wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, September 18, 2009

TweetThis! Kujiandikisha kupiga kura ikiwa vurugu hivi, uchaguzi je?

Askari wa kikosi cha FFU kisiwani Pemba wakiwazunguka wananchi waliosusia zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa kukaa chini kwenye kituo cha uandikishaji cha Shule ya Kiuyu Minungwini,
Askari wa kikosi cha FFU kisiwani Pemba wakiwazunguka wananchi waliosusia zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa kukaa chini kwenye kituo cha uandikishaji cha Shule ya Kiuyu Minungwini,

Habari zinazoripotiwa kuhusiana na uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura mjini Pemba na kisiwani Zanzibar si za kufurahisha kwa namna yoyote ile.


Majuzi hapa nilisoma habari ya watu ambao ni raia wa Zanzibar kuwa wameamua kwenda kuomba hifadhi nchini Somalia kutokana na 'vurugu' hizi, si utani, habari iliandikwa na kuripotiwa katika tovuti ya BBC (bofya linki hao chini usome habari nzima).
The Zanzibari residents in Mogadishu say that out of the 192 families living in Somalia, 85 of them are still living in Mogadishu."There are six of us but we only have one mattress to sleep on, so we put our upper bodies on the mattress and our legs on the ground," Mr Ja'far says - BBC.
Habari hii imekuwa ikiripotiwa kila kukicha katika vyombo kadhaa nchini Tanzania.
Mi najiuliza, ikiwa hali hii inatokea wakati wa uandikishaji kupiga kura, itakuwa vipi wakati wa kupiga kura yenyewe? Napata wasiwasi, nahisi hali haitakuwa shwari.

Vurugu Pemba / Pemba Chaos:
  1. Nyumba zachomwa moto - http://majira.co.tz
  2. Zanzibaris seek safety in Somalia - http://news.bbc.co.uk
  3. Zanzibar sasa ni balaa tupu,mabomu risasi zarindima - http://mzalendo.net

2 feedback :

Subi Nukta said... Fri Sep 18, 05:50:00 PM MST  

Candy,
Tafadhali ahirisa safari yoyote ya 2010 hasa mwezi wa Oktobala, labda iwe ya isiyoahirishika. Tanzania ni nchi nzuri na ya amani lakini kipindi cha uchaguzi katika nchi yoyote ile huwa ni kipindi cha mpito na mambo mengi hutegemea hali ya uchaguzi na matokeo yanavyokuwa, utajajikuta unakwama katika kukamilisha mambo kadhaa na safari yako ukaijutia bure.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads