Nimeshindwa kuvumilia. Wacha Dk Ponsiano akuelezee ndo uelewe!
Sijui kama kweli kuna mtu anaweza kuvumilia hali hii ikiwa anao uwezo wa kufanya maamuzi kubadili hali ilivyo. Eti akaamua kupuuzia kwa vile tu, haimwathiri yeye moja kwa moja? Labda awe punguani. Walahi naomba mtu wa aina hiyo siku moja apatwe na taabu itakayomfunza adabu, na akiwa mkaidi, limpate na jingine hadi ashike tabia njema. Tumechoka sisi kuishi maisha haya ya kudhulumiwa huku ninyi mkiendelea kutusweka na kutulazimisha kujipanga kwenye handaki la umasikini kwa uongozi wenu mbovu na wa kilaghai kabisa. Mnafurahi wananchi wanavyotaabika il hali ninyi mnahakika ya kula na kusaza na kufanya sherehe kwenye majumba makubwa na kumwaga vyakula na vinywaji? Siku moja vitawatokea kwa puani nakuelezeni, iwe hapa au ahera. ...mi naendelea kutafuta gobole... nikilipata? hamna rangi mtaacha kuhesabu!Maoni ya Dk. Ponsiano yametokana na habari ya jana, 'Wagonjwa watibiwa kwa tochi usiku - Kisarawe"
Kwa machungu Dk. Ponsi anaelezea kwa kuandika:Kwa kweli mimi nimeguswa na nakushukuru sana Dada Subi kwa kutuletea habari za namna hii,sishangai na nakubaliana kabisa na unachosema. tena mbona hapo umetumia lugha ya kupoza. Ngoja mimi nikupe ushuhuda wa nilichokusanya kwenye utafiti wangu na uzoefu wa maeneo ya pwani vijijini ambako ndiko wilaya ya Kisarawe ipo pia.
Mbali ya kutumia kurunzi. Kuna sehemu nyingine. Mgonjwa hasa mama mjamzito akifika, lazima atoe fedha za mafuta, lazima atoe fedha za bomba la sindano ingawa eti anaambiwa dawa ipo.Ngoma inakuwa mbaya zaidi kama akikataa, kwani itabidi ndugu watembee usiku huo kilometa kibao kwenda kununua mafuta na bomba la sindano. Sijaongelea hapo glovu.
Tunajua kwamba vyombo vya hospitali lazima vifanyiwe sterilization. Kwa sababu hakuna mafuta, basi usishangae mgonjwa anaambiwa akanunue kuni au atoe fedha za kuchemshia vyombo. Kwanza kuchemsha kwa kuni kamwe hakufanyi vyombo viwe salama, kwa hiyo mgonjwa anatoa fedha, na hapohapo anapata maambukizo mengine toka kwenye vifaa, sitaki kuyataja baadhi ya maabukizo kwani hali ni mbaya.
Mbali ya wizara ya afya kutoa tamko la huduma za ambulance kuwa bure.Hali halisi sivyo ilivyo kule vijijini. Mganga wa zamu atadai kwanza fedha za kuitia ambulance (voucher), baadaye atamdai mgonjwa fedha kiasi cha shillingi 10,000-15,000 eti ni ghalama ya mafuta.Ingawa ambulance inaweza kuwa ni bure , Dereva na mganga wanachikichia hizo fedha. Mara nyingi wanawatarget mama wajawazito kwani wanajua hawana jinsi na muda wa kuulizia, wapo kwenye uchungu, wamechanganyikiwa, wanataka kuokoa kichanga wao na mama yake.
Swali la kujiuliza ni je Halmashauri haziwezi kupunguza kero hizi?.Jibu ni ndiyo, zinaweza! zinaweza kabisaaa, kwani baadhi ya kero hizi zipo chini ya uwezo na udhibiti wao.
Idara ya afya katika halmshauri zinauwezo sasa wa kupanga mipango yao (health interventions) kulingana na vipaumbele na matatizo yanayo wasibu (local problems).Pia kwa kutumia their communities strenght and resources. Hiyo ni kutoka na mabadiliko ya serikali za mitaa (sectoral reforms under decentralization by devolutions ya miaka kama saba iliyopita).
Kuhusu matumizi ya tochi- Idara inauwezo wa kusambaza chemli katika zahanati zote na kuwapatia mafuta ya taa kila wanapokuwa wanawapekea gesi au mafuta ya frigi za kuhifadhia sindano za chanjo, kwa hiyo ni suala la kuongeza kabadgeti kidogo tu, baadaye wanaweza kwa kila financial year kupanga kuweka soral power katika vituo vitatu au vinne kila mwaka. Nasema ni suala la how do they allocate their resources kwenye COMPREHENSIVE DISTRICT HEALTH PLANS (CCHP) zao.
Kuhusu mabomba ya sindano, glovus ni utashi tu, hakuna sababu,ni uzembe, kutofuatilia, na njaa kali, wala sihitaji kulielezea hili.
Kuhusu vifaa vya kuchemshia. Hili ni suala gumu kidogo, lakini linawezekana. Najua hawawezi kununua modern sterilization machines kwa zahanati zote, kwanza nyingi zinatumia umeme, ambalo ni tatizo pia, lakini wanaweza kuimprovise angalau vifaa vitakavyoweza kufanya sterilization at least 80-90%. Kuna majiko ya sayari, yanatumia gesi, kuna gesi cookers kubwa sana. vyote ni kwa bei rahisi Bongo na vinaweza kutumika hata vijiji ndani kabisa. Gesi watakuwa wanarefill wanapokuwa wanawapelekea gesi za frigi za chanjo.Utashangaa kila mwaka kuna fedha nyingi za trainings on sterile procedures,mafuzo yakiisha kwaheri,wahitimu hawapewi vitendea kazi.
Suala la maji ni tatizo kubwa sana. Nalo linawezekana. Kwa kutumia nguvu za wananchi, kuchimba visima virefu au kugema na kuhifadhi maji ya mvua kwenye matank, Hii inahitaji utashi tu wa wapanga mipango wa idara ya afya katika wilaya.
Nitaendelea baadaye.....
2. Dr Ponsi anaendelea....
Uzoefu wangu mimi, unanilazimisha kutuma lawama nzito kwa wapanga mipango idara ya afya za halmashauri nyingi (Council health Management Team). hawana local criterion za kupanga mipango yao. Interventions zao nyingi zinajikita kwenye seminars, kongamano na retrainings kibao.Zaidi ya asilimia 40% ya badget ya afya inaliwa na seminars, trainings na kongamano. Sitaki kuongelea posho kwani nitakuwa nawagusa sehemu mbaya.Mbaya zaidi, trainings hizo zinajirudia kila mwaka. Hivi hao wanafunzi gani jamani?
Nilijaribu kipindi fulani kuwauliza hawa wanamipango wa idara ya afya katika wilaya yangu kwenye pre-planning meeting fulani, ni vigezo gani walitumia kuandaa zile activities. kila mtu alibaki kimya, nikaendelea kuwauliza ni matatizo gani walikuwa wakikumbana nayo kwenye utoaji wa huduma kwenye zahanati wakati wakifanya, wao wanaziita "Supportive supervisions" wanamaneno mazuri hao!eti supportive! wakasema: 1) hakuna mafuta ya taa 2)hakuna glovu na sindano 3) Poor sterilization 4) Hakuna maji NK. Nikawaambia, kwa nini sasa hakuna hata mmoja wao aliyeweka vitu hivyo kwenye mpango,kuna maana gani ya kutengeneza mpango,nini maana ya wao kwenda kufanya hiyo supportive supervision huku walikilpwa karibu shillingi 20,000 kwa siku. Jamaa wakabaki kimya, kwa kweli inauma, fedha zipo(BUSKET FUNDS & CAPITATION &COST SHARING,MTEF nk). Ingawa hazijawahi kutosha lakini zaweza kupangwa vizuri kwa maslahi ya wananchi, kwani ni zao.
Kihoja kilichonisikitisha ni kwamba kila mmoja alipewa mda wa kwenda kurudia activities zake wakiaddress vile ambavyo tulikubaliana.Wakafanya kama tulivyokubaliana, tukaingiza fedha za kutengeneza mashine za maji, kuchimba visima, kununua sterilizers na majiko ya gesi, kuongeza supliment budgetya glovus na sindano kwenye zahanati na vituo vya afya, kutenga fedha za vochers kwa wakuu wa zahanati,NK.Tukapunguza trainings zote na nyingine tukaziunganisha kama ni 1 WEEK REFRESHER TRAINING ON IMCI, tukakubaliana waingize humo na TB, MARALIA, SKIN DISEASE,nk.Tukasave fedha nyingi ambazo tulizidiverge kwenye activities tajwa hapo juu.
Mpango ukawa umekamilika, kabla ya kupelekwa mkoani, total budget ikawa imeongezwa,si unajua tena mambo ya donor dependent budget! ikabidi turudie tena kufidia nyongeza nami nikawa sipo. Unajua kilichofanyika! Waliondoa kila kitu nilichaoagiza, wakaingiza trainings zao na maposho .Nilitaka kuzimia baada ya mwaka kukuta vitu ambavyo viliondoka ndivyo vinatekelezwa na vile vya wananchi vimeondolewa.
Si lengo la ushuhuda huu kumlaumu mtu.Bali nilitaka kusema kuwa HATUNA VIPAUMBELE KATIKA UPANGAJI WA MIPANGO YETU. KILA MPANGAJI ANAJIANGALIA YEYE KWANZA ATAFAIDIKA VIPI NA MPANGO HUO. MLENGWA AMBAYE NI MWANACHI ANAKUWA KIPAUMBELE CHA TANO KAMA SI CHA MWISHO.
To conclude, I will not even question the credibility of our local governments’ planning tools. Effective planning is supposed to be supported by continuous needs assessment and evaluations of the previous and the current developmental programs. Planning without base, planning by copy and paste is like seeding in a dry land, never expect good yield. Infarct, that plan will never yield the intended outcomes. We really need a total reforms of our planning procedures and our MIND-SET.
Dr Ponsi.
0 feedback :