wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, October 08, 2009

TweetThis! Mdau Eva C anasema 'tule mboga majani tu jamani'

Sisi waTanzania tunafahamu au tumewahi kusikia kuwepo kwa kitoweo 'samaki nchanga', wengine husema 'panya buku' japo watu wengi wanaoishi maeneo ya mjini, neno hili litakuwa la kufikirika tu na pengine mzaha na masikhara. Bila shaka yoyote, nikweli kuwa panya ni kitoweo kwa baadhi ya makabila ya Tanzania hasa yale ya Kusini, mikoa ya Nyanda za juu Kusinina hasa kaskazini kwenye jamii ya Wahadzabe. Vile vile mnyama huyu ni kitoweo katika maeneo ya baadhi ya nchi nyingine za dunia katika mabara kama vile Asia na Amerika ya Kusini.
Baadhi ya viumbe wanaoliwa ambao aghalabu ni nadra kukubalika katika jamii nzima ni pamoja na, Panya, Panya buku, Nyoka, Chura, Ng'e, Mende (aina fulani), Senene, Barale, Kumbikumbi nk.

Hizi ni picha alizonitumia mdau Eva na video inayoonekana hapo baada ya picha nimeipata YouTube.


















2 feedback :

Yasinta Ngonyani said... Thu Oct 08, 04:31:00 AM MST  

Nilifanya makosa nilianza kuangalia hapa baada ya kula ugali na Tilapia ambayo niliipka sana. Kilichotokea unaweza kumalizia yaani nime........

Subi Nukta said... Thu Oct 08, 04:36:00 AM MST  

ha ha ha, Yasinta, pole umetapi..?
Ni kwa kuwa hujakulia kitoweo hicho, mimi nakumbuka siku moja nimeambiwa nionje mlenda (alitengeneza Msukuma mmoja kwa kuchemsha bamia, akaziponda zikawa uji unaoteleza, akawekamo na majani ya maboga yaliyochemshwa na kupondwa ikawa rojo wakaongezamo karanga, chumvi, kitunguu na nyanya rojo...), nami nilitap...! wao wakala kwa raha zao.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads