wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, December 29, 2008

TweetThis! Umuhimu wa elimu ya afya ya msingi inayowalenga watoto

Zaidi ya akina mama mia moja wenye watoto wa chini ya umri wa miaka mitano wenye utapiamlo katika vijiji vya Sangabuye na Kabusungu katika manispaa ya Mwanza wamepatiwa mafunzo ya siku nne chini ya mpango wa shirika la Plan Tanzania juu ya lishe bora.

Mafunzo haya yamepangwa kutokana na majibu ya utafiti uliofanyika katika mkoa huo ambapo ulibaini kuwa asilimia 8.7 ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano walikuwa na utapiamlo na hii ikachangia kuongezeka kwa vifo vya watoto walio katika umri huu.
``This was a serious concern and this is why Plan Tanzania has decided to conduct such training so as to tackle poor diet among the under-fives in the region,`` said Sophia Mhonzwa, a micro-nutrients point person with Plan Mwanza.
Walengwa: Mafunzo hayo ambayo yalifanywa chini ya wahudumu kutoka TAHEA - Tanzania Home Economy Association, yaliwalenga walezi, wazazi, watumishi mbalimbali wa jamii na viongozi wa serikali za mitaa na vijiji vilivyokuwa na idadi kubwa ya tatizo hilo.

Lengo kuu: Kuhamasisha ufahamu wa matumizi ya vyakula vinavyopatikana katika jamii husika na matumizi yake katika kuboresha afya ya watoto na jamii nzima. Kutokana utafiti, iligundulika kuwa watoto wengi wamekuwa wakikosa afya madhubuti kutokana na ulaji usiofaa ambapo watoto wamekuwa wakikosa vyakula kama vile matunda, mboga za majani na uji wenye vitrutubisho vya afya mwilini. Kwa mfano, familia yenye wastani wa watoto wanne hadi watano na mifugo imekuwa ikiuza maziwa yanayotokana na ng'ombe wanaowafuga bila kutenga kiasi kadhaa ajili ya kwa matumizi ya nyumbani.
``People here regard these types of food to be inferior and that they`re for the poorest. One of the mothers attending the training told me that she never includes vegetables in the family food and that none of her children would ever eat such food,`` Mhonzwa said.
Kwa hivi, watafunzwa kwa vitendo namna ya kuandaa lishe bora kwa watoto wao ambayo itakuwa na virutubisho muhimu kama vile wanga, vitamini na protini.
  • Ni imani yangu kuwa elimu ya msingi kabisa juu ya afya ya mtoto itasidia katika kupambana na tatizo la utapiamlo na hatimaye kukuza vijana watakao kuwa na afya njema na hivyo kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria shule kupata elimu itakayowafaa wao na taifa letu siku za usoni.
  • Ni imani yangu vile vile kuwa mafanikio ya elimu hii katika eneo hili dogo yatachagiza kuendelezwa kwa elimu hii katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania ili hatimaye tuwe na taifa lenye afya na hivyo nguvu kazi ya kutosha.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads