wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, July 21, 2009

TweetThis! Uhaba wa madaktari bingwa Tz wasababisha ulemavu

Mi kwa kweli nashangaa sana, sijui vipaumbele vya Tanzania vipo wapi kwa kweli. Kwenye elimu hola, kwenye kilimo kapa, kwenye miundombinu mwendo wa ado ado kwenye afya ambayo ndiyo mama wa kila mtu kuweza kufanya shughuli zake ndiko kumedorora, hoi bin taaban! Leo wanalalamika hakuna wataalamu wakati wanaotaka kusoma utaalamu huo hawapewi nafasi, pale Muhimbili ulikuwepo msemo  maarufu kuwa, 'watakunyonya macho' kwa maana kuwa, kujitahidi kufikia ngazi zao, wanakukaba kama 'sungusungu' kuhakikisha jasho linakutoka, mwenyewe utaachia ngazi. Sasa kwa mwendo huo wa kukabana na kutishana na kuogopeshana, mtu  mzima anauwezea wapi? Wanaogopa nafasi zao kunyemelewa... sasa haya ndiyo matokeo yake.

Habari kutoka gazeti la HabariLeo
TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu hali inayosababisha baadhi ya wagonjwa kukosa huduma za upasuaji kwa wakati na wengine kupata ulemavu. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Ofisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Almas Jumaa wakati alipozungumza na 'HabariLeo'.

Alisema madaktari hao hivi sasa wapo watatu wanaotoa huduma nchi nzima hali inayosababisha baadhi ya wagonjwa wanaopata matatizo hayo kukosa huduma kwa wakati na wengine kusafiri umbali mrefu kumwona daktari ili waweze kupewa huduma.

Aliiomba serikali kuhamasisha zaidi watu mbalimbali waliofuzu masomo ya sayansi kusoma kozi za aina tofauti ili waweze kuwasaidia wagonjwa wanaokumbana na matatizo hayo.

Alisema asilimia 70 ya wagonjwa wanaopokelewa Moi wanatokana na ajali, kuvunjika mifupa, magonjwa ya kichwa mishipa ya fahamu na asilimia 30 wanatokana na magonjwa ya kuzaliwa, kujaa miguu kwenye visigino na magonjwa yanayowapata watu wenye umri mkubwa.

Alisema hospitali hiyo pamoja na hospitali zote nchini zinakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kutolea huduma za upasuaji na viungo bandia hali inayosababisha baadhi ya wagonjwa kuwatupia lawama watoa huduma wakati vifaa muhimu havifiki kwa wakati.

Hata hivyo aliwasihi wagonjwa mbalimbali wanaofika Moi kupata huduma hususan ya viungo bandia kuwa wavumilivu mara wanapoambiwa vifaa hivyo havipo kwani wakati mwingine vinachelewa kufika hospitalini hapo kwa sababu ya usafiri kutoka nje ya nchi.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads