wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, October 04, 2009

TweetThis! Moto waua tena bwenini - kituo ch Bethelem, Kilombero, Morogoro

Nashauri tutumie wataalamu wetu kikamilifu kupambana na majanga yanayozuilika; majanga yanayohitaji tu kutumia maarifa tunayoyapata masomoni na kwenye historia ya visa hivi inayojirudiarudia.
Moto umeua watoto watatu katika kituo kinacholea watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo kiitwacho Bethelem wilayani Kilombero, Morogoro kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge. Watoto hao wamekufa kwa kuunguzwa bwenini wakati wamelala usiku wa kuamkia leo. Bweni katika kituo hicho limeteketea, watoto sita wamejeruhiwa, wamelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis ya Ifakara, mkoani humo. Chanzo cha moto huo ulioanza saa 9 alfajiri hakijafahamika. Bweni lililoteketea lilikuwa na uwezo kuhudumia watoto 15, wakati wa ajali hiyo, 14 walikuwa wamelala bwenini humo, mtoto mmoja hakuwemo bwenini kwa kuwa anaumwa na alilazwa kabla ya tukio. Kituo hicho kina mabweni sita yenye uwezo wa kuhudumia watoto 93 wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo

Ndugu wa watoto hao wamewatambua marehemu kuwa ni Gerald Thomas (21) mkazi wa Dar es Salaam, Yohana George (11) mkazi wa Maswa, Shinyanga, na Victor Chilimba (15) mkazi wa Ifakara. Maiti za watoto hao zimehifadhiwa katika hospitali hiyo ili kusubiri taratibu za mazishi na maziko.

Mkuu wa Wilaya ya Ifakara, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa moto huo umemuunguza sana mlezi wa watoto hao, Paskalina Barua (22), mkazi wa Ifakara, amelazwa katika hospitali hiyo ya Mtakatifu Francis, Morogoro. Aliwataja watoto sita waliolazwa katika hospitali hiyo ni Deo Malongo, Said Salehe, Lusajo Loli, George Gaiza. Wengine wametambuliwa kwa jina moja la Amos pamoja na Mendrahad, wanaendelea kupatwa matibabu. Alisema kujengwa maeneo tofauti kwa mabweni hayo kumesaidia kuyanusuru mengine yasiungue.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, ameunda tume itakayochunguza chanzo cha moto huo na kutoa mapendelezo kuhusu hatua za kuchukuliwa kwa tahadhari za majanga ya moto ili yasitokee tena. Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro,Thobias Andengenye, ataongoza tume hiyo, inatakiwa kukamilisha kazi hiyo Ijumaa ijayo.

Habari hii imeripotiwa toka katika gazeti tando la Habarileo.co.tz/kitaifa

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads