wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, June 26, 2009

TweetThis! Video: Mhe. M. Pinda akizungumza bungeni kuhusu vifo vinavyotokana na uzazi

Vifo vinavyotokana na uzazi vinaweza kuzuilika ikiwapo nia ya kuboresha miundombinu kama vile barabara, vyombo vya kusafiria na upatikanaji wa vitendea kazi katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.
Waziri Mkuu, mhe. M.Pinda umezungumza kuwa suala hili la kupunguza na kutokomeza vifo hivi unalifahamu vyema na limekugusa. Langu moja, ninaomba (what the heck, ninaomba? nope) tunahitaji Serikali iwajibike kwa suala hili. Kauli zenu ndiyo shitaka lenu. Zitakuhukumuni.

Video hii ni kwa hisani ya Kennedy Kimaro wa blogu ya Magazeti ya Tanzania.

2 feedback :

Mzee wa Changamoto said... Sat Jun 27, 11:39:00 AM MST  

Dah!!! It's getting worse now. Si ni huyu huyu aliyesema kuhusu uwiano wa magri ya wabunge kuwa Gari moja la m'bunge ni sawa na matrekta 40? Na baada ya hapo sijasikia lolote kuhusu hili zaidi ya kusikia wakisema wanataka kuongezewa mshahara. Hivi hawa wanamchezea nani siasa hizi za kipuuzi? Hivi hawa wanadhani watu hawajui tofauti ya ujinga na busara? Hivi Mheshimiwa Waziri mkuu anastahili kujilazimisha kuonekana anajali na kuonekana anasikitika kwa yanayotokea?
HAWANA UPENDO WOWOTE NA HAKUNA LOLOTE JEMA WANALOWATAKIA WANANCHI WAO. Niliandika kuwa huu ni UJINGA 360 degrees na twahitaji kuwaelimisha zaidi. Bofya hapa kujionea http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/06/ujinga-360-degrees.html

Subi said... Sat Jun 27, 11:44:00 AM MST  

Mzee,
Dada Shally ametoa maoni juu ya habari hiikwenye Facebook, na maswali yake hayatofautiani kwa mbali na ya kwako:
Shally Hassan at 10:21pm June 26
Ni kweli serikali inatakiwa kutekeleza masuala hayo na sio kusema tu, sasa inamwambia nani? inashangaza kwani wajenzi wa barabara na hayo mambo mengine ni wao wenyewe. Pinda angewaambia Mawaziri wenzake ingekuwa bora.


nami nikamjibu na nadhani majibu hayo hayo utayaona yanaendana na dukuduku lako:
@Shally,
Naafiki kabisa swali lako la 'sasa inamwambia nani?'. Ikiwa yeye ameona, ni hatua gani alichukua kulirekebisha hilo aliloliona? Hapo sijasikia alichosema. Ina maana alikuwa akisubiri hadi kipindi cha Bunge akahadithie alichoona? Mtu makini alitakiwa aelezee jinsi alivyosaidia kuhakikisha upungufu huo umeshughulikiwa na hatua iliyofikiwa. Hii nchi inachosha, we acha tu.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads