wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, August 25, 2009

TweetThis! Hongera Mubelwa! Una kipaji cha pekee!

Hii posti nimeichukua toka kwenye blogu yake ya ChangamotoYetu. Huyu dogo amekuwa akiblogu kwa mwaka mmoja sasa na posti zake zinatia changamoto si kidogo. Leo ametimiza mwaka mmoja akaja na posti hii unayoiona hapo chini, yaani kila neno lililokozwa wino na kuandikwa kwa herufi kubwa lina linki ya blogu! Jamaa ni kichwa, yaani kwa ufupi, ni fulu kipaji!
Hongera sana Mubelwa mwana wa Bandio, tuendelezee ChangamotoYetu!
Nimeipenda sana hii posti!
Ni kweli kuwa siku kama ya leo miezi 12 iliyopita, niliamua kufuata ushauri wa Kaka MICHUZI wa kuanzisha BARAZA langu ambalo lingeniwezesha niJIACHIE kimawazo hapa na kuwakilisha mengi kwa jamii. Nilifuata ushauri huo kwani karibu kila NUKTA ya MAISHAyangu nimekuwa nikizama MAWAZONIUTAONA NA KUSOMA UNACHOKIPENDA tena toka kwa wazalendo. Na hata MWANANCHI MIMI nilipoamua kujikita katika ukumbi huu, nilijua kuwa kuna mengi tunayostahili kuyasema ili jamii yetu iJIELEWE kwa namna mbalimbali lakini kuu ikiwa ni kuwafanya wapate UTAMBUZI NA KUJITAMBUA. Hilo si jambo rahisi, kwani kuna waonao UPANDE WA PILI wa mambo kama wenye manufaa zaidi (hata kama si wa manufaa kwa jamii) na hilo hutusababishia kazi ya ziada katika UDADISI wa kile tuandikacho na hasa katika UCHAMBUZI wa habari mbalimbali. Uchambuzi huu hubainisha ukweli na uozo unaoendelea na si ajabu sasa kushuhudia VIONGOZI NA HOFU YA KALAMU zinazoanisha mapungu, uongo na udhaifu wa utekelezaji wa ahadi zao na haki za wananchi.
Kwa mwaka mmoja niliokuwa karibu saana katika kufuatilia majamvi yetu haya, nimejifunza meengi sana ndani mwake. Blogu zetu zimekuwa na zitaendelea kuwa sehemu muhimu kwa jamii yetu, na zaidi kwa kuwa sasa twawafikia wengi tangu tulipoamua kuwa ni SWAHILI TIME kwa teknolojia hii. Tuna mada tofauti zenye hadhira tofauti kwa nia tofauti na kupafanya kuwe na majina tofauti na hata wale wapaonapo kama KIJIWENI, bado tunajivunia kuwa ni kijiwe chema chenye mengi mema. Tujuao faida hatuwezi kuacha kukaa kijiwe hiki cha blog. Habari ni mseto kwani tunao wafuatiliao habari zaMTAA KWA MTAA ambao kila kukicha wanakuja na habari za namna ya kutuwezesha kupigana na magumu ya maisha na kutambua kuwa INAWEZEKANA kuikomboa jamii yetu. HAPA KWETU(bloguni) pamekuwa chachu ya suluhisho la mengi na kuifanya jamii iVUKANI (Ooops!! nimeongea ki-ukweni nikimaanisha iamke) katika usingizi iliyopo. Blogu hizi zimeifunza jamii kuwa UHURU HAUNA KIKOMO na kuifunza mengi yasiyojulikana kwayo huku ikiwasisitiza kutojiona wajinga kwani ukweli uko kwetu sote kuwa UTAKAPOJUA HUJUI NDIPO UTAKAPOJUA. Nililojifunza katika mwaka huu wa kuperuzi kwenye blogu zetu ni kuwa tunagusa kote na yote. TunatumiaHADUBINI zetu kuchungulia na kujulisha KULIKONI UGHAIBUNI na kwa wale wasomi hawaachwi nyuma kwani kuna wanaowapasha yatokeayo huko kwa kuangalia PILIKA VYUO VIKUU. Walio na mpango wa kuingia huko pilikani wanaendelea kuwa ndoto hizo wanapoweza kuona namna ya kupata SCHOLARSHIPS kwa wenye uhitaji na waliomaliza na kuanza kazi na maisha, wanasoma mchakato mzima wa UCHUMI NA FEDHA.
Lakini si hayo tu. Tunawezeshwa kuANGALIA BONGO na hata nje katika SPOTI NA STAHERE na kujua mengi katika ujumla wa ANGA LA MICHEZO. Tunapata TASWIRA katika BONGO PICHA na hata habari kuhusu BONGO MOVIES zinazorekodiwa kila uchao bila kusahau kizazi kinachoonekana kuwa na PASSION 4 FASHIONambacho chaja juu kwenye mambo ya FASHION na pia katika fani yaUMODO. Tumeanza kutumia blog zetu kuenzi kazi za kila BONGO CELEBRITY ambao kwa namna moja ama nyingine wanaonekana kusahauliwa na wenye mamlaka na hii ni kuonesha kuthamini mchango wa waliotutangulia. Iwe ni katika muziki wa asili ama ile tuijumuishayo katika AFRICA BAMBATAA ama aina yoyote ile ya muziki. Kwa ufupi, kwenye blogu zetu twaweza kupata kila KALI NA MPYA TOKA BONGO. Niseme kuwa blogu zetu zatupa FULL SHANGWE. Uzuri wa mseto wa logu zetu, ni kama nilivyosema awali kuwa unatupa yote. Humu twapata NYIMBO ZA DINI na pia mijadala mbalimbali ihusuyo imani kutoka katika zile zilizojikita katika injili pekee (kwa lugha nyingine twasema STRICTLY GOSPEL).
Lazima tukubali kuwa blogu zetu ni MWANGAZA na kiunganishi muhimu kwa jamii yetu. TWATAKIWA KULITAMBUA HILO na kulienzi. Tusiwe kama wale wapishi :"wababaishaji" watumiao sura za walaji kupima ubora wa vyakula vyao wakisahau kuwa CHAKULA KITAMU NA KICHUNGU VYOTE VYAWEZA KUMFANYA MLAJI AKAKUNJA USO. Humu ni mahala unapoweza kuelimika vema, tuna hazina ya busara na mafunzo humu. Tuna ABSOLUTELY AWESOME THINGS katika blogs zetu ambazo takribani kila moja imejidhihirisha kuwa THE HILL OF WEALTH katika yale izungumziayo.
Labda mwisho niwashukuru kinadada wanaoendeleza fani hii wa nguvu zote. Ma-DIVA hawa wamekuwa WANAWAKE WA SHOKA katika kueleza, kutetea na kuelimisha mambo mbalimbali ambayo kinakaka / kinababa wasingeweza kuyajengea hoja kikamilifu.
Kwangu mimi blogu ni kama nyumbani na sina budi kuwakaribisheni katika awamu ya pili na blogu hii. Nasema KARIBUNI NYUMBANI. Nyumba ambayo inajumuisha yooote toka ulimwenguni. Ni ulimwengu wangu mdogo (ama niiseme kimsisitizo kuwa MY LITTLE WORLD) tunakojuvyana na kueleweshana mambo mbalimbali. Tukitafuta maisha bora kwa kila mTanzania. Na nina hakika tukiwa na umoja na niaTUTAFIKA TUUU!!!.

2 feedback :

Mzee wa Changamoto said... Tue Aug 25, 02:53:00 PM MST  

Da Subi, Da Subi, Da Subi!!!!!
Sijui nirejee lipi ambalo sijasema na sina hakika kama utasoma yote maana najua NIMECHOKA KUSEMA NAWE YAWEZEKANA UMECHOKA KUSOMA.
Lakini kwanza NISHUKURU kwa uwepo wako katika ulimwengu huu wa ku-Blog. Hapa ni kama "chuo" fulani tunaponyonya meengi kuhusiana na blog na ambapo tunaona mabadiliko nasi kujaribu kuyaendeleza kwetu.
Asante kwa kuwa KISIMA KISICHOKAUKA MISAADA ya kiufundi na unajua ni mara ngapi umekuwa ukinisaidia kuboresha "kibaraza" changu. Naweza kuwa mmoja wa watoa maoni wakuu hapa na kwingine kwingi lakini ni kwa kuwa NAJIFUNZA TOKA KWENU. Binafsi umekuwa msaada saaana hasa nilipotapatapa "kujazia" blogu yangu sauti. Nakumbuka Tarehe 16 November ilikuwa moja ya siku za furaha saana kwenye Blog uliponifanikisha hili (Najua hukuiona hii. Hebu iangalie hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/11/rockaway.html)na hiyo ilikuwa siku moja tu kabla ya Birthday ya Mamangu niliyemuwekea Song For Mama.
Mambo ambayo umeyarahishisha kwangu na ambayo ushirikiano wetu bloggers umeyafanikisha kwenye "changamoto yetu" ni mambo ambayo hata ikitokea nikawa nje ya blog sitaacha kujivunia. Utundu wa kufanya hili na lile, kujieleza bila kukwaza na kuwasilisha hisia halisi za ukweli wa maisha ya wahitaji ni mambo ambayo NAWASHUKURU SAAANA NINYI.
Hakuna ninalojivunia katika blog kama kuwa na uhusiano mwema na karibu kila mmoja ninayewasiliana naye na umekuwa mfano kwa wengi.
Nakushukuru wewe, na NAWASHUKURU BLOGGERS WOOOTE WAPIGANIAO NIA NJEMA YA MAISHA MEMA KWA JAMII NJEMA ILIYOJAA WEMA YA TANZANIA NJEMA
Uwe Mwema dada na HESHIMA, AMANI NA UPENDO NAKUTAKIA
Blessings

EDWIN NDAKI (EDO) said... Sun Sep 06, 04:46:00 AM MST  

Ni kweli Subi kijana anafanya kazi nzuri sana.Na ni jambo la busara na uungwana kumpongeza na mkumtia mtu moyo anapofanya jambo zuri sio kuwa kama wana SI HASA ambao mazuri wanayaona mtu akidedi..

tutafika tu

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads