wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, June 25, 2009

TweetThis! Ninyi waandishi wa habari wazembe hivi, mna matatizo gani?

Kichwa cha habari kinasomeka: Dereva afa akigongana na basi

Hivi kweli ninyi waandishi (baadhi) wa habari ambao kila leo mnalalamika kuwa jamii haiwaheshimu, mnatarajia heshima itoke wapi il hali wenyewe mnaandika 'hovyo hovyo'? utumbo mtupu.
Uandishi gani huu wa kukurupuka kubandika habari bila marejeo? Yaani 'bora liende' kwa kuwa unataka kuwa wa kwanza kuripoti au jina lako litokeze hewani upatiwe ndururu zako ukanywee ulabu.
Mhariri wa gazeti anakuwa wapi wakati habari inaandaliwa namna hii hadi kuchapishwa?
Mna nini ninyi lakini?
Huu si ugonjwa bali uzembe na kutokujali.
Huwezi ukawa umesoma na unaiheshimu taaluma yako kisha ukaandikie watu ati dereva afa akigongana na basi; Tangu lini binadamu alianza kufanya migongano na mabasi? Dereva alikuwa akigongana vipi na basi? - walao uelezee kwenye habari tujue, aaa wapi, huelezei. Mnakera ninyi kwa uandishi wenu huu wa 'hovyo hovyo', basi tu.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads