wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, September 24, 2009

TweetThis! Eti, mikoa 15 Tanzania ina upungufu wa chakula, kibo!

Nchi yangu ina watendaji wa Serikali ambao naapa nikiamua kuwasikiliza kucha kutwa naweza kupatwa na ugonjwa wa moyo ghafla! Si muda mrefu walisema kipo chakula cha kutosha, lakini sasa kiitikio cha wimbo ni 'chakula hakitoshi', wala si utani, njoo kwetu Ko'gwe uone songombingo ambayo imeshaanza kujionesha wazi wazi. Sijui mikoa mingine, sijafika huko maana nauli sina. Eniwei, wakuu wanazungumza kuwa tatizo ni ukame, halafu mi najiuliza kama wasomi na wenye madaraka walipewa dhamana ya nyadhifa hizo ili waweze kutafuta njia ya kukabiliana na matatizo haya kungali mapema, na hawakufanya hivyo, leo wanakuja kuripoti mambo ambayo wakulima walishayaona tangu mwezi wa nne, utofauti gani kati yao na wakulima? Utaalamu wao wote umeishia kuketi na kuomba Mungu mvua inyeshe, sasa haijanyesha wanakuja kutangaza rasmi kuwa iko njaa? Mwe! njaa? Acheni kejeli jamani. Yaani Aliyesoma na Asiyesoma wote 'vishoiya'. Oi!
SERIKALI inafanya tathmini katika wilaya 65 za mikoa 15 yenye upungufu wa chakula nchini, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Stephen Wasira amesema. Mikoa inayofanyiwa tathmini kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Mbeya, Lindi na Mtwara.

Ili kukabiliana na tatizo hilo Serikali imetenga tani 65, 160. 5 katika maeneo yenye upungufu na hadi Septemba 17 mwaka huu tani 50, 003. 035 zilikuwa zimeshasambazwa kwa walengwa katika maeneo yaliyokumbwa na njaa.

Hali hiyo ya upungufu wa chakula ilitangazwa jana na Bw. Wasira alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya kilimo kwa msimu wa 2009/10 na kutumia nafasi hiyo kutangaza kuendelea kutoa msaada wa chakula kwa wananchi wanakabiliwa na upungufu huo. "Serikali itaendelea kutoa chakula kwa wananchi watakaothibitika kuwa wanaendelea kukabiliwa na upungufu wa chakula," alisema Bw. Wasira.

Ili kukabiliana na tatizo hilo, Bw. Wasira alisema Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) itauza sehemu ya chakula katika soko kwa lengo la kupunguza makali katika maeneo ya nchi yatakayoonesha kuwa na bei kubwa ya chakula. Vile vile wizara inatoa wito kwa mikoa kuwahamasisha wafanyabiashara kununua chakula katika mikoa na maeneo yenye ziada na kukiuza katika maeneo yenye upungufu. Waziri huyo alisema serikali itaendelea kusitisha biashara ya uuzaji wa mazao ya chakula nchi za nje hadi hapo hali itakapokuwa nzuri.

Bw. Wasira alitoa wito kwa wakulima waliopata mavuno ya ziada wahifadhi chakula cha kutosha kwa mahitaji ya kaya zao na kuuza ziada tu katika soko la ndani. Kwa upande mwingine katika msimu wa mwaka 2008/09 hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula haikuwa nzuri kutokana na sehemu kubwa ya nchi kukabiliwa na ukame, hali iliyosababisha bei za vyakula nchini kuwa juu na kufanya watu wa kipato cha chini kuwa na hali ngumu.
Godfrida Jola na Prosper Mosha, http://majira.co.tz,Tanzania.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads