wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, July 22, 2009

TweetThis! Pale tunapokuwa na keki ya njano na kuila tusiile (au tukiila, twafwa!)

Bila kificho, Tanzania ina "keki ya njano" yaani kwa jina jingine, madini ya Uranium. Inafahamika kuwa madini haya ni mahsusi kwa utengenezaji wa mabomu hatari sana duniani. Hii ndiyo inayosababisha nchi kama Iran na Korea na nyingine za iliyokuwa shirikisho la zamani la Urusi ziitwe 'ncha ya uovu' (axis of evil). Sasa kwetu madongo kuinama, tuna karibu kila kitu kinachohusishwa na utajiri lakini tutizame sisi wananchi tulivyo choka mbaya utadhani tumewasili mnadani tokea safari ya alfajiri ya jana na Baba Yeyoo.

Sasa kukufahamisha kuwa tumekujatiwa adabu kuhusu hiyo keki ya njano kuwa japo tunayo, tusithubutu kuidokoa la sivyo 'itatuua', basi mtia adabu wa Shirika hilo la kuzuia ulaji keki kwa wapishi yaani The International Atomic Energy Agency (IAEA) mheshimiwa Katibu Mkuu wake ndg. Mohamed ElBaradei atawasili nchini kwa ziara rasmi ya kukutana na Raisi wa Jamhuri. Akiwa katika ziara hiyo atakutana waziri  wa Tume ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano mheshimiwa Peter Msolla. Vile vile atafika katika hospitali ya Ocean Road inayohusika na matibabu ya wagonjwa wa saratani ili kuzindua mradi unaofadhiliwa na IAEA.

Yote  haya yanafanyika baada ya kutangazwa kuwa kampuni takribani 70 zimetaka kibali cha kujishughulisha na uchimbaji unga wa keki ya njano.

Tutajuuuta kuwa na keki ya njano!

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads