wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, August 01, 2009

TweetThis! Drugs worth millions go missing in Tanzania

Kumbe ndiyo sababu watu wanafia mabarabarani na wengine wananunua 4WD? Alaaa! Ninyi kwa kweli, kweli ya kweli nasema kweli, ipo wakati mtakiona kilichomnyoa kuku manyoya, walahi si utani! Hii laana itakula kwenu. Na zitawatokea mapuani kwa spidi hamjawahi ona! Subirini apo hapo. Ninyi nakula mali ya mwananchi? Sawa iyo? Haaata! Hiyo si sawa...!

Part of Nick Mathiason of The Observer, Sunday 2 August 2009 reads:
Millions of dollars worth of life-saving drugs destined for Tanzanians living with AIDS, Tuberculosis and Malaria are missing or have expired, an internal Global Fund audit has discovered.

The Global Fund audit discovered large amounts of drugs sitting in warehouses past their sell-by date and found that other vital medicines were unavailable due to serious logistical failures. The audit also revealed that drugs worth $819,000 (£497,000) were missing.

Unless the situation improves, the Global Fund, the main source of funds for programmes to combat Aids, tuberculosis and malaria, has threatened to withold new funding to Tanzania.

Senior officials in the Global Fund say the country's national store does not have medical management systems with real-time online data. Logistics problems are so serious because anti-retroviral medicines have a short shelf life.

The fund's spokesman said: "It is vital that life-saving drugs get through to those who need them most and action must be taken to ensure this sort of thing does not happen in future."

Read the uncut story via the following link: http://www.guardian.co.uk/business/2009/aug/02/tanzania

3 feedback :

Masangu Matondo Nzuzullima said... Sat Aug 01, 07:44:00 PM MST  

Kweli hawa watu wana roho ngumu. Binadamu mwenzio anakufa kwa UKIMWI na wewe uliyepewa dhamana ya angalau kuhakikisha kwamba anapata msaada unauiba huo msaada - unapata mamilioni unajinunulia shangingi na kujenga jumba la kushangaza, then what??? Hakuna hata ile moral guilty. Hawa watu ni wauaji. Inasikitisha sana!

Juzijuzi hapa nilituma vitamin maalumu kwa ndugu yangu aliyekuwa anazihitaji sana. Mbali na kuandika memo na kuomba sana kwamba dawa hizo zilikuwa ni kwa mgonjwa aliyekuwa anazihitaji na kwamba hazina gharama yo yote kubwa na kwamba zimfikie - kamwe hazikufika. Zilipotelea Dar es salaam. Mpokeaji wake akienda pale anaambiwa zimepelekwa Mwanza, Mwanza wanasema hawajaziona. Tracking yangu ikawa inaonyesha kwamba zilipokelewa Dar. Watu wanaiba hata vitamin za dola 40 zinazokwenda kwa mgonjwa! Kazi ipo tena ngumu sana!

Mzee wa Changamoto said... Sat Aug 01, 08:02:00 PM MST  

Pole Prof. Mie kuna mzigo wangu una miaka mitatu kwenye "traffic" ya Washington DC - Dodoma.
Mie sijui kwanini hata wimbo wa Taifa usibadilishwe? Hivi ni kweli kuwa TUNAMUOMBA MUNGU A"WABARIKI VIONGOZI" WA TANZANIA? Heshima na umoja na amani tunavyowaombea sijui ni kwa manufaa ya nani?
Mimi sijui. Lakini ninaloona ni kuwa tunazidi kupelekwa pale ambapo AMANI HAITAKUWA NA THAMANI na kuwa na UPENDO HAKUTAKUWA MWENENDO KWA HAWA WACHAFUZI.
Kila mtu na ATABEBA MZIGO WAKE.
Walahi tena
!@$%^&*()_+_)(*&^%^&*()_+

Subi said... Sun Aug 02, 12:41:00 AM MST  

Pole sana Prof. Matondo, ukituma kitu Tanzania hakikisha una mtu wa kupokelea pale Dar, kisha atume Mwanza kwa usafiri wa njia ya basi au kupitia ndugu/jamaa/rafiki anaeyeelekea huko. Ninajua hii haitakiwi kuwa hivyo lakini kutokana na uzembe ulipo pale, ni vigumu sana kuwakaba wakupe amaelezo ya kilipo kifurushi chako.

Mzee, juzi kwenye e-group moja tunajiita PorojoClub, nilipatwa na hasira na wimbo wa Taifa niliuandika kwa kuimba hivi:
Mungu ibariki Afrika.
Wabariki WANANCHI wake.
Hekima Umoja na Amani.
Mungu, tupatie. Mali na Afya njema!
Isipokuwa Viongozi. Isipokuwa Viongozi.
Tubariki, Walalahoi wa Afrika.

Ni kama WaTz wengi kwa sasa tunawaza mamoja, hili ndilo linalonipa matumaini kuwa mabadiliko yatatukia Tanzania, ole wao waliojidhania wamesimama, ninawahurumia kwa anguko watakalolipata.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads