Kero: Miundombinu
Swali:
Je, tupambane vipina tatizo la mazingira, mafuriko na magonjwa ya mlipuko?
Maoni:
Dr. Matechi E, anasema:
Ungependa suluhisho la kisomi au kisiasa?
Nadhani kisomi hatuna mipango miji. Huwa nawaza itagharimu kiasi gani kuteketeza slams na kujenga residential apartments. Hilo ndio suluhisho la kudumu.
Kisiasa, tutafute mtu, hata mtendaji wa kata, tumuwajibishe!
Nadhani kisomi hatuna mipango miji. Huwa nawaza itagharimu kiasi gani kuteketeza slams na kujenga residential apartments. Hilo ndio suluhisho la kudumu.
Kisiasa, tutafute mtu, hata mtendaji wa kata, tumuwajibishe!
______________________
Dr. Mahamba V, anasema:Nakubaliana na wewe Matechi.
Maeneo kama hayo yapo mengi sana Dar, na yanaonekana sana mvua zikinyesha. Kuna eneo sugu pale Magomeni, na bado watu hawafanyi lolote…wanasubiri Serikali.
Mipango miji tukubali kuwa wameshindwa kazi maana hata hizo barabara zinazojengwa ziwe za kiwango cha lami au kifusi tu hazina mitaro (storm water drainage) ya kuweza kupunguza matatizo kama hayo.
Mimi ninafikiri pia kuna umuhimu wa kuelimisha jamii kuhusiana na matatizo kama hayo, wasiisubiri Serikali, ninaamini wanaweza kuyatatua wenyewe pia. Rejea Azimio la Arusha!
Mtu ni afya….
______________________
Dr. Mashuda F, anasema:
Wajiorganise ki mtaa na kutengeneza mifereji katika eneo lao.
______________________
Dr. Mvungi K, anasema:
Kujiorganise ni sawa lakini hawa watu hulipa 20% kama VAT katika kila bidhaa wanayonunua kuanzia sindano hadio kondom hadi soda, sasa serikali haitengi fungu la miundombinu ?
Hela tunalipa kodi zikiwekwa na watu wanachota wanaenda kujitajirisha.
Japo si vizuri kuangalia nani mbaya lakini hii vicious cycle, Serikali inapokea hela haitendi haki, anayeumia ni hao hao wananchi.
Hela tunalipa kodi zikiwekwa na watu wanachota wanaenda kujitajirisha.
Japo si vizuri kuangalia nani mbaya lakini hii vicious cycle, Serikali inapokea hela haitendi haki, anayeumia ni hao hao wananchi.
______________________
Evans M (BPh) anasema:
Ukipita uswahilini unaweza kushangaa pale utakapowaona watoto wanakula vitumbua huku wakicheza karibu sana na maji machafu… na ukipita kwenye daraja letu maarufu kuna harufu mbaya yaani siku nyingine unashindwa kukimbia ufukweni, kisa bomba la maji machafu…
Kuna waheshimiwa wamejaribu kujenga majumba bila kuweka mitaro ya kuhimili maji. Ukitaka kujua shughuli yake pita mvua ikinyesha! Hapatoshi!
Kweli inabidi tubadilike, tuendelee kupiga kelele, mambo yatapendeza. Tatizo ni kwamba mtu akianzisha anaonekana adui na mbegu ya upinzani au katumwa na Upinzani. Huu mtandao wa chini chini utaendelea kututafuna na ndo siri ya kudumaza maendeleo ya nchi yetu. Hadi utakapokufa kabisaaa ndo tutatoka.
Kweli inabidi tubadilike, tuendelee kupiga kelele, mambo yatapendeza. Tatizo ni kwamba mtu akianzisha anaonekana adui na mbegu ya upinzani au katumwa na Upinzani. Huu mtandao wa chini chini utaendelea kututafuna na ndo siri ya kudumaza maendeleo ya nchi yetu. Hadi utakapokufa kabisaaa ndo tutatoka.
______________________
Dr. M Tonny, anasema:
Ninachochangia ni kwa wale ambao wana-plan kujenga ni vizuri kununua sehemu zilizokwishapimwa au zinazopimwa kuondoa huu usumbufu. Kununua plot sababu ya unafuu fulani matatizo yake ndio haya. Haya matatizo yanakuja hata Kimara, Mbezi, Kibamba, Mbagala…. ni balaa.
Mipango miji sijui kama wapo, inasikitisha, mbaya zaidi wabongo tunatumia muda wa mvua kuzibua vyoo!
Mipango miji sijui kama wapo, inasikitisha, mbaya zaidi wabongo tunatumia muda wa mvua kuzibua vyoo!
______________________
Dr. Ngemrera D, anasema:
Hiyo mifereji inapotoka na inapoelekea…
Mmwingiliano wa hiyo mitaro ya maji machafu….
Kwa kifupi naona Dar es salaam yote imezungukwa na vinyesi kila sehemu…
Je, malaria, miharo, kipindupindu nk vyaweza tokomezwa kwa mtindo huu?
______________________
Dr. Mrema E, anasema:
Hili swala liko mikononi mwa mipango miji.
Kwanza tuangalie mazingira ya hii nyumba kama yalivyo hapo kwenye picha na pia eneo lililopo hiyo nyumba ni mwananyamala..
Haya ni matokeo ya ufisadi kuanzia mtu binafsi, ngazi za chini za Serekali za mitaa mpaka juu.
1. Tuanze na mazingira ya nyumba ya picha katika picha
* Nyumba iko USWAZI ambako huwa hakuna mpangilio wa nyumba pamoja na wenyeji wenyewe.Pia huwa hakuna miundo mbinu mizuri na sehemu hizi kuna vyanzo vingi vya uchafu kwa sababu ya mlundikano wa watu nyumba moja ni mkubwa na hakuna njia sahihi ya kutupa taka zaidi ya kutupa popote pale.Kwanza tuangalie mazingira ya hii nyumba kama yalivyo hapo kwenye picha na pia eneo lililopo hiyo nyumba ni mwananyamala..
Haya ni matokeo ya ufisadi kuanzia mtu binafsi, ngazi za chini za Serekali za mitaa mpaka juu.
1. Tuanze na mazingira ya nyumba ya picha katika picha
* Kuna kuta 2 zimejengwa kati ya hizi nyumba mbili zikiwa na lengo si la ulinzi bali maji yanayopita yasiharibu nyumba au yasiingie ndani.kwa hiyo hizi nyumba zimejengwa kwenye mkondo wa maji ndo maana hizi tahadhari zimechukuliwa na wajenzi wenyewe.
* katikati ya hizi kuta 2 ni mtaro wa maji na hii sehemu nyingine ni barabara ambayo imejaa maji kwa sababu maji yamekosa mwelekeo baada hilo daraja[karavati] limeziba.Shuhudia makaratasi,matairi na uchafu mwingine ulivyozagaa.
* Mbaya zaidi kuna bomba la maji limepita juu ya karavati na kufunikwa na maji machafu.Hilolinapelekea jamii maji safi ya kunywa.
* Nafasi ya kati ya hizi nyumba mbili ni ndogo sana
* tuanahitaji na picha ya hili eneo kutoka juu kwa ufafanuzi zaidi na pia picha za mlango mkuu tujue kama ina namba maana itakuwa inatambulika kwa ajili ya kodi ya majengo kwa manispaa ambayo ni 10000 kwa mwaka.
2. Eneo lililopo nyumba hii ni Mwanayamala
* Ni nani asiyeijua Mwanayamala? Sehemu nyingine zimepimwa zikaachwa zilizo karibu na vijito vya maji machafu kwa ajili ya kuruhusu free drainage systemS sehemu hizi zilivamiwa na watu wakajipangi na kusongamanisha nyumba mpaka hakuna njia ya kupita kwa miguueven kupishana watu wawili inabidi iwe kimgongomgongo.
* uchafu mwingi unaozalishwa katika hizi nyumba unatupwa mtoni na kwenye vijito hivi na huko kwenye njiana mitaro halali.kwa njia hiyo sikilizia mvua ikinyesha.
* Drainage system ya maeneo mengi ya Dar kuanzia Magomeni,Muh2,Ilala,Tabata,Ubungo mpaka Kimara huwa ina destination yake maeneo ya Mwananyamala.wengi mtakuwa mashaidi wangu.angalieni yafuatayo hapa chini,
o Bonde la msimbazi linapeleka maji machafu kupitia eneo la Jangwani pale ambapo saa moja usiku unakabwa bila ridhaa yako.Hili linapokea kutoka Tabata,Sukita na maeneo ya Kigogo na Ilala.Hapo jangwani yanapitia uchafu wa Breweries to Muhimbili to salender bridge.Pia yanaungana na yatokayo huko huko kupitia KAJIMA mpaka nyuma ya Mkwajuni na uchafu unaozalishwa hapo.
o Kumbuka Riverside ni kijito kinachosafisha Kibangu na maeneo yote.Ulishaona Dampo la pale jirani na daraja?Kweli maji yatapita kwa UHURU? Hiki kinapita kando kabisa ya Bar ya LANDMARK ambayo imejengwa ndani ya kijito na kinapitia External Mabibo to SUKITA then Jangwani.
o Kijito kinachopita Ubungo TBS is from Kimara matangini,Msewe via Sinza Kamanyola,Uzuri darajani to Mwananyamala.Hiki kinapitia kwa Mtogore na kukusanya mambo makubwa ya huku uzuri kusiko na Road.
o Eneo la daraja la Kawawa Road kati ya Mkwajuni na Magomeni kuna kiunganishi pale cha bonde la Jangwani hadi Mwananyamala ambapo inakutana na kijito kitajwa hapo juu na kina uchafu wote .Hapo vinapokutana ni maeneo ya katikati ya Kwa Tumbo na Popo Bawa hili lijito linakutana na kile cha Kijotonyama kupitia kwa Mtogore.Muunganiko huu hujikusanaya na kuelekea baharini kupitia pale sayansi [OIL COM] petrol station via Msasani karibu na Kwa Nyerere.
o Maeneo ya Kinondoni A na B yapo juu na mengi yana system kidogo ya kudrain ingawaje sio sustainable.Uchafu wake hutafuta njia ambazo mara nyingi ni barabara ili yaelekee katika vijito tajwa hapo juu au direct to Jangwani.
Chanzo cha haya mafuriko ni UJENZI HOLELA BILA YA KUFUTA KANUNI NA MIPANGO MIJI. Asilimia kubwa hakuna mipango miji hapa Dar hata maeneo mengi ya Tanzania. Mafuriko yalipo hapo pichani si tu kwamba yamesababishwa na wanamwananyamala balia ni watu wa mbali. Matatizo yote yapo pale Msasani kwa Nyerere.Ujenzi uliofanyika pale ni Ufisadi mtupu na haujazingati utaratibu.
Ili maji yaweze kutoka vizuri yale maeneo yalikuwa ni nia ay kupitia maji machafu kwenda baharini.Mfano kuanzia eneo la TANESCO. May Fair Plaza na mahekalu mengi yalijengwa maeneo yale ambapo kwa walioona hapo zamani kabla ya huo ujenzi kulikuwa na TINDIGA ambapo maji yalikuwa yanapia.Pia eneo la Msasani karibu na baharini kuna Waarabu walijenga juu ya mkondo wa maji.kwa hiyo inabidi maji yarudi nyuma.matatizo ya uharibifu huu wa miundo mbinu yalianza tangu 1985.
Pia wannchi wengi wa maeneo ya uswazi wanajenga ovyo ovyo tu na kuna mlundikano wa watu na uchafu ni mwingi ambao unaziba miundo mbinu ya maji kupitia.
Nini kifanyike?
Kwa kuwa tumeona kuwa njia kuu ya maji kupita nia via Jangwani to Mwananyamala to Msasanita baharini,kinachotakiwa ni kufungua hii njia kuanzia kule maji yanakotakiwa yaishie.Hii ni kwa kutekeleza yafuatao,
1. Watu kuwa wazalendo yaani viongozi na wanachi kwa kutofumbia macho haya mambo maana athari zake ni za muda mrefu kama tunavyoona.Mfano kuwepo na miundombinu na mipango miji ya muda mrefu na mfupi ya kisayansi na iliyoenda shule.Tuache siasa.wananchi wajenge kwa kufuata utaratibu.kama tuna mpaka viongozi wa mitaa ambao wanaona ujenzi holela wanakaa kimya watakuwa wamekula kitu kidogo.
2. Njia ya maji kuazia Jangwani kupitia mwanayamala to msasani isafishwe na watakaobainika kujenga kwenye mkondo wa maji inabidi wawajibike ikiwa ni pamoja na waliowaweka hapo.hapa kuna kubomolewa kwa utaratibu wa fidia au kutofidiwa.kama rushwa ilitumika hakuna kuangalia mtu usoni. Nadhani kama kukiwa na utaratibu maalumu bila kukurupuka inaweza kufanikiwa. Isiwe kama ile ya Tabata dampo ambayo ilikuwa kumwondoa black na kumweka white.Hata kama May fair itabomolewa ni sawa tu ikiwa wamejenga juu ya mkondo wa maji.hatauangalii uzuri wa jengo.
3. Wananchi waelimishwe juu ya usafi wa mazingira hata ikibidi kwa viboko.nakumbuka kuna wakati jiji lilikuwa chafu sana na wajina wangu alitumia mbinu ya siku 7 kulisafisha.Alisema baada ya muda huo kama uchafu ukikutwa mbele ya nyumba yako na hakuna pipa la taka unaadhibiwa.Kwa kweli watu waliitikia mwito ingawaje haukuwa endelevu.
Nadhani wengine wachangie namna ya kufungua njia ya maji.
Mzazi nimeboreka sana maana hiyo picha inanionyesha tulivyo mbali kupigana na adui maradhi. Kweli Malaria, Cholera etc zitaisha kwa mtindo huu? Kweli this is Bongo Dar.
0 feedback :