wavuti.com Updates

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, February 01, 2009

TweetThis! Jinsi ya kuweka 'read more' au 'endelea' kwenye blogu. Method 1

Rafiki yangu kaniandikia kuniuliza, inawezekana vipi kuweka 'read more' ama 'endelea' ikiwa umeandika posti ndeeeefu na ungependa kumpa msomaji wako muhtasari badala ya kumchosha na posti ndeeefu bila sababu? Tuseme unataka kumpa msomaji wako nafasi ya kuchabo kisha yeye aamue kama aendelee kusoma posti nzima ama la.

Bloga anayetumia Wordpress wanaweza kutumia 'read more' au 'full story' nk kwa kuwa tayari ipo kwenye Wordpress templates nyingi.

Bloga anayetumia Blogspot hana uchaguzi wa 'read more' kwa sababbu bado haijawekwa kama defaut feature hivyo inabidi kuiweka mwenyewe.

Leo nitaeleza njia moja ya kufanikisha hilo, nitaandaa njia ya pili na nikimaliza nitaibandika hapa halafu wewe utachagua njia ambayo unaona ni rahisi kutumia.

Kuongeza 'read more', 'endelea', 'soma zaidi' nk katika posti fanya hivi:

Login kwenye blogger account ambayo itakupeleka kwenye 'Dashboard'.
Kwenye blogu yako, bofya 'Layout'
Bofya 'Edit HTML' tab inayopatikana kwenye 'Template' tab
Bofya 'Expand Widget Template'
Sasa tafuta neno hili
<data:post.body/>
kwenye template yako. Njia rahisi ya kuipata ni kwa kutumia kibodi yako 'Ctrl+F', ukishaipata, KABLA ya sentensi hiyo weka code ya kwanza ambayo ni hii:
<b:if cond='data:blog.pageType == "item"'>

<data:post.body/>

<b:else/>

Sasa BAADA ya
<data:post.body/>
weka code ya pili ambayo ni hii:
<b:if cond='data:blog.pageType != "item"'>
Read more / Endelea>>>
</b:if>
</b:if
Baada ya kuweka code zote mbili, html yako itaonekana hivi:

Baada ya kuweka code kwenye template yako bofya 'Save Template'
Sasa nenda kwenye 'Blogger Settings' kisha 'Formatting' kisha kwenye 'Post Template' weka code hii:

Malizia kwa kubofya 'Save Settings'.

Code uliyoiweka ndiyo itakayotumika wakati unaandika posti yako. Hivyo kuwanzia sasa, wakati unataka kuandika posti, kuna maneno tayari yataonekana, hayo ndiyo yale uliyoyaweka kabla ya kubofya 'save settings' yanayokuruhusu kutumia 'Read More' kwenye posti husika ambapo inatakiwa kuandika posti kwa kutumia ' Edit Html ' mode badala ya 'Compose' ambayo ni default kwa kawaida kila wakati unapoandika posti. Maneno yote unayotaka yasomeke kwa muhtasari yaandike kabla ya  na maneno yote mereeefu unayotaka yaendelee kusomeka, yaandike baada ya  kama inavyoonekana kwenye picha hapa:

Ikiwa hutaki kuyatumia, basi ukiwa kwenye 'Edit Html' yaondoe kisha andika posti yako na itasomeka nzima bila 'read more' option.

Hadi kufikia hapa, umejifunza mawili matatu katika kujifunza kucheza na sehemu fulani ya html ya template yako. Sasa jaribu kuandika posti yako uone itakavyokuwa.
Maneno yaliyoandikwa 'READ MORE / ENDELEA' unaweza kuyabadili kadiri utakavyopenda.

Tuonane tena wakati ujao.

Rejea zilizotumika wakati wa kuandaa posti hii:
Blogger Help
Blogging to fame
NoFancyName
BlogspotTutorial

2 feedback :

ERNEST B. MAKULILO said... Sun Feb 01, 05:46:00 PM MST

Da Subbi,
Tunashukuru kwa hii njia. Binafsi sikupenda kukuchosha kukusumbua kwa mambo mengi..ujue msaada ulionipa wa kurekebisha blog yangu kuwa hivi ilivyo sio jambo la kitoto my dear.Sasa hii naanza kuitumia soon. Nasubiria na hiyo njia nyingine nione ipi ni rahisi kwangu kuitumia.

Mungu akubaridi Da Subbi,
MAKULILO Jr,

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads