wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, October 02, 2009

TweetThis! Arrogance + Ignorance = ? Mahiza agoma kuwaomba radhi Walimu

You know exactly that YOU ARE DAMN WRONG but you won't admit it ofcourse, why would you? Tell you what, it's a civil thing to do especially for a high figure like you. Guess what, if civility is not a vocabulary to you it could be echoing a form of feeling low in your mind, and that probably doesn't suit you, it belongs to others. I heard you that other day when you opened your mouth, I have it in records (well, ofcourse not that it matters anything to you, but just so you know, I have it in records... just thinking... and wondering... that's all).
But, aren't you the smartest thing ever?
Just listen to yourself...

How does it feel?
Great huh?
What a.......!
One wonders what's the motive and what's behind all that harsh tone!
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, amekataa kuwaomba radhi walimu, na amemtaka mwalimu yeyote anayeoona kwamba ualimu haufai au haulipi aache kazi. Mahiza amesema, hafuti kauli hiyo na haombi radhi kwa kuwa alichokisema ni sahihi. “Kuliko mtu kukaa asiwajibike wala kufuata kanuni za kazi na kubangaiza ni bora aondoke ”, amesema Mahiza leo. “Nimesema tena narudia na uandike hivyo hivyo, mimi Mahiza siombi radhi anayeona ualimu haufai au haulipi aanze (aondoke),” amesema.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba, leo amemtaka Mahiza afute kauli aliyoitoa Agosti 22, mwaka huu alipozungumza na wanachuo katika Chuo cha Ualimu Songea. Kwa mujibu wa Mukoba, kiongozi huyo wa Serikali aliwataka walimu au wanafunzi wa ualimu wanaoona mshahara wa ualimu ni mdogo kuanzia sasa wakasomee biashara au siasa. Kwa mujibu wa Mukoba, Mahiza aliwataka wenye mtazamo huo waondoke katika taaluma hiyo kwa kuwa haiwafai. “Ni vibaya sana kama mwalimu anafahamu kuwa mshahara ni mdogo halafu anajibaniza hapo, halafu uende ukafanye fujo, wakati umefika shuleni. Kama uko mwaka wa kwanza hujachelewa, hata mwaka wa pili,” Mukoba amemnukuu Mahiza. Mukoba amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mahiza alitoa msimamo huo baada ya mwanachuo kumuuliza kama Serikali ina mpango wa kuinua viwango vya mishahara. Amemtaka Mahiza awaombe radhi walimu wote nchini kwa madai kuwa, amewadharau na amewadhalilisha. Mukoba amesema, kiongozi huyo amepuuza hadhi ya mwalimu na uhuru wa mwalimu kuhoji, na kwamba, hali hiyo ilitafsiriwa kwamba, walimu wote wanaotaka mishahara mikubwa wamekosea kuchagua taaluma hiyo.

http://habarileo.co.tz/kitaifa

3 feedback :

Masangu Matondo Nzuzullima said... Fri Oct 02, 03:11:00 PM MST  

Hii ni sawa na ile ya Profesa Sarungi wakati ule alipowaambia walimu waliokuwa wanajiandaa na mgomo kwamba wagome tu na yeye anaweza kuwachukua watu wanaotembea barabarani au sokoni waingie madarasani kufundisha. Utafikiri hawa mawaziri na maprofesa hawakufundishwa na walimu. Kama mimi ningekuwa rais mtu kama huyu namfuta kazi mara moja au nakata marupurupu yake yote na kuanza kumlipa mshahara kama mwalimu. Kama ulivyosema hii ni arrogance + ignorance. Walimu ndiyo msingi wa jamii yo yote ile na kauli kama hizi kutoka kwa hawa wanaoitwa "viongozi" zinasikitisha sana!

Subi said... Fri Oct 02, 05:54:00 PM MST  

Kauli asili ilinikera, kauli iliyofuatia baada ya kuhojiwa na TBC ikanikera zaidi, hii kauli ya leo ya HabariLeo ndiyo imenikera kabisa yaani nikatoa maanani, sidhani kama inaweza kuhadidhika ama kuandika kwa jinsi nilivyokereka na dharau kwa watu muhimu kutoka kwa mtu aliyepewa dhamana ya kuongoza Wananchi, ni radhi kuwa bila kiongozi kuliko kuwa na kiongozi anayekuvunja moyo. Loh! aibu!

Anonymous said... Fri Oct 02, 07:55:00 PM MST  

leo 20/20 ya abc walikuwa wanaonyesha mauaji ya albino Tanzania

http://abcnews.go.com/2020/comments?type=story&id=8567612

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads