wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, July 12, 2009

TweetThis! Mkapa ulisahau kuwa 'ndugu wakigombana, shika jembe ukalime..."

"...wakipatana, chukua kapu ukavune!' Hakika dunia ya sasa imekuwa si ile ya kale. Siku hizi mtu anaumia barabarani na watu wanapita mbali kabisa kuleee, kwa kuogofya kusaidia na baadaye walundikiwe kesi isiyo kichwa wala mguu. Ah!

MWAKA WA BALAA: Mkapa abebeshwa msalaba Kenya - ndivyo kilivyoandikwa kichwa cha habari ambapo sehemu ya nakala ya gazeti la Majira inayopatikana kwenye mtandao inasomeka hivi:
"Kwa mujibu wa gazeti la The Nation la mwishoni mwa wiki iliyopita, Wakenya wamekasirishwa na hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Koffi Annan na timu yake akiwemo, Bw. Mkapa, kukabidhi orodha ya siri majina ya watu wanaodaiwa kuhusika kwenye machafuko ya uchaguzi mkuu uliopita nchini humo.

Imedaiwa kwamba Bw. Annan hakufanya maamuzi hayo peke yake bali kabla ya kufikia uamuzi huo mzito, aliishirikisha timu iliyofanya kazi ya usuluhishi wa mgogoro huo, akiwemo Rais Mkapa na mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Bi. Graca Machel na kwa pamoja wakaafika kukabidhi majina hayo ICC.

Uamuzi wa Bw. Annan kupeleka majina hayo ICC umewashangaza wakenya wengi na hata kuikasirisha Serikali ya nchi hiyo.

Vyama vikuu nchini humo vya Orange Democratic Movement (ODM) na kile cha National Unity, nia yao ilikuwa kumaliza tatizo hilo bila kutolewa adhabu kwa wahusika.".
Habari kamili zinapatikana hapa http://bit.ly/1uFtY

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads