wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, January 07, 2009

TweetThis! Kwa nini ubakaji?

...marehemu Maria Nyandwi, mwenye umri wa miaka 60, Mhutu, alibakwa na watu wasiofahamika hadi kufa katika kijiji cha Buramata, ndani ya makazi ya wakimbizi ya Mishamo, wilayani Mpanda. Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, alisema mwili wa marehemu uligundulika ukiwa karibu na nyumba yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, wabakaji hao walimvizia ajuza huyo akiwa anatoka matembezini na kumbaka, kitendo kilichosababisha kifo chake papo hapo.

Uchunguzi wa daktari ulielezea kuwa wabakaji hao waliacha kondomu sehemu za siri za ajuza huyo.
- Iliripotiwa na UhuruInfo

Inatia uchungu na hasira sana kuwaza juu ya hili suala la ngono ya lazima na kubakwa. Kwa mtu mwenye imani, suala hili ni mojawapo ya mambo yanayoleta laana mbaya na kubwa sana. Hii huchangia sana kutokuisha kwa vitendo vya kiovu kutokana na chuki, hasira na visasi inayojitokeza kati ya jamii ya aliyeondolewa haki yake ya kuishi na wale wanaotuhumiwa kuhusika na kitendo cha ubakaji.

Adhabu ya kufungwa miaka thelathini imekuwa kama wimbo tu. Kila kukicha vyombo vya habari vinaripoti kuhusu kadhia ya matukio ya ubakaji. Mbakaji anapoamua kumwadhibu binadamu mwingine kimaumbile kwa amri na sheria zake ama za kundi analolijua yeye, hafai kabisa akaachwa huru huku akiendelea kuamini kurahisi rahisi tu kuwa kitendo alichokifanya ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu ama kurukwa na akili vile. Bahati mbaya ya kumwona mtu, umvue nguo, uvue na nguo zako, kisha umlaze chini, umnyamazishe kwa njia unazozojua wewe, ujitahidi kuziba kilio chake, ubake... kweli hiyo iwe ni bahati mbaya? Jamani, tumwogope Mola.

Ikiwa kweli mtuhumiwa atakiri ama itathibitishwa bila tashwishi yoyote kuwa amebaka, kisingizio ama sababu yoyote ile ya kupunguza adhabu kali kwa mharibifu wa namna hii inatakiwa isiwepo ili iwe funzo kwa watu wengine wanaodhani kuwa wanaweza kukwepa mkono wa sheria kwa upenyo wa 'bahati mbaya' sikukusudia.

Binadamu umepewa utashi na hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya kuamua lile lililo jema ama baya.Visingizio vya kutamanishwa, mavazi, vichocheo vya mwili na kuzidiwa ashki ama tamaa inayotokana na kumtizama mtu mwenye maungo pamoja na/ama aina fulani ya mavazi, kwa kweli havina uzito kama tendo la kubaka. Anayepita na viguo vyake vifupi tena vya kubana, tafadhali mwone kama shetwani mshawishi ambaye lengo lake damima ni kuharibu hasa kwa kusambaza magojwa ya ngono kama vile VVU (kwa kiasi kikubw), Kisonono, Kaswende na Pangusa. Wazo hili litakusababisha ufikiri upya na hivyo itakuepusha na mengi mabaya. Kujisingizia na kujitetea kuwa ni kizuri, kitamu, kinavutia na kutamamisha, hata ikibidi kukitolea fedha ukipate, ni sawa na kununua majuto na matokeo yake yakawa ni kuzaa mauti.

Wakati ule nikiwa mtoto mdogo ninakwenda skuli, vilikuwepo visa vya hapa na pale vya baadhi ya watu kupatwa na mifadhaiko katika vituo vya daladala na kwenye misongamano wa watu ama ndani ya vyombo vya usafiri. Lakini punde, sheria kali na zilizotiwa mkazo ziliwekawa na kufuatwa na hii ilipungua kama si kwisha kabisa. Ikawa nadra sana kusikia malalamiko ya udhalilishaji huu mbaya.

Hili la ubakaji kwa namna nyingine ni sawa na kupokezana mapepo kwa kujiendekeza kupenda ngono. Sikuwahi kusikia mtu asiye na akili (zaidi ya kichaa mmoja wa Moshi maarufu kwa jina la Kiroboto) kuwa amebaka, je itawashinda watu wenye akili timamu? Tafadhali mwone huyo kama Mzazi wako, Dada yako ama Mwanao na hivyo umhurumie (ingawaje wapo wanaowabaka wazazi, dada na watoto wao - huu nao ni ugonjwa wa akili na kujawa mapepo wachafu kabisa).

Nadhani suala zima linaangukia katika mchanganyikko wa kutokujali mafundisho ya imani/dini na sheria za nchi, kupungua heshima na adabu, kuendekeza ngono, starehe na mitizamo ya hovyo.

2 feedback :

MARKUS MPANGALA said... Thu Jan 08, 01:29:00 AM MST  

Duuh! hasira sana,huzuni pia sijui kama nitafanikiwa kuandika kwa ufasaha. Kuna jambo huwa najiuliza kichaa halisi ni nani? Ikiwa vichaa hawabaki halafu watu tunaojiita tuna akili timamu tunabaka, inakuwaje hapo? sasa tafsiri ya kichaa halafu tunatenda matendo yanatuondoa katika akili timamu, duuh! au ndiyo tuamini imani za wanasayansi kuwa binadamu tunabaadhi ya ubongo wa mjusi. huu ni ubongo unaoratibu matendo yanayoshangaza utimilifu wa akili ya binadamu. matendo yanayoduwaza kisha kujiuliza maswali inakuwaje huyu au yule kutenda maovu haya ama yale? lakini ikiwa katenda mazuri ubongo wake upo sawa.hebu tujisomee kuhusu ubongo wa mjusi jamani.
Zambia ukibaka unakwenda jela miaka miwili, lakini nakwambia utajuta kuzaliwa katika ulimwengu huu, ni jela haswaaaaaaaaaaaaa siyo miaka thelathini Bongo kisha upate msamaha wa Rais ebooo!
Italia ukibaka au kubakwa wanaangalia mazingira ya mbakaji na mbakwaji! wanaangalia mavazi ya mbakwaji na mbakaji, ikiwa mavazi ya mbakwaji yanaashiria kumfanya mbakaji akubake basi ujue umekwisha hakuna kesi hapo. ushauri wao na bunge likaazimia kuwa lazima kuvaa suluwali za jeans ambazo haziwezi kuvuliwa au kuchanwa na mbakaji na kufanikisha azma yake. Duh! dada Subi. mada kali sana hii.
Hili pepo la ngono unalolisema jamani mmmm, unajua ni kama kichaa fulani hivi, hata sijui inakuwaje na wanaobaka wakati mwingine ni watu wa maana kabisa. wengine hawasemi kama wamebakwa sababu ya kuogopa fedheha! waseme wala wasiogope. Wafanyakzi wa ndani wangapi wanabakwa iwe wa kike au kiume.
Hili pepo sijui linaitwaje maana nashangaa sana naomba lisije likanivamia nami naliogopa sana mweeeee! VVU kila mtu afe na chake haswaaaaa

Subi Nukta said... Thu Jan 08, 10:44:00 AM MST  

Markus,
Asante kwa mchango wako wote na hasa kwa habari ya sheria za nchi nyingine. Umenipa sababu ya kutafuta na kusoma zaidi kuhusu sheria za ubakaji katika nchi nyingine.
Asante sana!

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads