wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, October 19, 2009

TweetThis! Alikufa na kuzikwa 2005... akutwa yupo hai 2009 Mwanza, Tanzania!

Habari hii imeripotiwa kwa kirefu toka Mwanza na Jovin Mihambi katika gazeti tando la majira.co.tz


...alipokuwa shule ya msingi


...wakati wa mazishi yake huko Sweya Nyegezi, Kata ya Mkolani


...akiwa katika Hospitali ya Bugando, wodi C-1 anakofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa akili

"SIKUAMINI macho yangu baada ya kugundua mwanangu ambaye nilimuuguza katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuanzia Septemba 30 mwaka 2005 na baadaye kufariki dunia Oktoba 3, mwaka 2005, tukamzika baadaye ninakutana naye akiwa hai!" Hayo ni maneno ya Bi. Stella Joseph ambaye ni mama mzazi wa binti anayedaiwa kufariki na baadaye kukutwa shambani miaka minne baadaye, Bi. Juliana Gembe (pichani).

Akizungumza na Majira kwa uchungu, Bi. Joseph amesema kuwa binti yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria na alikuwa amelazwa katika wodi namba nane katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza. Baada ya binti yake kufariki dunia, uongozi wa hospitali ya Bugando ulitoa kibali cha mazishi chenye Nambari 0861800 cha Oktoba 3, 2005 na marehemu kuzikwa siku hiyo hiyo kwa kufuata utaratibu wote wa mazishi, na baba Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino, aliendesha ibada ya kumuombea marehemu. Mama huyo anasema hazikuwepo hisia wala imani zozote za kishirikina kwa sababu yeye ni mcha Mungu na kuwa anajali sana maombi, hata kuliko dawa za hospitali au mitishamba kwa ajili ya kuponya magonjwa mwilini. Anasema kuwa wakati akimuuguza mwanawe, mgonjwa huyo alikuwa akimwambia kuwa alikuwa anaona watu kadhaa wanafika kwa wingi kitandani mwake na kutaka kumchukua, na kuwa hata wakimchukua, atarudi tu na wala hawezi kuishi nao milele.

"Mama, naona watu wananisogelea kwa wingi kitandani hapa, eti wanataka kunichukua eti wanipeleke nikalime, ila mimi wakidhubutu kunipeleka, mie ni jeuri nitarudi tu muda wowote," alisikika binti huyo akimweleza mama yake maneno ambayo yamenukuliwa na mama huyo.

Akisimulia jinsi binti huyo alivyopatikana akiwa hai, Mjumbe wa CCM, Shina Nambari 5 Kitongoji cha Buhima, Malimbe-Nyegezi, Bw. Sadik Ramadhani, amesema kuwa mnamo Oktober 15, mwaka huu majira ya saa 10.00 jioni, alishtukia umati wa watu ukifika nyumbani kwake na kumweleza kuwa kwenye ubalozi wake ametokea kiumbe wa ajabu mwenye jinsi ya kike ambaye ni wa kutatanisha. Aliongozana na umati huo wa watu hadi mahali ambapo binti huyo alikuwa amekaa, huku akiwa akionekana kuchoka, kavalia matambala akiwa hawezi kuongea ila kwa ishala wakati alipokuwa akiulizwa kama anahitaji chakula. Alimchukua binti huyo hadi nyumbani kwake huku akiandamana na watu hao na kumpikia ugali ambao alikuwa anaumeza bila kutafuna. Wakati akimchunguza zaidi, aligundua kuwa ulimi wake ulikuwa ndani na hauonekana huku akiwa na meno mawili moja likiwa juu na lingine chini. Pia mgogoni mwake kulikuwa na michirizi kama ya mtu ambaye alikuwa akichapwa fimbo. Kwa muda mrefu alikuwa amefumba macho hata mtu akijaribu kumfumbua anayafumba tena, hali ambayo anaendelea nayo hata wakati huu akiwa katika wodi C-1 katika Hospitali ya Bugando akichunguzwa akili yake.

Bw. Sadiki amesema kuwa kadri watu walivyokuwa wakimininika kwenda kumwangalia, baadhi yao walimtambua kuwa ni binti ambaye alifariki mwaka 2005 na baadaye kuzikwa. Wengine ni wale ambao walikuwa wanasoma naye katika Shule ya Msingi, Nyamalango iliyoko Nyegezi, jijini Mwanza.

Dk. Rodrick Kabangira wa Hospitali ya Rufaa Bugando katika wodi C-1 inayolaza wagonjwa wenye matatizo ya akili, amesema kuwa ugonjwa alionao binti huyo, unatokana na mtu kuishi mbali na jamii na pia kuishi sehemu moja bila ya kuongea na mtu.

Naye Bw. Adina Sefania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Afya, katika hospitali hiyo, alisema kuwa tayari idara yake ilishapokea matukio mawili ya aina hiyo.Amesema kuwa serikali, ilipotoa kibali cha kufufua kaburi hiyo, walikuta kisiki ndicho kilikuwa kimezikwa katika kaburi hiyo badala ya kukuta mifupa ya binadamu.

Mama mzazi wa binti huyo anasema alipokuchunguza alama zote alizokuwa nazo binti yake wakati wa uhai wake, alithibitisha kuwa ni mtoto wake ambaye alifariki mwaka 2005.

2 feedback :

Faith S Hilary said... Mon Oct 19, 12:33:00 PM MST  

Mmh...this makes me curious, suspicious and gives me shivers...and not in a good way...very weird, spooky and creepy.

Anonymous said... Tue Oct 20, 04:18:00 PM MST  

Wewe "Candy1,

Mambo kama haya yanatokea kila mara huko Mwanza, sio stori ya kutunga ni ukweli. Unatakiwa uamini. Mambo kama haya yalikuwepo pia kwa wazungu (uingereza) kwenye karne ya 14. Ubaya wa sisi "Blacks", hatupendi kuonyeshana na kuelimishana sayansi za aina hii.

It's Great To Be Black=Blackmannen

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads