wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, July 28, 2009

TweetThis! Picha: Mkutano Mkuu wa CCM Tawi la London 26-07-2009

Habari na picha zimeletwa na M.O toka London.

Na Mwandishi wetu.
Takribani wanachama Mia Tano wa CCM Nchini Uingereza wahudhuria Mkutano Mkuu wa Tawi jijini Reading UK uliofunguliwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mhazini Mkuu wa CCM Taifa Mhe.Amos G. Makalla.
Pamoja naye toka Tanzania ni Mshauri Mkuu wa Siasa wa Mwenyekiti wa CCM Taifa
Mhe.Rajabu Luhwavi.

Katibu wa Tawi Bi Suzani Mzee aliwakilisha Taarifa ya maendeleo ya CCM UK na Mwenyekiti wa CCM UK Nd. Maina Owino alimkaribisha Mhe. Amos Makalla kufungua rasmi Mkutano huo Mkuu.
Mhe. Makalla alisema kazi ya ujenzi wa Chama na Taifa la Tanzania ni letu wote na lazima wote kwa usawa bila ubaguzi tuvune matunda ya Uhuru wetu

Viongozi hao wa kitaifa waliwataka Watanzania kuongeza juhudi za makusudi kuitangaza Tanzania kwa mema na pia Kutosita kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali ili kuboresha utawala bora na maadili mema ya uwajibikaji.

Aidha wote wamewataka Watanzania wanaoishi Ughaibuni wasikae kimya na watoe taarifa katika vyombo husika pale wanapo ona hawajatendewa haki kwa mujibu wa sheria za Tanzania mara warudipo nyumbani.

Watanzania wengi walihamasika na kuendelea kujiunga na CCM siku hiyo ya Jumapili 26/07/2009. 0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads