Kizungumkuti cha Vithlani na sheria za Tanzania za mwaka 1880!
Nilikuwa nasoma habari ya 'now you see me now you don't' ya kumsaka mtuhumiwa Shailesh Vithlani kwenye gazeti tango la THISDAY (http://www.thisday.co.tz/News/6175.html) nikabaki kushusha tu pumzi.
Ama kwa hakika tuna matatizo makubwa. Yaani... hata nashindwa nishangae au nisikitike, ni kwamba, tangu tumepata 'uhuru' mwaka 1961 hadi leo hatujaweza kubadilisha sheria, kanuni na taratibu za Mkoloni kuwa za kwetu? Ni lazima tuzunguke kwa Mkoloni ili kupata kutimiza mahitaji yetu? Kwa hivyo likitokea kosa jingine, tutarudi kwa Mjerumani kuulizia sheria aliyoiweka alipotutawala? na likija la nyuma ya hapo tutamtafuta Tipu Tipu na Bushiri watupe sharia za Oman? Najua kuna mtu ana uelewa zaidi kuhusu hizi sheria na ataniambia, kama hujui kitu kaa kimya, mi kwa bahati mbaya kama sijui nitasema ili anayejua anikosoe nami nipate kujua, siwezi kubaki na ujinga wangu. Ila kwa hili la kupatikana-na-kupotea kwa mtuhumiwa na sheria mkanganyiko hivi, hadi leo? sheria zile zile hasijabadilishwa? Tuna laana nawe. Si bure, a - a! Haya manne hapa ndo yaliyoniacha nashangaa:

- He stressed the point that the extradition of any suspect from Switzerland is only possible with the consent of the wanted person himself/herself, or through a decision of the Swiss Federal Office of Justice.
- Explained Schlapfer: ”In past years, there have been no extradition cases between Tanzania and Switzerland. In principle, the application of the Extradition Treaty between Switzerland and the United Kingdom of 26 November,1880 remains possible.
- In case the relevant conditions of that treaty are not fulfilled, Swiss domestic law is applicable, in order to grant cooperation as far as possible.
- "This effectively means that UK authorities, via the long-standing extradition treaty with their Swiss counterparts, are in a position to lodge an authentic application for Vithlani’s extradition on confirmation that the fugitive suspect is indeed in Switzerland
0 feedback :