wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, July 15, 2009

TweetThis! Wagonjwa watibiwa kwa tochi usiku - Kisarawe

Kwa kweli tunapiga hatua katika maendeleo, kuelekea nyuma ama mbele? ah, ni mbele. Ninyi hamuoni? Mna visa nawe, si bure. Ni vile basi tu sijui hamna kurunzi ama vipi wivu tu umewashika. Yaani hamuyaoni ninyi? Kazi yenu kupiga keleeele kelele, keleeele tu, wakati mafanikio yanaonwa na wachache kwa mwanga wa kurunzi. Ah, kwa mwendo huu babu? mmh, natafuta mawe ya kurunzi, kurunzioooi yoyo!

Utani tuache, hapo kijiji cha jirani wanatibiwa hospitali kwa mwanga wa tochi, sikiliza John Gagarini, wa Kisarawe alivyoiripotia DarLeo, ya leo leo:
KITUO cha afya cha kata ya Masaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani kinakabiliwa na tatizo la umeme hali inayofanya wagonjwa kutibiwa nyakati za usiku kwa kutumia tochi (kurunzi).

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kuangalia miradi ya afya katika wilaya hiyo, Mganga mkuu wa kituo hicho Dk. Ahmed Mkamba alisema tatizo hilo ni kubwa kwa wagonjwa hasa wale wanaokwenda nyakati za usiku kituoni hapo.

Dk. Mkamba alisema kuwa tatizo hilo limekuwa likisababisha utendaji kazi nyakati hizo kuwa mgumu na kusababisha usumbufu mkubwa wakati wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wao.

"Tunaiomba Serikali kutusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo hili ambalo limekuwa likitupa taabu kutoa tiba hasa anapokuja mgonjwa ambaye labda kapata ajali na anataka apate huduma ya kushonwa inabidi tutumie tochi au taa ya chemli," alisema Dk. Mkamba.

Alisema kuwa mbali na kuwa na tatizo hilo pia kituo hicho kinakabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya ukosefu wa maabara na wataalamu wake pamoja na vifaa, na upungufu wa wafanyakazi hali inayowafanya wafanye kazi kwa saa 24 ili kukabiliana na upungufu huo.

"Mgonjwa ambaye anahitaji vipimo inabidi tumpeleke hospitali ya wilaya kupata vipimo jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wagonjwa ambao wanakuwa wamezidiwa," aliongeza Dk. Mkamba.

Naye Mganga mkuu wa wilaya Dk. Elly Helela alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa ofisi yake inayashughulikia matatizo hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na mpango wa kutumia umeme wa jua kukabiliana na tatizo la umeme.

Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2006 na kinahudumia wagonjwa 800 kwa mwezi ambapo wagonjwa hutoka kwenye vijiji vya Bwama, Msanga Zalala, Mkamba, Kisanga na Kipanga kutoka kata tatu za Msimbu, Masaki na Kibuta.

2 feedback :

Anonymous said... Wed Jul 15, 05:51:00 PM MST  

Kwa kweli mimi nimeguswa na nakushukuru sana Dada Subi kwa kutuletea habari za namna hii,sishangai na nakubaliana kabisa na unachosema. tena mbona hapo umetumia lugha ya kupoza. Ngoja mimi nikupe ushuhuda wa nilichokusanya kwenye utafiti wangu na uzoefu wa maeneo ya pwani vijijini ambako ndiko wilaya ya Kisarawe ipo pia.

Mbali ya kutumia kurunzi. Kuna sehemu nyingine. Mgonjwa hasa mama mjamzito akifika, lazima atoe fedha za mafuta, lazima atoe fedha za bomba la sindano ingawa eti anaambiwa dawa ipo.Ngoma inakuwa mbaya zaidi kama akikataa, kwani itabidi ndugu watembee usiku huo kilometa kibao kwenda kununua mafuta na bomba la sindano. Sijaongelea hapo glovu.

Tunajua kwamba vyombo vya hospitali lazima vifanyiwe sterilization. Kwa sababu hakuna mafuta, basi usishangae mgonjwa anaambiwa akanunue kuni au atoe fedha za kuchemshia vyombo. Kwanza kuchemsha kwa kuni kamwe hakufanyi vyombo viwe salama, kwa hiyo mgonjwa anatoa fedha, na hapohapo anapata maambukizo mengine toka kwenye vifaa, sitaki kuyataja baadhi ya maabukizo kwani hali ni mbaya.

Mbali ya wizara ya afya kutoa tamko la huduma za ambulance kuwa bure.Hali halisi sivyo ilivyo kule vijijini. Mganga wa zamu atadai kwanza fedha za kuitia ambulance (voucher), baadaye atamdai mgonjwa fedha kiasi cha shillingi 10,000-15,000 eti ni ghalama ya mafuta.Ingawa ambulance inaweza kuwa ni bure , Dereva na mganga wanachikichia hizo fedha. Mara nyingi wanawatarget mama wajawazito kwani wanajua hawana jinsi na muda wa kuulizia, wapo kwenye uchungu, wamechanganyikiwa, wanataka kuokoa kichanga wao na mama yake.

Swali la kujiuliza ni je Halmashauri haziwezi kupunguza kero hizi?.Jibu ni ndiyo, zinaweza! zinaweza kabisaaa, kwani baadhi ya kero hizi zipo chini ya uwezo na udhibiti wao.

Idara ya afya katika halmshauri zinauwezo sasa wa kupanga mipango yao (health interventions) kulingana na vipaumbele na matatizo yanayo wasibu (local problems).Pia kwa kutumia their communities strenght and resources. Hiyo ni kutoka na mabadiliko ya serikali za mitaa (sectoral reforms under decentralization by devolutions ya miaka kama saba iliyopita).

Kuhusu matumizi ya tochi- Idara inauwezo wa kusambaza chemli katika zahanati zote na kuwapatia mafuta ya taa kila wanapokuwa wanawapekea gesi au mafuta ya frigi za kuhifadhia sindano za chanjo, kwa hiyo ni suala la kuongeza kabadgeti kidogo tu, baadaye wanaweza kwa kila financial year kupanga kuweka soral power katika vituo vitatu au vinne kila mwaka. Nasema ni suala la how do they allocate their resources kwenye COMPREHENSIVE DISTRICT HEALTH PLANS (CCHP) zao.

Kuhusu mabomba ya sindano, glovus ni utashi tu, hakuna sababu,ni uzembe, kutofuatilia, na njaa kali, wala sihitaji kulielezea hili.

Kuhusu vifaa vya kuchemshia. Hili ni suala gumu kidogo, lakini linawezekana. Najua hawawezi kununua modern sterilization machines kwa zahanati zote, kwanza nyingi zinatumia umeme, ambalo ni tatizo pia, lakini wanaweza kuimprovise angalau vifaa vitakavyoweza kufanya sterilization at least 80-90%. Kuna majiko ya sayari, yanatumia gesi, kuna gesi cookers kubwa sana. vyote ni kwa bei rahisi Bongo na vinaweza kutumika hata vijiji ndani kabisa. Gesi watakuwa wanarefill wanapokuwa wanawapelekea gesi za frigi za chanjo.Utashangaa kila mwaka kuna fedha nyingi za trainings on sterile procedures,mafuzo yakiisha kwaheri,wahitimu hawapewi vitendea kazi.

Suala la maji ni tatizo kubwa sana. Nalo linawezekana. Kwa kutumia nguvu za wananchi, kuchimba visima virefu au kugema na kuhifadhi maji ya mvua kwenye matank, Hii inahitaji utashi tu wa wapanga mipango wa idara ya afya katika wilaya.

Nitaendelea baadaye

Dr Pons

Anonymous said... Wed Jul 15, 05:54:00 PM MST  

Uzoefu wangu mimi, unanilazimisha kutuma lawama nzito kwa wapanga mipango idara ya afya za halmashauri nyingi (Council health Management Team). hawana local criterion za kupanga mipango yao. Interventions zao nyingi zinajikita kwenye seminars, kongamano na retrainings kibao.Zaidi ya asilimia 40% ya badget ya afya inaliwa na seminars, trainings na kongamano. Sitaki kuongelea posho kwani nitakuwa nawagusa sehemu mbaya.Mbaya zaidi, trainings hizo zinajirudia kila mwaka. Hivi hao wanafunzi gani jamani?

Nilijaribu kipindi fulani kuwauliza hawa wanamipango wa idara ya afya katika wilaya yangu kwenye pre-planning meeting fulani, ni vigezo gani walitumia kuandaa zile activities. kila mtu alibaki kimya, nikaendelea kuwauliza ni matatizo gani walikuwa wakikumbana nayo kwenye utoaji wa huduma kwenye zahanati wakati wakifanya, wao wanaziita "Supportive supervisions" wanamaneno mazuri hao!eti supportive! wakasema: 1) hakuna mafuta ya taa 2)hakuna glovu na sindano 3) Poor sterilization 4) Hakuna maji NK. Nikawaambia, kwa nini sasa hakuna hata mmoja wao aliyeweka vitu hivyo kwenye mpango,kuna maana gani ya kutengeneza mpango,nini maana ya wao kwenda kufanya hiyo supportive supervision huku walikilpwa karibu shillingi 20,000 kwa siku. Jamaa wakabaki kimya, kwa kweli inauma, fedha zipo(BUSKET FUNDS & CAPITATION &COST SHARING,MTEF nk). Ingawa hazijawahi kutosha lakini zaweza kupangwa vizuri kwa maslahi ya wananchi, kwani ni zao.

Kihoja kilichonisikitisha ni kwamba kila mmoja alipewa mda wa kwenda kurudia activities zake wakiaddress vile ambavyo tulikubaliana.Wakafanya kama tulivyokubaliana, tukaingiza fedha za kutengeneza mashine za maji, kuchimba visima, kununua sterilizers na majiko ya gesi, kuongeza supliment budgetya glovus na sindano kwenye zahanati na vituo vya afya, kutenga fedha za vochers kwa wakuu wa zahanati,NK.Tukapunguza trainings zote na nyingine tukaziunganisha kama ni 1 WEEK REFRESHER TRAINING ON IMCI, tukakubaliana waingize humo na TB, MARALIA, SKIN DISEASE,nk.Tukasave fedha nyingi ambazo tulizidiverge kwenye activities tajwa hapo juu.

Mpango ukawa umekamilika, kabla ya kupelekwa mkoani, total budget ikawa imeongezwa,si unajua tena mambo ya donor dependent budget! ikabidi turudie tena kufidia nyongeza nami nikawa sipo. Unajua kilichofanyika! Waliondoa kila kitu nilichaoagiza, wakaingiza trainings zao na maposho .Nilitaka kuzimia baada ya mwaka kukuta vitu ambavyo viliondoka ndivyo vinatekelezwa na vile vya wananchi vimeondolewa.

Si lengo la ushuhuda huu kumlaumu mtu.Bali nilitaka kusema kuwa HATUNA VIPAUMBELE KATIKA UPANGAJI WA MIPANGO YETU. KILA MPANGAJI ANAJIANGALIA YEYE KWANZA ATAFAIDIKA VIPI NA MPANGO HUO. MLENGWA AMBAYE NI MWANACHI ANAKUWA KIPAUMBELE CHA TANO KAMA SI CHA MWISHO.

To conclude, I will not even question the credibility of our local governments’ planning tools. Effective planning is supposed to be supported by continuous needs assessment and evaluations of the previous and the current developmental programs. Planning without base, planning by copy and paste is like seeding in a dry land, never expect good yield. Infarct, that plan will never yield the intended outcomes. We really need a total reforms of our planning procedures and our MIND-SET.

Dr Ponsi.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads