, tizama hapo mwisho wa blogu utamwona katika ulimwengu wa kublogu!
Malkiory anasema kuwa blogu yake itakuwa chachu ya kusemea na kukosoa kile ambacho anaona hakijakaa sawa popote pale katika nchi ya Tanzania.
Tafadhali changia mawazo yako huru katika blogu ya Makiory kupitia: http://www.malkiory-matiya.blogspot.com
Malkiory ni mmoja wa rafiki zangu katika Google Connect & Follow, tizama hapo mwisho wa blogu utamwona katika ulimwengu wa kublogu!
8 feedback :
Mzee wa Changamoto nashukuru sana kwa kunikaribisha jamvini na pia kunikumbusha kuhusu sehemu ya comments huru.
Binafsi ni kama nilihisi kitu kama hicho, maana sijawahi kupata commments hata siku moja.Naomba nikiri kuwa tekelinalokujia imenipiga chenga kidogo.
Ili kuruhusu open comment doesn it mean that i have to remove word verification? naomba ushauri wenu hapo, Mzee wa Changamoto na Da. Subi.
Malkiory, kuruhusu maoni si lazima kuondoa 'word verification' kwani hiyo ni uchaguzi wako. Ukiwa ume-login kwenye blogu yako sehemu ya 'Settings' kisha 'comments' hapo fanya uchaguzi kadiri unavyotaka kwani mengi ni 'yes' na 'no' na unaweza kubadilisha badilisha vyovyote unavyotaka na kwa wakati wowote kadiri unavyopenda.
Asante sana Da Subi. Nadhani maelezo yamejitosheleza hapo. Asante Melkiory kwa "kusikia kilio chetu" na tuko pamoja
Nawashukuru kwa namna ya pekee Subi na Mzee wa Changamoto kwa kunikaribisha kwenye anga za kublog. Ila nimesikitishwa na baadhi ya owners mashuhuri wa blog kwa kuiipuuzia ombili langu la kiitambulisha blog yangu.
s
Nimegundua kuna wapiginga maendeleo wengi tanzania. Siamini kama ni suala tu la ubize maana baada ya kufuatilia hiyo blog wanapublish mambo ambayo yana umuhimu kidogo katika kulijenga taifa. Mfano, kama blogger unapoipa harusi priorty na ukaminya developemental issues, hii inauma sana.
Malkiory, usisikitike sana kuhusu kutokukaribishwa ukatetereka, songa mbele alimradi umeshaanza kublogu, nawe siku moja utawakaribisha wengi watakaotaka kujifunza kutoka kwako, haya yote yanatukumbusha kuwa huku ndiko kujifunza katika utofauti wetu. Karibu sana!
Nashukuru Subi, kwa kinipa moyo. Naahidi kusonga mbele, nyuma mwiko/ forward ever backward never.
Wanasema Serikali ya mtu kichwa chake. Kama hujagundua ni kuwa wengi wenye kuandika developmental things hawana maoni mengi wala hits za kutisha. Angali na chunguza. PHabari ya kupinga vita mauaji ya albino inapata maoni machache kuliko ya mtu anayetoka kichakani kukojoa. Lakini ndivyo ilivyo na kama kila mtu atakaa bila kuweka jitihada za kubadili hilo, hakuna atakayebadilika. Ni lazima kujitoa kuelimisha. Jua kwamba wengi wanasoma hata kama hawatoi maoni. Kwa hiyo wewe fanya lililo muhimu na sahihi na wengine wataanza kubadilika kidogpkidogo na baada ya muda tutabadili fikra toka kwenye upuuzi kuelekea kwenye ujenzi.
s Kila la kheri na sante kwa uwepo na nia yako ya kuwepo.
sSubi. Asante saaaana
Mzee wa Changamoto nakubaliana kabisana maoni yako hapo juu. Nimejunza mengi kwenye hizi blogs. Japo sibahatika kutembelea zote lakini nimefurahishwa na nukta77 na mwanakijiji kwani wemegusa kwa namna moja au nyingine.
s
Si viruzi kufanya kazi kwa ushabiki au kutafuta sifa bali tunatakiwa kuijenga Tanzania. Tanzania itajengwa na wachache wenye ari na nia ya kuthubutu. Naimani ipo siku mambo yatabadilika.
s
Hivi sasa changamoto tuliyonayo ni namna ya kuwaelimisha watanzania waliopo vijinini, ni kwa vipi tutaweza kuwapata hata wafadhili wa kuchapisha gazeti japo moja tu ambayo itakuwa ni ya bure na yenye kubeba mambo mengi yahusuyo maendeleo na vita dhidi ya rushwa na ufisadi.