wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, June 17, 2009

TweetThis! Serikali Tanzania yawasikiliiza Maaskofu kuhusu msamaha wa kodi

Serikali imebatilisha uamuzi wake wa kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa taasisi za dini na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na kuunda Timu Maalum itakayofutilia mianya ya matumizi mabaya ya msamaha huo.

Kutokana na uamuzi huo, Serikali italazimika kurekebisha vipengele kadhaa kwenye bajeti ya sh. bilioni 9.5 iliyosomwa wiki iliyopita bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo na kuweka vipya kwa baadhi ya maeneo ili kukidhi marekebisho hayo.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa itasaidia wabunge kupitisha bajeti hiyo kwa urahisi na kupunguza maswali magumu kwa Serikali leo jioni, wakati Bw. Mkulo atakapotoa majumuisho ya michango ya wabunge.

Akizungumza jana na waandishi wa habari nyumbani kwake mjini hapa, Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, alisema baada ya Serikali kusikia kilio cha wabunge na taasisi za dini, alikukutana na viongozi dini juzi na kukubaliana kwamba ni umuhimu wa kuendeleza msamaha huo kwa sasa huku wakimwahidi kushirikiana na Serikali kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

"Wabunge hasa wa CCM walipigia kelele suala hili na kuishauri Serikali kuangalia upya. Viongozi wa dini nao walisema hivyo, ile rai ilikuwa ya msingi, jana (juzi) nilipata fursa ya kukutana na viongozi wa dini maaskofu, alikuwepo Askofu Mokiwa (Valentino-Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania), Malasusa(Alex Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania -KKKT), Rwaichi (Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki), Katibu Mkuu wa Kanisa Anglikan Tanzania,(Dkt. Raphael Mwita), Shekhe wa Mkoa na mashekhe wengine.

"Waliisihi sana Serikali iangalie upya jambo hili, walisisitiza katika kazi zao wanasaidiwa na wahisani wa nje wanaojinyima na kwa kufanya hivyo inaweza kuwavunja moyo na kuwa na athari kubwa kwetu Tanzania. Nilimtafuta Mheshimiwa Rais nikamweleza na kumpa ushauri, akakubali akaridhia kwamba msamaha huu uendelee kama ilivyokuwa,"alisema Bw. Pinda.

Alipoulizwa ni kwa nini Serikali inaoneka kukosa uamuzi sahihi na kukubali jambo kisha kubatilisha alisema, " Ukiwa kiongozi wa Seriakli ni lazima usikilize watu unaowaongoza, Serikali ingeweza kusimamia uamuzi wake lakini baada ya kusikiliza watu wake na Rais Jakaya Kikwete, alivyomsikivu ndio maana tumeona haya katika hili tukubali kufuta kwanza, hawa viongozi wa dini nao ni viongozi wana watu wanaowaongoza,"alisema.

Alipoombwa kueleza ni kwa jinsi gani Serikali itaziba mianya ya fedha ambazo zingetokana na kufutwa misamaha hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa fedha hizo ziliingizwa katika bajeti ya trilioni 9.5 alisema;

"Tayari nimemwagiza Waziri wa Fedha kufanya kazi hiyo na leo, alinihakikishia kwamba tayari ameshafanya kazi hiyo sasa mimi siwezi kumsemea ataeleza mwenyewe,"alisema.

Alipotakiwa kueleza hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa waliobainika kutumia mwanya wa msamaha vibaya kama alivyoainisha Bw. Mkulo alipozungumza na waandishi wa habari Jumamosi iliyopita alisema;

"Bahati nzuri Viongozi wenyewe wa dini waliniomba hayo majina ili wao kwanza waanze kuwashughulikia, pia katika timu hiyo tutakayounda itawajumuisha naamini hili litashughulikiwa vizuri tu na kuziba mwanya huo.

Kuhusu muda na muunda kamili ya timu hiyo, alisema kazi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mkulo kwa kushirikina na Kamishna Mkuu wa TRA na kwamba ana uhakika ndani ya miezi miwili hadi mitatu itakuwa imekamilika.

"Kazi kubwa ya Timu hiyo itakuwa ni kuangalia njia bora zaidi ya kuziba mianya ya matumizi mbaya ya misamaha hiyo, lakini bado tunaweza kuendelea na hoja hiyo (kufuta msamaha wa VAT hata mwakani) lakini tulioni kwamba kweli si wakati wake kwa sasa,"alisema Bw. Pinda alipotakiwa kujibu swali lilihoji ni lini Serikali itadhibiti kabisa tatizo lamatumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Kuhusu swali la DECI Waziri Mkuu, alisema yeye alipitia ripoti hiyo na kumwagiza Bw. Mkulo kuitoa kwa wana habari. Kutokana na agizo hilo Waziri Mkulo aliahidi kutoa taarifa hiyo leo asubuhi kwa waandishi wa habari Ofisini kwake.

Baadhi ya Wabunge waliozungumza na Majira kwa njia ya simu walisifu na kupongeza hatua hiyo ya Serikali kukubali ushauri wao huku baadhi yao wakiionya kwamba iwe makini katika maamuzi mazito kwa kuwashirikisha wadau badala ya kujifungia na kutoa maamuzi hatari kwa Taifa.

Baadhi yao walisema bado wanasubiri kusikia kufutwa kwa misamaha ya kodi kwa kampuni zote za madini na kuongeza kwamba kipengele hicho pamoja na kile cha kuondoa kodi ya asilimia 10 kwenye mafuta, yanayotoka nje bado itamgharimu Bw. Mkulo leo iwapo hatakubali kufanyia marekebisho mapema -
 John Daniel, Majira.co.tz, Dodoma.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads