Makatibu Wakuu na Manaibu wapya
Kufuatia baadhi ya matatibu na manaibu kustaafu, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete imemlazimu kubadilisha safu zao na kuteua watendaji wapya, uteuzi unaoanza mara moja.
Naibu Katibu Mkuu wa Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah anakuwa Katibu Mkuu. (Anachukua nafasi ya Gray Mgonja ambaye yuko kwenye likizo ya kustaafu).
Makatibu Wakuu wapya
Makatibu wakuu waliohamishwa:
Manaibu Katibu Wakuu.
Dk. Phillip Mpango, anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Fedha na Uchumi (alikuwa Msaidizi wa Rais Uchumi).
Selestine Gesimba, anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Elimu na Mafunzo ya Ufundi (alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia).
Fanuel Mbonde, anakwenda kushika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu, TaMiSeMi Ofisi ya Waziri Mkuu.
Unaweza kusoma wasifu zaidi ya wakuu hawa kupitia tovuti za Bunge ama AfdevInfo.
Naibu Katibu Mkuu wa Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah anakuwa Katibu Mkuu. (Anachukua nafasi ya Gray Mgonja ambaye yuko kwenye likizo ya kustaafu).
Makatibu Wakuu wapya
- Dk. Florens Turuka, anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo (Naibu Katibu Mkuu Viwanda, Biashara na Masoko).
- Andrew Nyumayo anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu).
- Joyce Mapunjo anakuwa Katibu Mkuu Viwanda, Biashara na Masoko (Naibu Katibu Mkuu Miundombinu).
Makatibu wakuu waliohamishwa:
- Paniel Lyimo, Ofisi ya Waziri Mkuu (anatoka Kilimo, Chakula na Ushirika).
- Mohamed Muya, anakwenda Kilimo, Chakula na Ushirika (anatoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
- Wilson Mukama, anakwenda Maji na Umwagiliaji (anatoka Afya na Ustawi wa Jamii).
- Dk. Stergomena Tax Bamwenda, anakwenda Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anatoka Viwanda, Biashara na Masoko).
- Patrick Rutabanzibwa, anakwenda Mambo ya Ndani (anatoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji).
- Kijakazi Mtengwa, anakwenda Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana; (alikuwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo).
- Seti Kamuhanda, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (alikuwa Msaidizi wa Raisi wa hotuba).
- Dk. Ladislaus Komba, anakwenda Maliasili na Utalii (anatokaWizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana).
- Blandina Nyoni, anakwenda Afya na Ustawi wa Jamii (anatoka Maliasili na Utalii).

0 feedback :