wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, July 16, 2009

TweetThis! Kina Klothing Yafungua Duka Mtandaoni

Salaam kwa wadau wote wa blogu ya Nukta77.

Kina Klothing ina furaha kuwafahamisha kuwa tumefungua duka letu mtandaoni na unaweza sasa kununua Tshirt moja kwa moja kupitia www.kinaklothing.com

Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho tumetoka na kollektion inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.

Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.

Kama kauli mbiu yetu inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio tunavyotarajia kuendesha lebo yetu, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.

Tshirt hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.

Hata hivyo, katika kollektion hii ya kwanza tumeamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.

Tutembelee www.kinaklothing.com na tuambie mawazo yako.

Pia usisahau kujiunga nasi katika ukurasa wetu ya facebook (http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819) na kutufuatia katika http://www.twitter.com/kinaklothing

Kaa mkao wa kula kwa kollektion inayofuatia, Samora avenue. Iko jikoni.

Amani.Mkuki na Susan (Kina Klothing)





Nikiwa kama mdau mdogo wa blogu hii, najionea fahari kubwa kutangaza kazi za WaTanzania wenzangu kwa uhuru bila gharama wala maswali yoyote! Yeyote mwenye tangazo asisite kutumia nukta77 kuwafikia japo wawili watatu wenye kusoma blogu hii.

Ninawatakia mafanikio mema wadau wote wa Kina Klothing.

Daima pamoja!

1 feedback :

Anonymous said... Fri Aug 14, 02:15:00 AM MST  

Kwa ufupi. Kitu kimeshiba kisanii, kimapinduzi, na ki-nakshi nakshi. Ama kweli mapambano bado. Mkuki mbele kwa mbele

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads