Tahadhari: Wizi wa kimazingara [updated]
UPDATE
Wizi wa computer umekuwa tatizo kubwa hapa Bongo. Kuna mwenzetu mmoja aliibiwa laptop yake kwenye hoteli pale Chalinze. Pana hoteli fulani inaitwa Amazon, mpya mpya, huwa tunashukia hapo tukipeleka wanafunzi field. Asubuhi alitoka chumbani na kukabidhi valuables zake zote reception, ikiwa ni pamoja na laptop yake. Alivyorudi jioni akavichukua vitu vyake na kupeleka chumbani ambapo alikaa akifanya kazi na hiyo laptop. Aliamua kwenda kula kwenye restaurant ya hapo hapo hotelini kwa hiyo akafunga tu chumba na kwenda kula. Haikupita hata nusu saa anarudi laptop haipo. Alivyouliza kila mtu anasema sijui. Kwenda polisi kitu cha kwanza walichofanya ni kumpigia simu mwenye hoteli ikionesha walikuwa wanafahamiana. Walifika eneo la tukio na kuuliza uliza wala wasikague chumba chochote au kuongea na wapangaji. Mwenye nyumba akamwambia haiwezekani laptop iwe imeibiwa hapo kwake akitaka aende mahakamani. Imeishia hapo, amepeleka mahakamani lakini hategemei kupata chochote. Alikuwa na research proposal yake aliyokuwa anaimalizia kwa ajili ya PhD program anayotegemea kuanza na hakuwa na backup. Baada ya kuongea ongea na waalimu wengine wa chuo kumbe chumba hicho alichokaa funguo zake zinafunguliana na reception. Alivyotoa hizo taarifa kwa polisi wakaenda na kujaribu wakakuta ni kweli. Swali walilomuuliza ni "ULIJUAJE KUWA HIZI FUNGUO ZINAFUNGULIANA?". TUJITAHIDI KUBACK UP KAZI ZETU. Vile vile tusiweke flash drive zetu kwenye mfuko wa laptop. Mimi pia niliwahi nyolewa mkavu mkavu hivyo hivyo hapa Dar.Hii si hadithi ya kutunga au kufikirika, kisa hiki kimetokea na kimempata mkazi mmoja wa jijini Dar Es Salaam:
Hope you all fine. Jamani napenda kuwapa tahadhari wenzangu kutokana na kilichonipata Jana (sunday 31 May 2009). Ilikuwa hivi: Nilikwenda Mlimani City kufuata Salary yangu . Nilikomba kiasi chote (si mnajua pesa yenyewe kiduchu na daima huwa haitoshi). Nikaondoka bila hata kuangalia left or right kuepusha tamaa ya jengo lile.
Baada ya kujipakia ktk daladala kuelekea kwangu TABATA. niliketi seat ya dirishani na mwanamke mmoja aged kidogo yuko kama lateforties (48,49....) . Baada ya kutoka pale kufika kituo cha superstar that aged woman waved her hand usoni kwangu. Suddenly my body was heavy, my lips went more heavier . I couldn't move a hand or anything. Nilistuka kituo cha RELINI (mwananchi) that woman alinigusa begani akaniambia NASHUKA KWA HERI then kama vile nimestuka usingizini nikamwambia OK.
There after fahamu zikanirudia kutazama my handbag iko wazi wallet yenye SENT zangu imefunguliwa na hakuna sent tano. Nikawaambia abiria wenzangu "nimeibiwa". Ilibidi driver asimamishe bus kusikiliza huo wizi na ikibidi bus liende police. abiria wenzangu wakanieleza kuwa mimi na that woman tulikuwa tunazungumza vizuri muda wote kama watu tunaofahamiana na hata manaeno yangu walinisikia nikimwambia huyo woman kuwa pesa ziko LAKI NNE NA ISHIRINI. kusema kweli nilikuwa na kiasi hicho kweli na ilinibidi kukubali kuwa ni kweli nimeshaibiwa kwa ushirikiano wa hali ya juu. kila mtu mle katika daladala hakuamini kuwa ati nimeibiwa na yule SHOSTI wangu. Wengine walidhani ninataka kuwatapeli na kuwasingizia. Kumbe muda wote mimi najiona mzito kufanya chochote lakini machoni kwa wengine nilikuwa kawaida tena very cooperative. Mshahara wangu wote umeondoka kwa that style.
My advice jamani wizi huu umefikia hatua ya ajabu zaidi ambayo sikuwahi kufikiria. Tahadhari za ziada zitakazokujia usizipuuze zitakusaidia Dunia imekuwa tambara bovu. Tumuombe Mungu atusaidie
Frankly speaking NIKO CHALI sio mchezo. mwezi huu nimefulia tena bila sabuni. Inaniuma sana kuwa nitaishije this month. Yote namwamchia MUNGU naomba awalinde na nyie pia wambieni ndugu jamaa na marafiki muwapendao wakao chonjo.
4 feedback :
Pole sana na maisha ya Dar itakuwaje sasa. Kwali Dunia/TZ,Dar imeharibika. Yaani inafikia watu wanafanya hivyo. Kazi kwelikweli!!!!Asante kwa kuiweka hii taarifa hapa Da Subi.
Asante kushukuru Yasinta!
Maisha ni kujifunza na kuchukukua tahadhari katika mabaya na kulinda mazuri.
Aisee pole sana mpendwa,na mambo ya ajabu sana haya hapa Bongo jamani inabidi tuchukue tahadhari ya kufa mtu na kama hii inabidi sala za kutosha.Ni veme haya mambo yakawekwa wazi hivi ili wengine tujifunze kutokana na haya.
Umesema sawa Tina,
Tunajifunza pia kutokana na makosa na matukio ya kusikitisha.