Raisi wa Kenya kuzuru Tanzania siku ya Alhamisi
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Kenya, Raisi wa nchi hiyo mhe. Mwai Kibaki anatarajiwa kufanya ziara nchini Tanzania siku ya Alhamisi.
Akiwamo nchini, atakutana na Raisi wa Tanzania, mhe. Jakaya Mrisho Kikwe ambapo watatia saini baadhi ya mikataba na maafikiano yanayohusu nchi hizi mbili.
Vile vile, Raisi huyo wa Kenya atafungua ubalozi wa Kenya nchini.
Anatarajiwa kutembelea visiwa vya Zanzibar na kuzungumza na Raisi wa Zanziba mhe. Abeid Amani Karume.
Ndege ya Raisi na watakaoongozana naye inatarajiwa kupaa kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta saa tatu asubuhi.

0 feedback :