wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, September 23, 2009

TweetThis! Upumbavu tu! "Wauguzi na Madaktari watuhumiwa kwa wizi wa dawa"

Watu wasiokuwa na adabu wala lepe la woga ndo wanaweza kufanya mambo kama haya. Kusingizia ati mishahara midogo ndo iwe sababu ya kuonea mwananchi ni sababu ya kipumbavu mno, hata asiyekwenda shule anaitumia hiyo. Badala ya kuonesha utofauti wa akili na maarifa, jitu linatumbukia kufanya anayofanya asiyekwenda shule, ndo maana hata wanasema kama wasomi wanafanya utumbo huu kama sisi, ipo haja gani ya kwenda shule na faida ya kusoma ni ipi? Maarifa-less! Wapumbavu sana tu wote mnaofanya hivi. Ni upumbavu tu, kama wangekuwa na akili wasingefanya hivi kisha wasingizie njaa, upumbavu tu. Kama ni njaa si wende udai haki yako huko inakotakikana? kwani Mwananchi ndo anakunyima haki yako? Upumbavu tu.
WANANCHI wa Kata ya Mzenga wilayani Kisarawe mkoani Pwani wameiomba Idara ya Afya wilayani humo kuwachukulia hatua baadhi ya wauguzi na madaktari wanaojihusisha na wizi wa dawa katika kituo hicho na kuyauza tena kwa walengwa kwa maslahi yao binafsi. Walisema baadhi ya wauguzi na madaktari hao wameanzisha viduka vidogo vya kuuza dawa ambapo huzichukua kituoni hapo na kuziuza katika viduka hivyo. Waliendelea kusema kuwa mgonjwa anapofika kupata matibabu katika kituo hicho, huwa wanakosa dawa, lakini katika viduka hivyo dawa hupatikana, jambo linalowafanya wagonjwa kuwa katika wakati mgumu wa kupata huduma bora za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya, Dk Elly Helela, alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa wauguzi na madaktari katika vituo vya afya, zahanati na hata hospitali ni vigumu kuiba dawa kutokana na vituo hivyo kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.

John Gagarini, http://DarLeo.co.tz Kisarawe, Pwani.

1 feedback :

Mzee wa Changamoto said... Wed Sep 23, 09:56:00 PM MST  

Dada, SALAAAM toka huku Shamba.
Umesahau kuwa mtu anapofumaniwa sio kwamba ndio kaanza kuzini nje ya ndoa. Na kwa nyumbani ni vivyo hivyo. Mafamasia ndio wenye famasi kubwa na zenye kuweka ushindani na za serikali. Si jambo baya kwa mfamasia kuwa na famasi kwani atakuwa anafanya alichosomea, lakini anakopata dawa sasa!!!!!!!!!!1
Hii kwa hakika ukilinganisha na tumuma za hivi ni kati ya vile tunavyoweza kusema "ajali kazini" kwani haya ni maisha ya wengi wafanyao hivi. Si sekta hii tu, bali sekta mbalimbali.
Inauma saaana Dada

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads