wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, June 01, 2009

TweetThis! WARNING! GROSS photos. Abambwa akichuna mbwa apate kitoweo

In the middle of the road in Kilolo, Iringa - Tanzania, a man was seen peeling and scraping off a dead dog's skin. The dog was hit by a car and died on the spot.

Mzee Mla Mbwa abambwa " LIVE" na blogu ya Francis Godwin

UMATI mkubwa wa wananchi wakazi wa Manispaa ya Iringa leo walifurika katika eneo la Kihesa Sokoni kushuhudia mkazi mmoja wa kutoka wilaya ya Kilolo ambaye alikutwa akimchuna ngozi mbwa kwa ajili ya kitoweo.
Tukio hilo la aina yake litokea majira ya saa 6 mchana katika eneo la Kihesa Sokoni katika Manispaa ya Iringa ambapo mbwa huyo alikuwa amegongwa katikati ya barabara ya Kihesa, Tumaini Iringa .
Kutokana na mzoga huu wa mbwa kubaki katikati ya barabara mkazi huyo ambaye alikuwa akinywa pombe ya kienyeji katika kilabu kimoja kilichopo jirani na eneo hilo alilazimika kunoa kisu chake na kumsogea mbwa huyo pembeni ya barabara na kuanza kumchuna ngozi huku akionyesha kuchekelea kuwa amepata mboga.

Pamoja na tukio hilo kuonyesha kuwakwaza baadhi ya watu waliofika kushuhudia tukio hilo na hata kutaka kumpiga mkazi huyo bado baadhi yao walionekana kumkingia kifua mkazi huyo kuwa kipenda roho hula nyama mbichi na kuwa hakuna sheria inayomkataza mkazi huyo kumla mbwa huyo.

Bw Salum Omary na Sarah Kalinga wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio walisema kuwa wao walipata kushuhudia mbwa huyo akigongwa na daladala inayofanya safari zake kati ya Tumaini - Mwangata na kuwa baada ya kugongwa mbwa huyo aliendelea kubaki barabarani kwa zaidi ya saa moja huku wapita njia na magari yakionyesha kumkwepa mbwa huyo hadi alipofika mkazi huyo na kumwondoa barabarani na kuanza kumchuna ngozi.
"Ujue alipoanza kumvuta mbwa huyu pembeni mimi na huyo mwenzangu tulikuwa tukishuhudia ...lakini tulijua labda mwenzetu huyo ni chizi ...lakini baadaye tulibaini kuwa ana akili timamu na kuwa baada ya kutusalimia na kutaka tumwonyesha mwenye mbwa kwanza ila aweze kuomba mbwa huyo kwa ajili ya nyama" alisema Bi Kalinga.

Kuwa kutokana na mwenye mbwa huyo kutofahamika haraka mzee huyo ndipo alipoanza kumchuna ngozi kwa madai kuwa isije nyama yake ikaharibika kwa kucheleweshwa kuchunwa ngozi .

Hata hivyo alisema kuwa upande wake alikuwa akisikia tu kuwa wapo watu wanaokula mbwa ila kutokana na tukio hilo amepata kuamini kuwa kweli mbwa ni kitoweo kwa baadhi ya watu.

Kwa upande wake Bw Omari alisema kuwa pamoja na baadhi ya watu kujaribu kumtakaza mzee huyo kumchuna ngozi mbwa huyo ila bado alionekana kulazimisha kuendelea kuifanya hivyo huku akitishia kuwarushia mbwa huyo kama njia ya kuwatisha ili wakimbie na kumwacha aendelee kumchuna ngozi.

Kwa upande wake mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Iddy Kisalanzakulima (55) alisema kuwa wapo watu wanaofanya mambo ya kinyama zaidi ila hawasemwi ila inakuwaje watu wakimshangaa kwa yeye kula mbwa wakati mbwa ni mnyama kama walivyo wanyama wengine.

Alisema kuwa moja ya nyama ambazo amekuwa akipendelea zaidi ni pamoja na nyama hiyo ya mbwa na kuwa kutokana na wengi kuogopa kula binafsi amekuwa akiifaidi zaidi .Hata hivyo hakuweza kuweka wazi zaidi kama nyama hiyo ya mbwa amekuwa akiila peke yake ama amekuwa akiiuza mitaani .
" Nimesema kuwa hii ni nyama kama nyama nyingine sasa sio kazi yako kujua kama nitakwenda kuiuza ama kuila ila wapo wenzangu ambao wanakula nyama hii na ni wapenzi wakubwa hata wakisikia leo nimebahatika kupata kitu kama hiki wapapenda sana.... mbona wewe umekuja na kunipiga picha hapa kwani mimi nimekuuliza unakwenda kuziuza ama kuziweka kwako "alihoji mzee huyo huku ekiendelea kumchuna mbwa wake .

Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kufanya mahojiano na mmoja kati ya madaktari binafsi mkoani Iringa akiwemo Bw. Mwingongo Kapwani ambaye ni mganga mkuu wa Zahanati ya Makosa mjini hapa alisema kuwa japo hajawahi kufanya utafiti wa kina juu ya madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtu kula nyama ya mbwa ila bado nyama hiyo inaonyesha haina madhara yoyote .

" Sijafanya utafiti wa kina sana ila nyama hii ni kama nyama nyingine inaonyesha haina madhara yoyote kwani kama nchi za Mashariki ya Mbali wamekuwa wakila kwa wingi sana nyama za mbwa ila kwetu huku mtu ukikutwa unakula mbwa watu wanakushangaa".
Hata hivyo kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Iringa Dk. Oscar Gabone alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu juu ya ulaji wa nyama ya mbwa kama una madhara katika mwili wa binadamu alisema hakuna kitu kama hicho na kuwa mbona WaChina wanakula sana nyama hiyo ya mbwa na hawapati madhara yoyote.

5 feedback :

Egidio Ndabagoye said... Mon Jun 01, 10:06:00 AM MST  

Mzee Iddy hana kosa lolote naona kuna wananchi wenye hasira zao walitaka kumpa kipigo.Kama haina madhara kwa mlaji basi ruksa!

Anonymous said... Tue Jun 02, 06:47:00 AM MST  

Mbona watu wanamshangaa. anaweza kuwa ni mgonjwa wa akili ikiwa hiyo kitoweo si jambo linalokubalika huko. Kwanza kwa nini hakumchukua mbwa mzima mzima mpaka afanye uchunaji barabarani. Halafu ao watoto wanatafuta nini hapo. Nji hii bwana.

Subi Nukta said... Tue Jun 02, 07:31:00 AM MST  

@ Dio, haina neno kuliwa lakini hata kibudu? haijapimwa hiyo halafu, kama gonjwa je? akitoka na kichaa cha mbwa hapo au magonjwa ya mbwa? ndo mafua ya mbwa tena!

@ Anon, nadhani watoto wanashuhudia sinema ya bure, si unajua tena utoto kushangaa kila kitu, ndivyo walivyo. Ila hilo la kumchunia barabarani, sijui, pengine imezoeleka sasa anaona afiche ili iweje?

Anonymous said... Wed Jun 03, 09:50:00 PM MST  

Huu ni ujinga wa huyu mzee si sifa anavyofanya dawa apate kipigo hapo, Hata kama kufa njaa si hivyo tena kuokota mizoga ya wanyama wasioliwa na kuwachuna njiani hadharani bora nile majani kuliko mzoga wa mbwa, halafu kwa nini asiuchukue shemeu ya mbali na watu akafanya anavyotaka au ni ushirikina huu, Pumbavu sana huyu mzee na ni mchavu wa kupindukia mi nikimuona nitampa kibano.

Anonymous said... Thu Jun 04, 04:59:00 PM MST  

Nyama ni nyama tu bwana bora iwe na chumvi. By the way anawasaidia wafanyakazi wa mamlaka za usafi katika huo mji maana mara zote hao huwa ni wazembe, huyo mbwa angekaa hapo kwa wiki nzima! And lastly he is a free citizen in a free country.

Godlove,
Shalombroz.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads